Tumlaumu Nyoka au Adam na Eva?

Tumlaumu Nyoka au Adam na Eva?

Suala la Adam na Eva ni suala la hatma nusu ambayo inahitaji utendaji nusu ikamilike kuwa jinai.....Yani Adam na Eva walizaliwa na hiyo hatma lakini walipewa uwezo wa kuishinda hatma yao na wao wakashindwa kuishinda hatma ya kumsaliti Muumba wao.....

Maisha yetu wote yapo hivyo tunaumbwa na hatma zetu ziwe nzuri au mbaya.....mfano mtu anaumbwa na hatma ya kuwa kiongozi bora na baadae anakuwa kiongozi, lakini katika uongozi wake anakuwa muuaji na kinyume cha maadili ya uongozi na maandiko huyu mtu atakufa kifo kibaya au ataenda mahali pabaya sababu ameruhusu hatma mbaya nusu ishinde hatma yake nzuri nusu....

Hatma zetu ni saa na chungwa nusu, iwe kwa ubaya au uzuri na tunaishi kuitafuta nusu nzuri au nusu mhaya inayoweza kutuokoa au kutumaliza kabisa na hatna mbaya
Aisee umemaliza..
 
Tumlaumu Mungu, mpanga yote. Nyoka, Adam, na Eva hawana makosa, bali aliyepanga na kuacha yatokee yaliyotokea wakati alikua na uwezo wa kuzuia, huyo ndo wakulaumu!!!
 
Hata kwenye Uislam Vivyo hivyo, Bali hadithi inaeleza Musaa alimwomba M/Mungu amletee Adam kwa Ajili majadiliano nae ina ilikuwa in term of miracle Ufufuo tu wa part time.
Huyo Musa na Adamu walikutana lini na wapi?
Ni akina nani walishuhudia huu mkutano?
 
Namlaumu Eva kwa kukubaliana na nyoka kuchapa lile tunda.
Kweli kabisa, kwa wanadamu Eva ndo kaanzisha zoezi la kuleta dhambi duniani, lakini vipi kama Adam angekataa kula lile tunda na Eva hivi maisha yangekuwaje hapo!!!!
 
Kwanza nyoka hana kosa mungu wa biblia na qurani ndo mwenye makosa. Baada ya nyoka kutuona tukitembea uchi kama hayawani akatuonea huruma sana ndipo akampa eva maarifa kwani adamu kichwa yake alikuwa haweZi kupokea knowledge.

Baada ya kula tunda wakapata akili kuwa wako uchi ndipo wakajistiri tupu zao kwa majani. Swali langu. kama adamu kaubwa mfano wa mungu kwanini mungu alikuwa akifurahi adamu kutembea uchi bustanini? Wewe utafurahi kumuona kichaa akitembea uchi? Hata kama huna cha kumsaidia nafsi yako itaona hiki sio kitu kizuri na pengine utamwonea huruma kichaa huyo.

Kwanini mungu aliona ni sawa eva kutembea uchi bustanini. Alikuwa anawafanyanini wakiwa uchi hapo mpaka nyoka wa watu akawaonea huruma na kuwapa elimu ya maarifa ya kujitambua? Kumbuka walikuwa hawana akili ya kujua zuri na baya au mema na mabaya Chochote wakifanyiwa waliona ni sawa.

Na kwanini mungu alivyoona adam ana akili ndo akampa nguo. Swali kama yeye mungu wq bible nguo alikuwa nazo siku zote kwanini hakumpa adamu na eva bali aliamua kuwacha uchi hadi nyoka alipoona hii sio sawa?

Source kitabu cha mwanzo.
Aisee kweli hili swala lina angle nyingi za kulidadavua
 
Irudiweee [emoji23][emoji23] huenda Hawa akawa anajielewa this time!
Anyway hii mijadala inavuruga sana akili
Ni kweli hii ni option nzuri ambayo nadhani hata sasaivi inaweza kutekelezeka sababu muumba ni muweza wa yote, arudishe time nyuma Eva na nyoka wafanye maamuzi mazuri this time tuje kuishi maisha mazur na sisi kizazi chetu kikifika. Lakini kwanini option hii haijatekelezwa?
Inavuruga sana akili
 
Kwa mm mkristo naamini kwenye kitu kiitwacho "Mpango wa Uokovu"...(Plan of salvation).
Ambao unaanzia kule mbinguni kabla misingi ya ulimwengu bado haijawekwa.
Ambao wote tulikua kule na MUNGU lakini tulikua kwenye mfumo wa roho.(hatukua na miili).

Binadamu wote ambao wamezaliwa,walizaliwa na watakaozaliwa walikuwepo katika mfumo huo tajwa na moja ya roho zilizokuwepo ni Adam,mussa,lucifer,Yesu,mm,ww ndugu msomaji na kila mtu ambae ana mwili wa nyama na mifupa kwa sasa.

Ndo mana ilikua Rahisi kwa MUNGU kusema Jeremia utakua Nabii, fulani utakua hivi ni sababu tulikua nae na tulikua tunajifunza na kila mtu alikua ana potential zake.

Sio coincidence leo mtu anazaliwa anakua muimbaji mfano jide, rubi etc,au mtu anakua soccer player kama samatta na wengine wengi wenye vipaji tofauti tofauti.

To cut the long story short ni kwamba kwenye huu mpango kila kitu tulikubaliana na kilipangwa mfano Adam kukengeuka,yesu kusalitiwa,shetani kuasi, etc.

So MUNGU anajua kila kitu....sisi baada ya kuzaliwa tumepita kwenye kitu kiitwacho "Veil"..ambacho kime erase kumbukumbu zetu zote za kilichotokea kabla hatujazaliwa.
Nakuomba uje na Uzi tafadhari unaoelezea plan of salvation.

Natumai Kuna kitu unacho,sema umeeleza Kwa kifupi,

Tafuta muda uwandike Kwa kilefu uwe Kama Uzi kabisa
 
Kwa mm mkristo naamini kwenye kitu kiitwacho "Mpango wa Uokovu"...(Plan of salvation).
Ambao unaanzia kule mbinguni kabla misingi ya ulimwengu bado haijawekwa.
Ambao wote tulikua kule na MUNGU lakini tulikua kwenye mfumo wa roho.(hatukua na miili).

Binadamu wote ambao wamezaliwa,walizaliwa na watakaozaliwa walikuwepo katika mfumo huo tajwa na moja ya roho zilizokuwepo ni Adam,mussa,lucifer,Yesu,mm,ww ndugu msomaji na kila mtu ambae ana mwili wa nyama na mifupa kwa sasa.

Ndo mana ilikua Rahisi kwa MUNGU kusema Jeremia utakua Nabii, fulani utakua hivi ni sababu tulikua nae na tulikua tunajifunza na kila mtu alikua ana potential zake.

Sio coincidence leo mtu anazaliwa anakua muimbaji mfano jide, rubi etc,au mtu anakua soccer player kama samatta na wengine wengi wenye vipaji tofauti tofauti.

To cut the long story short ni kwamba kwenye huu mpango kila kitu tulikubaliana na kilipangwa mfano Adam kukengeuka,yesu kusalitiwa,shetani kuasi, etc.

So MUNGU anajua kila kitu....sisi baada ya kuzaliwa tumepita kwenye kitu kiitwacho "Veil"..ambacho kime erase kumbukumbu zetu zote za kilichotokea kabla hatujazaliwa.
Naomba maelezo ya kina hapa kwenye maelezo yako haya chini;

kwenye huu mpango kila kitu 🤔tulikubaliana🤔 na kilipangwa mfano Adam kukengeuka,yesu kusalitiwa,shetani kuasi, etc.

Tulikubaliana mmh,ebu fafanua???
 
Uzi wa WAPAGANI naona mmeitana.

endeleeni kujadili ujinga wenu

Zab 53:1 SUV​

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.

Mt 11:25-26 SUV​

Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.
hzi kitu ukzama kw ndn kuna kuchoshan akil kuna njanj mwing hapa bila kutmia akil vzr utayumb sn
 
Yuda hata hukumiwa kwa sababu alimsaliti yesu kwa kuwa yesu alikwisha waombea msamaha kwa baba yake waliohusika na kifo chake kwa sababu ya kutokujua wanalolitenda lakini hukumu yake ambayo itakuwa kwa yeyote yule wa mfano wake ni kwa kule kufa kwenye dhambi kwa kuwa hakuona nafasi ya kutubu, huenda ni kweli unavyofikiria ni mpango wa Mungu amsaliti lakini swala la kupotea kwa sababu ya kushindwa kutubu sidhani kama ni sahihi kusema pia Mungu anahusika ila ni mtu mwenyewe maana hata petro unayemsema alimkana yesu mara tatu tena kwa kulaani na kuapa lakini aliona nafasi ya kutubu kwa sababu aliamini Mungu ni wa msamaha na Toba ya kweli anaipokea, na kwa Imani yake akasamehewa, maana hakuna dhambi ambayo Yesu hakuifia hata iwe mbaya kiaje, ukiamini kwa moyo wako wote na kukiri kwa kinywa ushaokolewa. Usipoamini ndio ushahukimiwau
 
Hii ndio kanuni ya kiroho iliyopo na inayotumika kutuokoa pia.kwa kuasi mtu mmoja Adamu wote tukahesabiwa hatia tumekosea na laana ya kifo ikatupata lakini pia kwa matendo ya haki ya mtu mmoja Yesu ambaye ni mwana wa Adam tukahesabiwa haki yake kuwa tunastahili kuishi na kupokea kipawa cha uzima wa milele kwa iman.
 
U

Sawa mkuu asante kwa mchango
 
Ulikua ni mpango wa Mungu.
Siyo kila jambo ni mpango wa Mwenyezi Mungu!
Mipango mingi mibaya ni mipango yetu sisi binadamu.
Usiniambie kuwa matendo yako yote tangu uamkapo hadi ulalapo ni mipango ya Mwenyezi Mungu.
Nitatoa mfano:
Miongo kadhaa iliyopita wakati nikiwa sekondari (maeneo ya kanda ya ziwa), mjukuu wa mama mwenye nyumba alifariki dunia. Msiba ulikuwa pale pale nyumbani tulipokuwa tumepanga mimi na kaka yangu.
Ni wazi kuwa kilichofanya aage dunia kilijulikana pale mtaani. Marehemu (binti) alikuwa mtu wa kujirusha sana na mwisho wake alibeba mimba. Ili kikwepa aibu na mambo mengine aliamua kumeza vidonge ili afanye abortion.
Mauti yalimkuta baada ya kuchukua uamuzi wa kuondoa maisha ya kiumbe kisichokuwa na hatia.
Pale msibani niliona kitu cha ajabu!
Wale wazee wenye kutia ina kwenye ndevu, walifika msibani kwa ajili ya kumpa pole mama mwenye nyumba juu ya msiba wa mjukuu wake. Kauli ya "Pole, hiyo ni kazi ya Mungu", ilitawala pale msibani.
Je ni kweli kuwa ile ilikuwa ni kazi ya Mwenyezi Mungu?

Mwenyezi Mungu ana mipango mizuri kwa wale wamchao - Romans 8:28.
 
Hii ndio kanuni ya kiroho iliyopo na inayotumika kutuokoa pia.kwa kuasi mtu mmoja Adamu wote tukahesabiwa hatia tumekosea na laana ya kifo ikatupata lakini pia kwa matendo ya haki ya mtu mmoja Yesu ambaye ni mwana wa Adam tukahesabiwa haki yake kuwa tunastahili kuishi na kupokea kipawa cha uzima wa milele kwa iman.
"Yesu ambae ni mwana wa Adam" !!!???
 
Back
Top Bottom