Tanzania Norway
JF-Expert Member
- Oct 9, 2022
- 338
- 658
Basi ngoja tuwasifie fisiemu kuwa ni a ni wateaji wazuriMsifie mwanafunzi shuleni uone atakavyofanya vizuri zaidi. Msifie mke wako au mme wako uone jinsi upendo wake utakavyoongezeka kwako. Isifie timu yako ya mpira, uone kama haitacheza vizuri zaidi...
Kitabu cha Mwanzo 1:27 kinatufundisha kuwa "Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake." Ndio sababu ndani yetu kila mtu ana hamu ya kuthaminiwa, kutazamwa na kutiwa moyo—kama Baba yetu wa mbinguni anavyofurahia tukimsifu.
Wanaotuongoza katika jamii, nao pia wanafurahia sana wakipongezwa na kutiwa moyo badala ya kuambiwa kasoro na udhaifu tu. Kukiri mema wanayofanya si 'uchawa.' Ni mapenzi ya Mungu kabisa.
Kitabu cha Wafilipi 4:8 kinatuambia:
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Tukijenga tabia ya kuonyesha shukrani na kutambua mazuri yanayofanywa na wengine, tutapunguza sana migongano katika jamii.
Mtu aliyebuni jina "opposition parties" au vyama vya upinzani, nafikiri ni shetani kabisa, kwa sababu shetani ni mpinzani tangu mbinguni. Alikuwa malaika mzuri lakini akaingiwa na kiburi na kuamua kumpinga Mungu. (Isaya 14:13-14). Jina "upinzani" linaleta mafarakano badala ya maelewano. Linafanya walio katika vyama vya upinzani wawaze tu kukosoa na kupinga kila kitu. Tutafakari upya jina hilo.
Ndugu yangu MastaKiraka tafakari tena uamuzi wako.Ndio maana niliamua kuachana kabisa na mambo ya mungu kwa sababu ni upuuzi puuzi tu
Mungu ni Mtakatifu, Mwenye haki na mwenye mamlaka juu ya wote. Hana mwanzo wala mwishoSasa swali kama mungu anatesa shetani usiku na mchana milele na milele huyu mungu mi nani?
Shetani ni malaika aliyeasi, akafukuzwa mbinguni; sasa ni adui wa Mungu na wanadamu.Huyu shetani kwanza ni nani tuanzie hapo.
Hapana. "Wana wa Mungu" hapo ni malaika; shetani alikuwa miongoni mwao kabla ya kuasi.Ayubu 1:16 ikawa hapo wana wa Mungu ....na shetani akaenda ...
Kumbe shetani ni mwana wa mungu si ndio ?
Mungu hamtesi mwana mtiifu; lakini shetani si mwana tena, bali ni muasi aliyehukumiwa tayari kwenda motoni.Setfree wewe
Unaweza tesa mwanao?
Amua leo kuokoka, Mungu atakupa neema na uwezo wa kushinda tamaa za mwili na ulevi. Ukitaka kuokoka, fuatisha sala hii:Unaweza kukaa na stress mpaka unatamani ubake na k vant dukani ni 4000 na bar 5000 tu?
Kwanini setfree?
Watu hawajaanza kuishi baada ya uwepo wa biblia, tafuta maarifa zaidi usiishie tu kusoma kitabu kimoja tu cha historia (biblia/quran)Ndugu yangu MastaKiraka tafakari tena uamuzi wako.
Halafu waambie watunga sheria wa nchi yako wafute kabisa sheria zote walizozi-copy kutoka kwenye Biblia, pamoja na katazo la kuiba na kuua. Halafu zikifutwa uone jinsi uasi utakavyoongezeka maradufu.
Utapotea bure mkuu, kama unaamini vitabu vilivyotungwa na watu. Ukitaka kupata ukweli, soma Biblia - kitabu kilichoandikwa kwa uongozi wa Mungu mwenyewe aliyeumba watu.Watu hawajaanza kuishi baada ya uwepo wa biblia, tafuta maarifa zaidi usiishie tu kusoma kitabu kimoja tu cha historia (biblia/quran)
Kama wewe ni binti na bado haujaolewa atakaye kuoa inabidi honeymoon akupeleke mirembe aseeUtapotea bure mkuu, kama unaamini vitabu vilivyotungwa na watu. Ukitaka kupata ukweli, soma Biblia - kitabu kilichoandikwa kwa uongozi wa Mungu mwenyewe aliyeumba watu.
