Tumpigie kura Rais Magufuli kuwa "Best Political Leader of the Year 2020"

Tumpigie kura Rais Magufuli kuwa "Best Political Leader of the Year 2020"

Wana Bodi Nawasalimu.

Nina Muda Mrefu Sana Kama Mkongwe Humu Jamvini Takribani Miaka Saba Sijaingia Humu Nikipambana Jimbo La Meru Lirudi Ccm Leo Imenibidi Niingie Kwa Hili Nyambo Nyeti Sana La Kupiga Kura Kwa Maraisi Watatu Africa Bora Katika Demokrasia Na Mojawapo Aliyeingia Ni Rais MAGUFULI Ambaye Kila Mtanzania Mzalendo Anajua Kazi Nzuri Alizofanya Kwa Miaka Mitano Iliyopita.


Ninawaombe Sana Wanatanzania Wetu Kwa UMOJA Wetu Tushikamane Kwa Pamoja KUMPIGIA KURA Kwa Wingi Rais Mnyenyekevu Na Mzalendo Kabisa Kutokea John Pombe MAGUFULI hili Ni Letu Sote Halina Uchama Wala Udini , Wapo Baadhi Ya Watu Hususani Wanachama Wa Chadema Wanaendesha Kampeni Chafu Dhidi Ya Rais MAGUFULI Asipigiwe Kura Za Kutosha Wakiongozwa Na Kima Mmoja Anaitwa Kigogo2014 Hawa Watu Ni Wa Kuupuzwa Ni Watu Wenye Chuki Binafsi Na Rais Wetu Mpendwa .


Watanzania Ni Wakati Wa Kumpa Raha Rais MAGUFULI Kwa KUMPIGIA KURA Za Kutosha Kuwa The Best Political AFRICAN Leader Of The Year 2021.

Naomba Kuwasilisha.
Umesoma vigezo kwenye hyo tuzo? Je magu anafiti?
 
Umesoma vigezo kwenye hyo tuzo? Je magu anafiti?
Hivi mtu akiona hana vigezo kwenye category husika si anaweza kuomba akajitoa au akawaomba waandaaji wamtoe? Ni ndoto tu zimenijia kabla sijalala
 
Ilitakiwa asiwemo kabisa kwenye mchuano, sema tu Africa bado tuna hali mbaya sana ktk utawala bora hadi Magufuli anakuwa considered.
Wanayofanya viongozi wengi wa Afrika ndiyo yale yale waliyokuwa wanayafanya wazungu
 
Kwenye ubunge wa Biharamuro alipigwa na Phares Kabuye ndio sababu hapendi kabisa uchaguzi na akahakikisha Chato linakuwa jimbo kutoka Biharamuro na tangu apate ubunge kupitia jimbo la Chato amehakikisha anapita bila kupingwa miaka yote.
Kwani yeye kipindi hicho ndio alikuwa anagawa majimbo??

Tangu lini mgombea akawa na mamlaka ya kugawa majimbo??
 
Anae himiza tumpigie kura rais Magufuli awe kiongozi bora wa kisiasa Africa atushawishi anazo sifa. Zipi na mashindano hayo yana vigezo vipi vinavyoshindanishwa. Bila kujua vigezo tunalinganisha nini na nani.
 
Mara ya mwisho kumpigia Kura ya Aina yeyote Ile Mwanasiasa wa Afrika ilikuwa mwaka 2015. Toka hapo Sina mpango Wala sitarajii kuja kufanya hivo Tena,, Kuwaelewa wanasiasa wa Afrika inahitaji upungufu wa akili ya kujitambua.

Kila la kheri enyi wachumia wanasiasa, sie wananchi tupo mbashara na matokeo tu.
 
Hawa jamaa nao wahuni Kama wahuni wengine, Kuna baadhi ya device ukitumia unakuta thanks for voting wakati bado haujapiga KURA, na Kuna muda ukiingia hasa usiku hauipati hiyo link mpaka utumie VPN. Tumpigie KURA ikibidi kwa VPN wajue sisi ndo wataalamu wa hizi kazi 😂
 

Attachments

  • Screenshot_20210105-024053.png
    Screenshot_20210105-024053.png
    12.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom