#COVID19 Tumpuuze Askofu Gwajima kuhusu Chanjo ya Corona

Sasa wewe unamsema mwenzako halafu wewe unatuongelea Taifa kama nani? chanjo ije anayetaka kuchoma achome asiyetaka amfuate Gwajima sawa tu hakuna wa kukulazimisha ila kila jambo lina gharama zake. Ila usiongelee kama unatuongelea sote hapana.
Ubarikiwe sana kiongozi
 
Unamdanganya nani? cdc wamesema jana kama umepokea chanjo huna haja ya kuvaa barakoa.uingereza almost karibia wote wamechanjwa na juma tatu ruksa kujichanganya. Sijui huwa mnawachukuliaje watanzania.
 
Unamdanganya nani? cdc wamesema jana kama umepokea chanjo huna haja ya kuvaa barakoa.uingereza almost karibia wote wamechanjwa na juma tatu ruksa kujichanganya. Sijui huwa mnawachukuliaje watanzania.
Haya mjuaji,,,maana hata sikuelewi,itakua Unajua sana
 
Yeye alikuwa anamshinikiza rais msimamo mkali kuhusu korona ni mpotoshaji.
Salizungumzia pia teknolojia ya 5G na kuipinga vikali akiihusisha na myama 666. Hajui maana ya 5g.
 
Kwahiyo tuache kuwasikiliza wataalamu wa Afya kuhusu ugonjwa wa Korona na Badala yake tumsikilize Gwajima ambaye hana hata cheti cha awali wa utabibu.
Yaani tumtegemee mtu mmoja mwenye maono ya kweli.
Mama kaunda Jopo la Madaktali waliobobea katika fani ya afya kufanya utafiti na kuja na napendekezo yakitaaluma.
Tuyaweke pembeni tumsikilize Gwajima.
Nyie waumini wa Gwajima mmelishwa maharage ya wapi ?
Mbona mnashikwa masikio namna hii.
Endeleeni kumsikiliza.
 
Ukipitia michango ya wadau...unagundua kuwa siasa inalipeleka pabaya taifa........

Watu kabla ya hoja wana muangalia mtoa hoja anatokea mlengo gani na ndio hapo anapopatia jibu la hoja yako badala ya kuangalia uhalisia wa hoja.......

Kimsingi Gwajima ametoa rai kama ambavyo watu wengine wanavyotoa maoni yao juu ya suala hili......Lakini bahati waliolipokea kwa mlengo hasi na siasa zimewapofusha bongo zao........badala yake yanateremka matusi badala ya kumpiga kwa hoja kinzani.........

Chuki hupofusha akili na kuzuia ubongo kutenda kazi..........

Watu wastaarabu wanajadili mambo kistaarabu na sio kwa matusi ya nguoni kama vibandani mwa wanywa gongo.......
 
Mkuu unapaswa kuwazoea wanasiasa wa nchi hii.....kwa ufupi ili mfuasi wa chama chochote cha siasa hapa nchini kitu cha kwanza unatakiwa umkabidhi akili zako mwenyekiti wako..........ukibakia na akili zako hutaweza kuwa mfuasi wa chama chochote achilia mbali kufuatilia siasa za nchi hii..........si unaona mtu akiwa huku ni mwizi na fisadi lakini akiwa kule anakuwa msafi lakini akirudi huku anakuwa mchafu kuanzia muda huo huo........kwa kifupi ili uwe mwanachama wa chama cha siasa nchini unatakiwa ukubali kuendeshwa na remote control..............hata huyu Gwajima wakati wa wimbi la ukawa alipewa mpaka sifa za unabii......
 
Labda kuna kamchezo! Mzungu anaweza kuchangiwa maji, wewe ukachangiwa dawa yenyewe na damu kuganga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…