Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

James Brown Sio Mfalme wa Soul tu, Bali Mfanyabiashara wa Maono 💰✈️

James Brown, anayejulikana kama “Godfather of Soul,” hakuwa tu gwiji wa muziki tu bali pia alikuwa kinara katika biashara na kujenga utajiri kwa Wamarekani wenye asili ya afrika.

Mwisho mwa miaka ya 1960, Brown aliripotiwa kuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza na mara nyingi hutajwa kama marekani Mweusi wa kwanza kumiliki ndege binafsi (private jet). Wakati huo safari za kibiashara zilikuwa bado na vikwazo vya ubaguzi na ukosefu wa fursa, kumiliki ndege kulimaanisha uhuru, mafanikio na udhibiti wa ratiba za kazi yake.

Ndege hiyo ilimuwezesha yeye na bendi yake kufanya ziara kwa ufanisi zaidi, kupiga show katika miji tofauti kwa muda mfupi, na kuepuka changamoto nyingi ambazo wasanii wengi Weusi walikumbana nazo walipokuwa safarini.

Zaidi ya anasa, ununuzi huo uliakisi falsafa yake ya umiliki na kujitegemea. Brown aliwekeza katika vituo vya redio, mali isiyohamishika na biashara mbalimbali, akihamasisha uwezeshaji wa kiuchumi kwa jamii ya Weusi kabla hata haijawa mjadala mkubwa.

Ndege yake binafsi haikuwa tu alama ya utajiri bali ilikuwa ishara ya uhuru, mamlaka juu ya maisha yake, na uwezo wa kujenga utajiri kwa masharti yake mwenyewe.

1772045839509.jpg
 
Mnamo mwaka 2003, msanii Michael Townsend pamoja na marafiki zake walifanya moja ya mambo ya kushangaza zaidi kuwahi kufanyika mjini. Walijenga kwa siri ghorofa ya takriban futi za mraba 750 ndani ya Providence Place Mall iliyopo Providence, nchini United States.

Wazo hilo lilianza baada ya maendeleo makubwa ya jiji kumfanya Townsend kupoteza sehemu aliyokuwa akiishi pamoja na wasanii wenzake. Akihamasishwa na tangazo la mall lililosema kuhusu “utajiri wa uzoefu wa kununua,” aliamua kulichukulia kwa vitendo. Wakati ujenzi wa mall ukiendelea, aligundua sehemu iliyojificha ambayo haikutumiwa na haikuonekana na umma wala walinzi.

Kwa kipindi cha miaka minne, kundi hilo liliingiza vifaa taratibu bila kugundulika. Walijenga ukuta kwa mawe ya zege, wakaweka mlango wenye kufuli, na wakaweka samani walizonunua mitumba ikiwemo sofa, meza ya chakula na kabati la vyombo. Hata waliunganisha umeme wa mall ili kuendesha taa na PlayStation.

Mchana waliishi maisha ya kawaida kama watu wengine, lakini usiku walirudi kwenye “nyumba yao ya siri” ndani ya mall. Ingawa hapakuwa na maji ya bomba, walitumia vyoo vya mall na kununua chakula kwenye food court.

Hatimaye mwaka 2007 walinzi waligundua ghorofa hiyo ya siri. Miaka kadhaa baadaye, hadithi hiyo imerudi kuwa maarufu tena baada ya kutolewa kwa filamu ya kumbukumbu (documentary) ya mwaka 2025 inayoonyesha picha ambazo hazijawahi kuonekana za maisha yao ndani ya kuta za mall.

1772070628680.jpg
 
HISTORIA YA WIMBO USINIPITE MWOKOZI. Tenzi namba 10

Wimbo huu wa usinipite ni moja kati ya nyimbo za kikristo maarufu sana Duniani. Na wimbo huu unaimbwa Na madhehebu karibu yote. Ni wimbo wa maombi, una ujumbe uliotulia, Na una tafakari itakayokuvuta kwa Mungu moja kwa moja.

Mwandishi wa wimbo huu maarufu anaitwa FRANCES JANE CROSBY na alizaliwa kaunti ya Putnam,New York,March 24,1820 na kufariki katika umri mwema wa miaka 95 mwaka1915.

Majuma kati ya sita hadi nane tu, baada ya kuzaliwa Daktari asiye na ujuzi alimfunika macho na plasta ya kemikali kimakosa, kitendo kilichomsababishia upofu wa kudumu. Upofu alioishi nao tangu akiwa Na wiki 6 mpaka maisha yake yote aliishi gizani, akuweza kuona tena, Na aliishi miaka 95. Kwa makosa ya daktari yalimsababishia asione maishani.

