Tumshauri kijana huyu cha kufanya, muda bado upo

mtaji unampasua kichwa anaanzaje
Akipata kuanzia 100,000 linaweza kufanyika jambo. Lengo ni starting point ya kuwa na chochote then confidence juu ya kufanya mambo mengine itamjia.

Kuwa na empty pocket kwa mtu mzima ni hatari kwa afya ya akili lakini kuanza kuwa na uhakika wa 5,000 kwa siku ni bora kuliko kutokuwa nayo.

Kuna biashara zinahitaji mtaji mdogo sana na zenye mzunguko mkubwa ila zinahitaji nidhamu na commitments. Jambo la msingi kwa sasa apate shughuli inayomwezesha apate chakula, kodi ya nyumba na mavazi then mengine yataanzia hapo. Asijifungie ndani

Kwa sasa ni ngumu kumshauri kwa kuwa hatujui anaishi wapi na anataka kufanya kazi ya aina gani.
 
Mungu atamlinda , kama anavyotulinda sisi sote, ilaa watu wanatoa shauri za kupiga vibarua, na shughuli za hapa na pale hahaha [emoji1787]. Ni kweli na apambane kweli kwelii.

Tupo tunapiga vibarua vya ujenzi na deals za mitaa, aloooh , Ukitoka hapo unapata pesa ,ila kutwa ni kutibu , Mgongo, kiuno , Mikono, uchovuu ,ili kesho uamke , Saving ni mtihani wa kufaulu [emoji2], Yaaani Maisha yanakua Kama adhabu kumbee ndio uhalisia [emoji3]. Unakunywa energy drink day to day zaidi kuliko maji (Mtaani tunaita luuzi Figo [emoji1787])

Yote tutasema, ila atambue yeye Ni mwanaume, na ameumbiwa kazi, Nimejifunza kutoa aibu , ili niishi , Na ninaishi, japo Hata robo ya malengo ya maisha sijagusa na namba inaelekea kusoma C [emoji28].Mtaa una Mambo Sana , apambane TU Kama tunvyo pambana na akubali mauvi (kihisia na mwili)kupata helaa.
#Ikiwezekana mpe simu asome shauri, atapata nguvu ya maisha ili aweze ishi.
#Mungu Atukuzwe.
 
Kama alisoma anashindwaje kupambana na mazingira take binafsi toka 2015 huyo atuna msaada naye
 
Oyaaaa,huyu nikijana wa kufikiria au wakutunga mbona kama anamaswqibu sana...eti tegemeo lake pekee nikujichua dahhhhh
 
πŸ˜€ shukrana sana @choz 14
unaongea vitu vya maana sana kwa lugha rahisi, nyepesi ya kitaa kabisa aisse. Ile inafurahisha zaid licha ya ugumu wa hali yenyewe still unafuraha, unapambana na unasonga mbele mdogomdogo bila kuchoka wala kukata tamaaa.....

pamoja sana kijana......
 
hii kitu kijifungia ndani, kuona haya na aibu ni vitu mbaya sana kuviendekeza...

shukran sana Japkas
 
Nikipita maeneo ya vyuo vikuu i.e UDSM,TIA,SAUT etc nikaona wanafunzi wanaenda madarasi kusoma hua nasikitika Sana.

Yajayo hayatawafurahisha.
Inabidi waendelee kusoma tu, hakuna namna
 
Ushauri bora nilio wahi kuona Jf
 
Nikipita maeneo ya vyuo vikuu i.e UDSM,TIA,SAUT etc nikaona wanafunzi wanaenda madarasi kusoma hua nasikitika Sana.

Yajayo hayatawafurahisha.
Unaonaje, wasiende na wasisome?🀣
Kweli hii ni top gear.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…