Tumsaidie Steven Mdoe aka Dj Steve B anaumwa sana

Wamewambia wameshindwa kumtibu!?

Nilitaka kushangaa huyo jamaa mwenyewe ni mjeuri sana kama hayo majibu yako nashangaa humu watu wanamuonea huruma
 
Ubarikiwe kaka
 
Gharama za matibabu ya figo NHIF hawawezi kutoa,sababu ni kubwa, gharama za kusafisha figo ni zaidi ya laki tano kwa wiki.
Kila wiki unatakiwa usafishe mpaka hali itapotengemaa.
Jiepushe kuongea mambo usiyoyajua vizuri kwenye mitandao kiongozi...
NHIF hiyo huduma ipo
 
Jiepushe kuongea mambo usiyoyajua vizuri kwenye mitandao kiongozi...
NHIF hiyo huduma ipo
Miaka mitatu nilisikia intv ITV wagonjwa wa Figo wakihojiwa hii huduma haikuwepo,labda hivi sasa na hata ikiwepo labda kwa mchangiaji na si mtegemeaji.Wewe mtegemeaji hata miwani hapewi anaishiwa kupimwa basi miwani utanunua mwenyewe.
 
Nataka kutuma Tsh. 3,000,000/= kwa namba hiyo
 
Madj wenzake na clouds waandae tamasha moja linatosha kumsaidia muda upo ila naona iko shida cmg....clouds huwa wanabeba kitu na kukifanya kwa haraka ila kwenye hili sioni

Sent from my SM-G7102 using JamiiForums mobile app
Utajua kwann walimlilia ruge kwa sauti sana. Jamaa ndio ilikuwa engine ya maarifa leo clouds unaiona ipo ipo tu hakuna ubunifu wowote unaofanyika, ukiona mtu anakufa kwa mshtuko wa kifo cha mwingine jua the true mastermind is gone.
 
Umeongea vizuri sana mkuu,kiburi cha uzima kinaponza wengi sana...
 
"Sitivuu biii, ni wewe nasababisha muji kutishingika kinoooma nooma tupa sisi rubudaniii...asaaanduuu" hahaha ilikuwa ni jingle jmosi bongoflava clouds fm kuanzia ngoma nne hivi...
 
Weka link ya hiyo video wengine hatujaiona bro.
 
Huyu bwana kuna kipindi fulani cha nyuma tulikuwa majirani hapo dsm, wakati huo anafanya kazi CMG, naweza kusema alikuwa ni mtu muungwana sana mnyenyekevu mno, kutoa ni moyo wadau tumsaidie kadiri tunavyoweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…