Tumshauri kijana huyu cha kufanya, muda bado upo

Tumshauri kijana huyu cha kufanya, muda bado upo

mtaji unampasua kichwa anaanzaje
Akipata kuanzia 100,000 linaweza kufanyika jambo. Lengo ni starting point ya kuwa na chochote then confidence juu ya kufanya mambo mengine itamjia.

Kuwa na empty pocket kwa mtu mzima ni hatari kwa afya ya akili lakini kuanza kuwa na uhakika wa 5,000 kwa siku ni bora kuliko kutokuwa nayo.

Kuna biashara zinahitaji mtaji mdogo sana na zenye mzunguko mkubwa ila zinahitaji nidhamu na commitments. Jambo la msingi kwa sasa apate shughuli inayomwezesha apate chakula, kodi ya nyumba na mavazi then mengine yataanzia hapo. Asijifungie ndani

Kwa sasa ni ngumu kumshauri kwa kuwa hatujui anaishi wapi na anataka kufanya kazi ya aina gani.
 
Mungu atamlinda , kama anavyotulinda sisi sote, ilaa watu wanatoa shauri za kupiga vibarua, na shughuli za hapa na pale hahaha [emoji1787]. Ni kweli na apambane kweli kwelii.

Tupo tunapiga vibarua vya ujenzi na deals za mitaa, aloooh , Ukitoka hapo unapata pesa ,ila kutwa ni kutibu , Mgongo, kiuno , Mikono, uchovuu ,ili kesho uamke , Saving ni mtihani wa kufaulu [emoji2], Yaaani Maisha yanakua Kama adhabu kumbee ndio uhalisia [emoji3]. Unakunywa energy drink day to day zaidi kuliko maji (Mtaani tunaita luuzi Figo [emoji1787])

Yote tutasema, ila atambue yeye Ni mwanaume, na ameumbiwa kazi, Nimejifunza kutoa aibu , ili niishi , Na ninaishi, japo Hata robo ya malengo ya maisha sijagusa na namba inaelekea kusoma C [emoji28].Mtaa una Mambo Sana , apambane TU Kama tunvyo pambana na akubali mauvi (kihisia na mwili)kupata helaa.
#Ikiwezekana mpe simu asome shauri, atapata nguvu ya maisha ili aweze ishi.
#Mungu Atukuzwe.
 
Amemaliza chuo kikuu ngazi ya Shahaada mathalani 2015. Amejitahidi kusaka ajira serikalini na kwenye sekta binafsi tangu wakati huo, mpaka sasa bila bila, na anaelekea kukosa sifa za kuajirika kwa mujibu wa sheria kutoka na kigezo cha umri na uzoefu.
Mambo ni mengi na ni Magumu, na muda ni mchache.

Uzuri wa kijana huyu, ni kwamba hajakata tamaa hata kidogo, ila anaelekea huko taratibu maana mvi zimemzonga hasa.

Na kinachomchochea kukata tamaa ni kwamba, anajiuliza hana hata ka plot au shamba, kijijini kwao wala mjini, hana mchumba wa uhakika wala hata mtoto wa kusingiziwa, faraja yake kwa muda mrefu huenda ni ilikua kujichua tu. Alikua na matumaini ya kupata ajira awe na kipato na mchumba mzuri pia.

Umri umesonga, fedha ngumu haoni cha kufanya, kodi ni shida, kula ni shida, anakwepa hata kushiriki mambo ya kijamii kama vile ndoa na misiba. Ni mnyonge sana hana ujasiri kabisa.

Kijana anasononeka mno, anajuta, ananung'unika na kujisemea mwenyewe moyoni alikosea wapi, mbona kama ni yeye pekeyake tu, anapitia masaibu haya.

Kijana anaona haya na aibu hata kurudi kijijini kwao kwenye maziwa na asali za kutupwa. Rika lake na wadogo zake wa shule, wameoa na kuolewa, wana nyumba nzuri, maisha mazuri, biashara kubwa, kipato kikubwa, wamezaa watoto wazuri, wakubwa wanawasomesha maeneo mbalimbali. Hili linampasua kichwa zaidi kijana huyu.

Kijana akitafakari hayo, moja haikai wala mbili haikai. Umri umesonga, mvi ndio kama zote, anaanza kuchuja na kukongoroka. Anahisi kama ana mkosi, hapendeki wala haitajiki tena kwenye jamii, roho ya kukata tamaa ina mnyemelea na kumkaribia zaidi....

