Hata wakiteka kuua ndugu zetu tuwasifu?Tusisubiri mtu aondoke duniani ndio tuanze kutaja mema yake kama wengi wanavyofanya kwenye misiba.
Mungu anahitaji kusifiwa!Msifie mwanafunzi shuleni uone atavyofanya vizuri zaidi. Msifie mke wako au mme wako uone jinsi upendo wake utakavyoongezeka kwako. Isifie timu yako ya mpira, uone kama haitacheza vizuri zaidi...
Kitabu cha Mwanzo 1:27 kinatufundisha kuwa "Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake." Ndio sababu ndani yetu kila mtu ana hamu ya kuthaminiwa, kutazamwa na kutiwa moyo—kama Baba yetu wa mbinguni anavyofurahia tukimsifu.
Wanaotuongoza katika jamii, nao pia wanafurahia sana wakipongezwa na kutiwa moyo badala ya kuambiwa kasoro na udhaifu tu. Kukiri mema wanayofanya si 'uchawa.' Ni mapenzi ya Mungu kabisa.
Kitabu cha Wafilipi 4:8 kinatuambia:
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Tukijenga tabia ya kuonyesha shukrani na kutambua mazuri yanayofanywa na wengine, tutapunguza sana migongano katika jamii.
Mtu aliyebuni jina "opposition parties" au vyama vya upinzani, nafikiri ni shetani kabisa, kwa sababu shetani ni mpinzani tangu mbinguni. Alikuwa malaika mzuri lakini akaingiwa na kiburi na kuamua kumpinga Mungu. (Isaya 14:13-14). Jina "upinzani" linaleta mafarakano badala ya maelewano. Linafanya walio katika vyama vya upinzani wawaze tu kukosoa na kupinga kila kitu. Tutafakari upya jina hilo.
Soma tena Wafilipi 4:8 kwa makini; halafu ukumbuke kuwa sifa mojawapo ya mtu mwenye upendo ni kwamba hahesabu mabaya.Hata wakiteka kuua ndugu zetu tuwasifu?
Wewe unayekosoa matumizi ya "Nili" na "Tuli" bado na wewe unatumia "USITUHUSISHE" Ungesema Usini... ningekuelewa. Ndio shida ya upinzani. Kila kitu kupinga tuNafikiri umekosea kutype - au pengine haujui bado matumizi ya "Nili" na "Tuli".
Hizo ni hisia zako na maoni yako binafsi - Usituhusishe.
TANU na ASP vilikua vyama pinzani dhidi ya mkoloni. Kwa andiko lako la leo, Nyerere alikosea kupinga mamlaka za wakoloni maana maandiko yanasema:Msifie mwanafunzi shuleni uone atakavyofanya vizuri zaidi. Msifie mke wako au mme wako uone jinsi upendo wake utakavyoongezeka kwako. Isifie timu yako ya mpira, uone kama haitacheza vizuri zaidi...
Kitabu cha Mwanzo 1:27 kinatufundisha kuwa "Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake." Ndio sababu ndani yetu kila mtu ana hamu ya kuthaminiwa, kutazamwa na kutiwa moyo—kama Baba yetu wa mbinguni anavyofurahia tukimsifu.
Wanaotuongoza katika jamii, nao pia wanafurahia sana wakipongezwa na kutiwa moyo badala ya kuambiwa kasoro na udhaifu tu. Kukiri mema wanayofanya si 'uchawa.' Ni mapenzi ya Mungu kabisa.
Kitabu cha Wafilipi 4:8 kinatuambia:
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Tukijenga tabia ya kuonyesha shukrani na kutambua mazuri yanayofanywa na wengine, tutapunguza sana migongano katika jamii.
Mtu aliyebuni jina "opposition parties" au vyama vya upinzani, nafikiri ni shetani kabisa, kwa sababu shetani ni mpinzani tangu mbinguni. Alikuwa malaika mzuri lakini akaingiwa na kiburi na kuamua kumpinga Mungu. (Isaya 14:13-14). Jina "upinzani" linaleta mafarakano badala ya maelewano. Linafanya walio katika vyama vya upinzani wawaze tu kukosoa na kupinga kila kitu. Tutafakari upya jina hilo.
Asante kwa maoni yako uliyoyaandika kwa Kalamu NzitoTANU na ASP vilikua vyama pinzani dhidi ya mkoloni. Kwa andiko lako la leo, Nyerere alikosea kupinga mamlaka za wakoloni maana maandiko yanasema:
"Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana Hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu." Warumi 13:1
Nimekupa andiko la Flp 4:8 linaloelezea mambo tunayopaswa kusifia. Sikusema tusifie ukoloni. Nikaeleza tena kwamba sio vizuri wapinzani wakapinga tu kila kitu kwakuwa wanaitwa wapinzani. Nyerere hakupinga kila kitu maana hata yeye alifurahia kupata elimu katika shule za wakoloni zilizomfanya kuwa mahiri katika lugha ya kiingereza. Katika uzi mwingine nimeeleza njia iliyo bora ya kutoa maoni kwa wakuu. Sijui kama tuko pamoja.Kwa Tanzania, Nyerere ndiye muasisi wa upinzani maana aliwapinga wakoloni. Kwa andiko lako, Nyerere alipaswa kuwasifu wakoloni kwa Kujenga shule, barabara, vituo vya afya na reli.