Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Msifie mwanafunzi shuleni uone atakavyofanya vizuri zaidi. Msifie mke wako au mme wako uone jinsi upendo wake utakavyoongezeka kwako. Isifie timu yako ya mpira, uone kama haitacheza vizuri zaidi...
Kitabu cha Mwanzo 1:27 kinatufundisha kuwa "Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake." Ndio sababu ndani yetu kila mtu ana hamu ya kuthaminiwa, kutazamwa na kutiwa moyo—kama Baba yetu wa mbinguni anavyofurahia tukimsifu.
Wanaotuongoza katika jamii, nao pia wanafurahia sana wakipongezwa na kutiwa moyo badala ya kuambiwa kasoro na udhaifu tu. Kukiri mema wanayofanya si 'uchawa.' Ni mapenzi ya Mungu kabisa.
Kitabu cha Wafilipi 4:8 kinatuambia:
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Tukijenga tabia ya kuonyesha shukrani na kutambua mazuri yanayofanywa na wengine, tutapunguza sana migongano katika jamii.
Mtu aliyebuni jina "opposition parties" au vyama vya upinzani, nafikiri ni shetani kabisa, kwa sababu shetani ni mpinzani tangu mbinguni. Alikuwa malaika mzuri lakini akaingiwa na kiburi na kuamua kumpinga Mungu. (Isaya 14:13-14). Jina "upinzani" linaleta mafarakano badala ya maelewano. Linafanya walio katika vyama vya upinzani wawaze tu kukosoa na kupinga kila kitu. Tutafakari upya jina hilo.