Wapendwa maisha hayana Extra time.
Hebu tusaidiene, tuelimishane, tuelekezane, tupeane moyo na njia katika hili, tumkwamue kujana huyu mpendwa alipokwama.

Asipotee bali apate mwanga na Nuru ya kutoka kimaisha Salama.

Wasalam.
Oyaaaa,huyu nikijana wa kufikiria au wakutunga mbona kama anamaswqibu sana...eti tegemeo lake pekee nikujichua dahhhhh
 
Mungu atamlinda , kama anavyotulinda sisi sote, ilaa watu wanatoa shauri za kupiga vibarua, na shughuli za hapa na pale hahaha [emoji1787]. Ni kweli na apambane kweli kwelii.

Tupo tunapiga vibarua vya ujenzi na deals za mitaa, aloooh , Ukitoka hapo unapata pesa ,ila kutwa ni kutibu , Mgongo, kiuno , Mikono, uchovuu ,ili kesho uamke , Saving ni mtihani wa kufaulu [emoji2], Yaaani Maisha yanakua Kama adhabu kumbee ndio uhalisia [emoji3]. Unakunywa energy drink day to day zaidi kuliko maji (Mtaani tunaita luuzi Figo [emoji1787])

Yote tutasema, ila atambue yeye Ni mwanaume, na ameumbiwa kazi, Nimejifunza kutoa aibu , ili niishi , Na ninaishi, japo Hata robo ya malengo ya maisha sijagusa na namba inaelekea kusoma C [emoji28].Mtaa una Mambo Sana , apambane TU Kama tunvyo pambana na akubali mauvi (kihisia na mwili)kupata helaa.
#Ikiwezekana mpe simu asome shauri, atapata nguvu ya maisha ili aweze ishi.
#Mungu Atukuzwe.
😀 shukrana sana @choz 14
unaongea vitu vya maana sana kwa lugha rahisi, nyepesi ya kitaa kabisa aisse. Ile inafurahisha zaid licha ya ugumu wa hali yenyewe still unafuraha, unapambana na unasonga mbele mdogomdogo bila kuchoka wala kukata tamaaa.....

pamoja sana kijana......
 
Akipata kuanzia 100,000 linaweza kufanyika jambo. Lengo ni starting point ya kuwa na chochote then confidence juu ya kufanya mambo mengine itamjia.

Kuwa na empty pocket kwa mtu mzima ni hatari kwa afya ya akili lakini kuanza kuwa na uhakika wa 5,000 kwa siku ni bora kuliko kutokuwa nayo.

Kuna biashara zinahitaji mtaji mdogo sana na zenye mzunguko mkubwa ila zinahitaji nidhamu na commitments. Jambo la msingi kwa sasa apate shughuli inayomwezesha apate chakula, kodi ya nyumba na mavazi then mengine yataanzia hapo. Asijifungie ndani

Kwa sasa ni ngumu kumshauri kwa kuwa hatujui anaishi wapi na anataka kufanya kazi ya aina gani.
hii kitu kijifungia ndani, kuona haya na aibu ni vitu mbaya sana kuviendekeza...

shukran sana Japkas
 
Almanusura niseme ni ww🤔lkn nikakumbuka siyo ww bn we ni mleta mada tu!

Kwa mtu aliemaliza chuo 2015 saiv atakua na miaka 30+ sio umri mbaya sana ukituliza akili, kwa miaka 8 uliyokua mtaani Kuna jambo utakua umeligundua na unaweza lifanya either mjini au kijijini kafanye kwa moyo wote.

Epuka kujiweka karibu na siasa na wanasiasa, achana na mawazo ya kujiweka karibu na makada wa chama flan ukiamini kwenye uteuzi, kua low key fanya yako siasa ina wenyewe

Epuka mahusiano kama hujaoa usihangaike piga kazi zako chora ramani vzr kila unachokifanya fikiria namna inaweza kukupa Hela sio kupoteza Hela.

Baki kwenye Imani yako acha kuwaza miujiza, acha kuwaza laana/baraka, acha kuwaza unachopitia ni majaribu, sali kwa Imani yako ishi vzr na watu Linda amani ya moyo wako.

KWA SAIVI NIISHIE HAPA
Ushauri bora nilio wahi kuona Jf
 
Nikipita maeneo ya vyuo vikuu i.e UDSM,TIA,SAUT etc nikaona wanafunzi wanaenda madarasi kusoma hua nasikitika Sana.

Yajayo hayatawafurahisha.
Unaonaje, wasiende na wasisome?🤣
Kweli hii ni top gear.
 
Back
Top Bottom