Pamoja na upofu aliokuwa nao bado Fanny Crosby aliweza kugundua kuwa alikuwa na karama ya kipekee ambayo Mungu alimjalia na alifurahia sana kuitumikia karama yake ya utunzi wa Nyimbo za tenzi na injili na mara nyingi alipendelea kusema,"Nina vitu vya thamani sana ndani yangu"

Alipokuwa na miaka tisa tu,aliandika maneno yafuatayo:
"Ni jinsi gani nafsi yangu ilivyo na furaha,Ingawa sioni,
Nimeridhika kuwa katika dunia hii, Nitaishi kwa furaha,
Ni baraka ngapi ninazifurahia,
Watu wengine wamezikosa?.
Kulia na kujuta Kwasababu ya upofu?,
Sitaweza,na wala sitathubutu."

Alipokuwa na umri wa miaka 15 alijiunga na taasisi ya watu wasioona ya New York, rekodi yake chuoni ilikuwa nzuri kiasi kwamba uongozi wa chuo ulimbakisha ili awe mwalimu pale chuoni,alidumu kwenye taasisi hiyo kwa miaka 11 akifundisha.

KISA CHA WIMBO

Mwaka wa 1868 William Doane mtunzi wa muziki na mfanya biashara maarufu wa Cincinnati,Ohio, Marekani , alipenda kuboresha kazi zake za utunzi kwa kushirikiana na watu wenye vipaji vya utunzi wa Mashairi ya nyimbo hivyo akamwomba Fanny Crosby kutunga Mashairi ya Wimbo utakaoanza na Usinipite Mwokozi .

Kazi hii ilimchukua Fanny Crosby majuma kadhaa mpaka siku moja alipokwenda kwenye gereza moja karibu na vitongoji vya Manhattan,New York kuhudumia wafungwa kwenye vipindi vya ibada,Ndipo aliposikia mmoja. wa wafungwa akipaza sauti na kusema ,“Bwana Mwema!Usinipite! Usinigeuzie mgongo,Nikumbuke" Mfungwa huyo alikuwa aliwaita wale wahudumu au askari wa magereza waliokuwa gerezani humu ili asije akasahauliwa.

Kilio hiki cha huyu mfungwa kilimwingia moyoni na kujaa kwenye fikra zake na kuwaza ni kwa namna gani wafungwa hawa walikuwa ni watu waliosahauliwa na jamii na kutohesabika kama watu wenye umuhimu.

Crosby alitafakari umuhimu wa kilio cha mfungwa huyu aliyekuwa akilia kwamba Bwana amkumbuke. Akawaza jinsi ambavyo watu wanavyoweza kumlilia Mungu Na pengine Mungu akafanya kwa wengine Na akawaacha wao. Ndipo alipoweza kupata wepesi wa kutiririka Mashairi Haya, kwamba siku Yesu atakapokuja Na majibu ya wengine basi namimi asinipite. Na baada ya kuyaandika akamkabidhi Bwana William Doane ili atengeneze muziki ambao ndiyo unatumika mpaka leo.

Hii ilikuwa ni kolabo yao ya kwanza na baada ya hapo waliweza kushirikiana kuimba nyimbo zingine nyingi, Fanny Crosby katika uhai wake alifanikiwa kuandika tenzi 8,000, nyimbo za kawaida 1,000 vitabu vinne vya Mashairi na vitabu viwili vya historia yake vilivyouzwa sana, mojawapo ya nyimbo alizoandika ni pamoja na "NDIYE DHAMANA YESU WANGU"

Wimbo huu wa "Usinipite Mwokozi" ulichapishwa rasmi mwaka wa 1870 kwenye orodha ya nyimbo za devotion na ulipata zaidi umaarufu baada ya kutambulishwa na L.Moody na Ira.D.Sankey kwenye mikutano yao ya uamsho huko London,Uingereza.

na kutokana na maelezo ya Dr.Young huu ni wimbo wa kwanza wa Fanny Crosby uliopata sifa nyingi Ulimwengu ni kote.

Haya ndiyo Mashairi ya wimbo
"USINIPITE MWOKOZI"

1. Usinipite Mwokozi,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

Yesu,Yesu,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

2. Kiti chako cha rehema,
Nakitazama;
Magoti napiga pale,
Nisamehewe.

3. Sina ya kutegemea,
Ila Wewe tu;
Uso wako uwe kwangu;
Nakuabudu.

4. U Mfariji peke yako;
Sina Mbinguni,
Wala duniani pote,
Bwana mwingine.

#ToGodBeTheGlory #FollowJesusView attachment 3547018
Pass me not o gentle savior
Hear my humble cry
While on other though at calling
Do not pass me by😍
 
Huwa natamani sana ni heri ningezakiwa miaka ya nyuma kabisa ili mwaka kama huu ningekua mzee kabisa...

Huwa naonea wivu sana watu wana a zamani.
Napenda sana life ya zamani na nachukia sana hi life ya sasa.

Natamani niende nikaishi mashambani huko mi kazi yangu iwe kulima tu..

Natamani sana sana sana natamani ile life. Ya 1900s...

