Tumeudharau ugonjwa wa Corona kwa kukosa Maarifa na itakuwa inaondoa mmoja mmoja?

Tumeudharau ugonjwa wa Corona kwa kukosa Maarifa na itakuwa inaondoa mmoja mmoja?

Amani iwe kwenu wapendwa katika bwana.

Wakati tukiendelea kuomboleza msiba wa Jemedari wetu Dkt Magufuli, tuna kila sababu ya kutafakari sana kama taifa. Haiwezekani tupoteze watu maarufu na wakubwa hapa nchini kwa kipindi kimoja, sababu ya kupoteza hawa viongozi zinatajwa kuwa ni chronic illnesses. Je, tunasahu kua huyu Kovidi ndio anawaondoa wenye Chronic illnesses? Kuna hata mmoja tuliyeambiwa kafa kwa Covid-19? Tutajuaje wakati halisemwi hili ni siri?

Ni kweli Mungu hupanga vifo lakini kwanza vifo hutangulia na sababu ndipo Mungu atume malaika wake kuja kubeba roho zetu. Tulipewa maarifa tuyatumie kupambana na mazingira lakini sasa huenda mazingira ndio yanatuzidi maarifa tunabaki na vilio kila kukicha.

Hivi tungekuwa strict kujikinga na COVID-19 100% tukachukua tahadhari katika kila kipengele kwa mujibu wa maelekezo ya wataalam na WHO mnafikiri leo hii tungekua na hamaki kila mitaa tunakopita au taifa sasahivi lingekuwa na utulivu wa aina gani?

Kuchukua tahadhari siyo lazima Lockdown wala si chanjo ya Mabeberu. Tahadhari tuliyokuwa nayo mwaka jana ilitosha sana kupunguza maambukizi na wala leo tusingekua na hamaki mitaani.
Tumepuuzia hili, timekimbizana kwenye njia za kienyeji au asili ambazo ni njia za pata potea kuliko za kitaalam. Tumeshindwa kuyatumia maarifa ipasavyo hii hali itatutesa sana.


Mwisho nawatakieni mwisho mwema wa wiki, tuchukue tahadhari binafsi kwa kujali afya zetu na familia zetu. Apumzike kwa amani Jemedari wetu JPM.[emoji120][emoji120]
Every man/woman for himself/herself, God for us all.
 
Hapana hawezi kufa kizembe mfano mfano wa Ngono zembe Dada
Tema mate Chini Kaka.. Usimneneee Mama wa mwenzio Kifo naamini hata wewe Hutopenda Mtu amtabirie Mama yako Kifo. Japo tunajua wote Tutakufa ila Kufiwa kunauma Mno.
 
Tema mate Chini Kaka.. Usimneneee Mama wa mwenzio Kifo naamini hata wewe Hutopenda Mtu amtabirie Mama yako Kifo. Japo tunajua wote Tutakufa ila Kufiwa kunauma Mno.
Uzembe unaua Ngono zembe inaua kutovaa Barakoa kunauwa
 
Corona ni vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku
 
Hao Wazungu wenye maarifa mbona Corona inawasomba kwa maelfu kila siku? Ingia kwenye mtandao wa worldometer uone jinsi maelfu wanavyoambukizwa Corona kila siku huku wamevaa barakoa!!
We mwenyewe hautoi takwimu embu tupe takwimu za kwako kwanza
 
Hao Wazungu wenye maarifa mbona Corona inawasomba kwa maelfu kila siku? Ingia kwenye mtandao wa worldometer uone jinsi maelfu wanavyoambukizwa Corona kila siku huku wamevaa barakoa!!
current statistics zinaonyesha gralh zinazidi kushuka since establishment ya chanjo.
kinacho wasumbua wao kwa sasa ni speed ya maambukizi ni kubwa kuliko speed ya ugawaji chanjo.

atleast wao wameonyesha juhudi. sisi tumechukua hatua gani kupambana na hili janga?
 
IMG-20210326-WA0122.jpg
 
Hebu nambie tu tangu walipoanza kuchukua hizo tahadhari, ni nchi gani angalau moja tu duniani imefanikiwa kudhibiti kusambaa kwa maambukizi na vifo vya UVIKO_19 na sasa wako salama kabisa. Ahsante
Australia, Newzealand, iceland, vietnam hizi ni baaadhi ya nchi ambazo zilifanya vizuri.. na zinafanya vizuri mpaka sasa kudhibit covid.
kilicho wabeba ni kuchukua hatua mapema.
 
Sikatai na hoja zako lakini nikukumbushe tuu hata hizo nchi bado watu wanaangaia hivyo kwa huku kwetu acha tutumie head immunity system kutokana na hali yetu, kikubwa wale wenye hizo changamoto wachukue tahadhari maani inaonesha kwa kiasi kikubwa wao ndio wahanga wakubwa
Huwezi uka compare wao na kwetu.
wao wanahesabu sisi hatuhesabu. there is not actual comparison.
heard immunity haifanyi kazi kwa magonjwa yote. sweden na india zikiwa ni moja ya nchi ambao walitaka kufanya hii kitu.
leo hii wanapumulia mashine.

current world statistics inaonyesha maambukizi kushuka kwa kasi. kuliko mwanzoni ambapo hakukuwa na suluhisho lolote.
 
Australia, Newzealand, iceland, vietnam hizi ni baaadhi ya nchi ambazo zilifanya vizuri.. na zinafanya vizuri mpaka sasa kudhibit covid.
kilicho wabeba ni kuchukua hatua mapema.
Na embu nambie kwan wimb la pili na la tatu si limekuja baada ya watu kuchukua tahadhari, mbona halijabadili chochote. Au ndo kama ukishawah ndo umewahi ukichelewa hata ufanye nn dude haliwez kudhibitiwa?
 
Afadhari Wamarekani wanatoa takwimu za maambukizi ya Covid-19,sasa huku tangu April mwaka jana,hatujatoa takwimu zozote kuhusiana na maambukizi ya Covid-19.
Kwa hiyo unatambuaje kama wao wameathirika kuliko sisi?.
Maanake Tanzania hata kutaja neno Corona ni kama siri fulani vile,badala yake umeanzishwa msamiati wa changamoto za kupumua au nemonia.
Njia nyepesi ya kujua athari kwetu ni kujiuliza, ww umeshakufa??? Ukijua hilo ndo utaelewa.
 
Back
Top Bottom