Inawezekana, Umri mkubwa akili za kitoto. NimeshuhudiaSi ajabu nakuzidi umri, maana hoja zako ni za ki-Gen-Z 🙂
Ah wapi. Waswahili wanasema: "Kuishi kwingi, kuona/kujua mengi." Mimi kwa miaka mingi nimeona mengi yanayothibitisha kuwa Biblia sio hadithi kama za Alf Lela Ulela kama unavyofikiri wewe.Inawezekana, Umri mkubwa akili za kitoto. Nimeshuhudia
Setfree wewe sio mnzima imeandikwq "wapendeni adui zenu..."wapi Mungu anapenda adui zake?Mungu ni Mtakatifu, Mwenye haki na mwenye mamlaka juu ya wote. Hana mwanzo wala mwisho
Shetani ni malaika aliyeasi, akafukuzwa mbinguni; sasa ni adui wa Mungu na wanadamu.
Hapana. "Wana wa Mungu" hapo ni malaika; shetani alikuwa miongoni mwao kabla ya kuasi.
Mungu hamtesi mwana mtiifu; lakini shetani si mwana tena, bali ni muasi aliyehukumiwa tayari kwenda motoni.
Amua leo kuokoka, Mungu atakupa neema na uwezo wa kushinda tamaa za mwili na ulevi. Ukitaka kuokoka, fuatisha sala hii:
Omba (kwa kufuatisha kwa moyo wako wa dhati) sala hii ya toba.
Omba hivi:
“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha ya utakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea kiroho. Ubarikiwe sana.
Imeandikwa katika kitabu cha Mathayo 5:44-45Setfree wewe sio mnzima imeandikwq "wapendeni adui zenu..."wapi Mungu anapenda adui zake?
Ndugu yangu Nanye GoNi Mwanaume au Adam pekee ndiye aliumbwa kwa mfano wa Mungu, Huyu Hawa sijui yeye alikuwa mfano wa nani, maana alikuja kumpunguzia adam stress badala yake akalikoroga zaidi.
Mungu alimuumba Adam, baada ya muda mrefu Adam kuishi pekeyake, alimuona Adam akiwa mpweke ndipo akaamua kumlaza na kumuumba Hawa/Eva kutoka ubavu wa Adam lakini Hawa hakuwa kwenye plan za Mungu tangu mwanzo, ni stress za Adam zilifanya akaumbwa Hawa/Eva.Ndugu yangu Nanye Go
Mwanamke pia aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Soma Mwanzo 1:27
"Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba; mwanamume na mwanamke aliwaumba."
Hilo andiko linasema wazi kabisa: mwanamume na mwanamke waliumbwa kwa mfano wa Mungu. Kumbuka Hawa alitokana na ubavu wa Adamu ambaye tayari alikuwa katika mfano wa Mungu.
Dhambi haikutokana na jinsia ya kike, bali uasi wa wote wawili(Adamu na Hawa).
Mwanzo 3:6 inaonyesha Hawa alikula tunda kwanza, lakini pia Adamu alikula akiwa na fahamu zote, bila kushurutishwa.
Hayo maelezo umeyatoa kwenye Biblia gani? Mungu aliumba kila kitu kwa siku sita tu, wewe huo muda mrefu wa Adamu kukaa peke yake umeandikwa wapi?Mungu alimuumba Adam, baada ya muda mrefu Adam kuishi pekeyake, alimuona Adam akiwa mpweke ndipo akaamua kumlaza na kumuumba Hawa/Eva kutoka ubavu wa Adam lakini Hawa hakuwa kwenye plan za Mungu tangu mwanzo, ni stress za Adam zilifanya akaumbwa Hawa/Eva.
Sikumbuki ni kitabu gani lakini nakumbuka kinasema, Baada ya kumuumba Adam, na alikaa akamuona adam akiwa mpweke ndiyo plan ya kumuumba hawa/Eva ikaja.Hayo maelezo umeyatoa kwenye Biblia gani? Mungu aliumba kila kitu kwa siku sita tu, wewe huo muda mrefu wa Adamu kukaa peke yake umeandikwa wapi?
Katika habari hiyo ya Mwanzo, shetani anaitwa nyoka.