Nawezaje kwenda mashambani nikajifiche huko nipate kipande cha ardhi maisha yaanze,

Niwe na acces ya
Umeme na Internet tuuu
Mbona inawezekana! Mfano mi mzee wangu alirudi anaishi kule analima na humwambii kitu! Tulishaongea mpaka basi ila huwa anakuja town kila baada ya week mbili au mwezi! Ukiamua unaweza vzr tu! Kuna vijiji bado vina mambo ya kizamani kabisa!
 
#makinikiayahabari: NYERERE NA KARUME WALIPOCHEZESHA MECHI YA SOKA BAINA YA VIONGOZI WA SERIKALI NA WANADIPLOMASIA

Rais Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanganyika, mnamo Jumapili Mei 10, 1964, alichezesha mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu kati ya Viongozi wa Serikali ya Tanganyika na wanadiplomasia, katika Uwanja wa Ilala, jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 0 - 0, lakini ikaacha kumbukumbu ya pekee ya uongozi uliokuwa karibu na wananchi.

Kipindi cha pili cha mchezo huo kilichezeshwa na Abeid Amani Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar, hatua iliyoonesha mshikamano wa kisiasa na kijamii katika siku za mwanzo za Muungano.


View: https://www.facebook.com/share/v/1FHDkBGAwa/
 
Mbona inawezekana! Mfano mi mzee wangu alirudi anaishi kule analima na humwambii kitu! Tulishaongea mpaka basi ila huwa anakuja town kila baada ya week mbili au mwezi! Ukiamua unaweza vzr tu! Kuna vijiji bado vina mambo ya kizamani kabisa!
Seran ebu naaomba nipe code naanzaje anzaje..
Sipendi maisha ya mjini najikuta nachukia sana, na sio sababu ni magumu hapana ila sipo comfortable sitaki nowe lazy kama sasa nataka niwe mtu kazi kazi ili niimarike kiafya..

Sitaki mambo ya mchanganyiko na watu... Napenda sana ile life napenda sana.

Niliwahi experience mara moja tu tena nikiwa shule ya msingi kule kivinje.

Asbhi ratiba ni kwenda shule.
Mchana unardi unakula unaenda baharini.

Usiku unakula unakaa nje kwa mbalamwezi..

Maisha kama haya pia yapo hapo pwani maeneo ya mkuranga..
Ila kingine napenda sana sehemu za bardi kama njombe, iringa, moshi na kwengine

Ningesema na mbeya ila tatizo mbeya nimekaa sana ila naona kabisa kule sipo comfortable labda faza ahame mbeya kule ndo takua comfortable...

Kuna watu wanakuaga na nyumba shambani huko na hamna mtu wa kukaa yaan unapata nafasi kama hiyo mi sirudi mjini kabisa
 
Seran ebu naaomba nipe code naanzaje anzaje..
Sipendi maisha ya mjini najikuta nachukia sana, na sio sababu ni magumu hapana ila sipo comfortable sitaki nowe lazy kama sasa nataka niwe mtu kazi kazi ili niimarike kiafya..

Sitaki mambo ya mchanganyiko na watu... Napenda sana ile life napenda sana.

Niliwahi experience mara moja tu tena nikiwa shule ya msingi kule kivinje.

Asbhi ratiba ni kwenda shule.
Mchana unardi unakula unaenda baharini.

Usiku unakula unakaa nje kwa mbalamwezi..

Maisha kama haya pia yapo hapo pwani maeneo ya mkuranga..
Ila kingine napenda sana sehemu za bardi kama njombe, iringa, moshi na kwengine

Ningesema na mbeya ila tatizo mbeya nimekaa sana ila naona kabisa kule sipo comfortable labda faza ahame mbeya kule ndo takua comfortable...

Kuna watu wanakuaga na nyumba shambani huko na hamna mtu wa kukaa yaan unapata nafasi kama hiyo mi sirudi mjini kabisa
Kama unaweza unanunua shamba eneo la pembeni ya mji kidogo unatengeneza hayo maisha unayoyataka! Sio lazima urudi vijijini kabisa.. ila kama unataka vijiji ni vingi sana unaangalia miji unayoweza kuimudu unaenda unaanza maisha huko na unaweza fanya kilimo na ufugaji, unaoa wake zako wanne na watoto kama wote basii🤭
 
Kama unaweza unanunua shamba eneo la pembeni ya mji kidogo unatengeneza hayo maisha unayoyataka! Sio lazima urudi vijijini kabisa.. ila kama unataka vijiji ni vingi sana unaangalia miji unayoweza kuimudu unaenda unaanza maisha huko na unaweza fanya kilimo na ufugaji, unaoa wake zako wanne na watoto kama wote basii🤭
Naenda kule kilwa ndani ndani kuchukua vitoto vidogo vidogo vile aiseeee umenikumbusha kitu Iseee
 
Back
Top Bottom