Tokea 2015 mpaka sasa kwavile hajafa njaa, maana yake hela anaingiza. Je, anafanya mishe gani kwa sasa?
Anaishi wapi?
Mkuu
Analyse,
siyo mtu moja ama wawili katika hili,
Ni kundi kubwa kidogo, miongoni mwao binafsi ninawafahamu. Wengine ni ndugu zangu, jamaa na marafiki zangu. Wengine tulisoma shule pamoja na hata michezo ya utotoni tuliicheza pamoja. Yawezekana pia unao.
Sasa ni watu wazima kiasi, social life forces marika zimewatupa mkono kidogo, si unajua zile lazima uvae pamba kali, raba kali, uchukue demu mkali wiki hii, wiki ijayao mwingine, club kila alhamisi na Jmos. Japo hizo forces bado zipozipo lakini umate umate unapiga breki kama zote.....
Na sasa hivi umri umekimbia kidogo. Real Life forces ndio hivyo tena zimeanza na zinahitaji kijana awajibike na hana namna.
Lakini kabachelor degree kako mfukoni.......
Mfukoni kijana hana jambo,
akilini kwa kijana, moja haikai mbili haikai....
kijana huyu hivi sasa bado yupo mjini anaishi kwa uncle, unt, shemeji, bamkubwa, bamdogo na washkaji kitaani tangu alipokuja mjini kusoma chuo na tangu amalize chuo miaka hiyo hajapata ajira mpaka sasa....
Katika ujumla huo ndipo, nikaomba nasaha na ushauri humu jukwaani kwajili ya kijana huyu, ili aondokane na huo mkwamao....