Tumshauri kijana huyu cha kufanya, muda bado upo

Tumshauri kijana huyu cha kufanya, muda bado upo

Mtu mmoja kashauri vizuri hapo juu kwamba ww acha vyeti ndani elimu iache kichwani na pia GPA iache km ilivyoandikwa kwenye cheti, we nenda vijijin huko mbarali wasikokufaham kapge kazi za kutumia nguvu, kwa mwez hukos 300k... No Way out ni kujitutumua tu. Huyu jamaa nimemwelewa sana
 
USHAURI Mimi nimemliza chuo 2015 nilifanya BAED ...Mojor Geo minor History

Nilitumia Mika Zaid ya mi2 kujitolea kweny shule Moja ya masista IPO Songea

Badae nilianza kujihusisha na kilimo Cha Mahindi trust me nilianza na heka Moja asahv nalima heka 15. Navuna Zaid ya gunia 200

Najuitia sana kupoteza muda kuatfuta Ajira nakujitolea

Vijana wengi hawataki kuanza upya
Nililima heka Moja Kwa mkono wangu w
Mwenyewe nilikongoroka U handsome wote ulitoka..nikanunua mbolea mifuko 3
Nikatia nikavuna gunia 17

Mwaka ulio fata ilikua 2018 nililima heka 3

Lakin nilikua na mtaji wa 180k ndio nilinunua mbolea mwk wa kwanza

Asahivi nimenunua Bajaj mbili mpya
Nimewapa vijana mmojaa ana diploma mwingine ni Account.

Wote nimewapa mkataba wakimaliza Miaka 2 zinakua zao.

Ukiwaambia ingia shamban Utaskia sina mtaji .....

NB: Shambani niliingia hakukua nyumbn ni mkoa ambao hawanijui kbisaaaa
Ruvuma ndani kabisa Kijiji kinaitwa Liganga wanalima Mahindi balaa.

Nipo huku Sasa ni kama nyumbani na nimeoa mngoni.maisha yanasonga.
Hongera na asante kwa ushauri murua kabisa.
 
W

Wangapi wana GPA nzuri ila bado wapo kitaa na msoto tu,na wangapi wana GPA fyongo ila wana ajira,mimi aliyekuwa best student katika kozi yangu pale MUHAS , mpaka leo hana ajira ,,
Bado Wewe ni kijana au ujajitambua! Hujui chochote katika maisha! Kwahiyo failures vilaza ndo wanaajiliwa best student wanasota mtaani? Kwahiyo watoto wetu tusiwapeleke shule? Si ndio kijana?
 
Alaf wakati tuliopo sio kujadili ugumu wa maisha na ajira akuna,, mbona amjadili wepesi wa kujiajili kwa vikundi na mitaji midogo ili tuikuze,, amna kitu kikubwa mwenye shahada anawaza tuu kulipwa 1M wakati huku kwenye jamii kunawatu wameanzisha biashara wanapata laki moja kwa mwezi Leo wanazaidi ya million tatu
 
USHAURI Mimi nimemliza chuo 2015 nilifanya BAED ...Mojor Geo minor History

Nilitumia Mika Zaid ya mi2 kujitolea kweny shule Moja ya masista IPO Songea

Badae nilianza kujihusisha na kilimo Cha Mahindi trust me nilianza na heka Moja asahv nalima heka 15. Navuna Zaid ya gunia 200

Najuitia sana kupoteza muda kuatfuta Ajira nakujitolea

Vijana wengi hawataki kuanza upya
Nililima heka Moja Kwa mkono wangu w
Mwenyewe nilikongoroka U handsome wote ulitoka..nikanunua mbolea mifuko 3
Nikatia nikavuna gunia 17

Mwaka ulio fata ilikua 2018 nililima heka 3

Lakin nilikua na mtaji wa 180k ndio nilinunua mbolea mwk wa kwanza

Asahivi nimenunua Bajaj mbili mpya
Nimewapa vijana mmojaa ana diploma mwingine ni Account.

Wote nimewapa mkataba wakimaliza Miaka 2 zinakua zao.

Ukiwaambia ingia shamban Utaskia sina mtaji .....

NB: Shambani niliingia hakukua nyumbn ni mkoa ambao hawanijui kbisaaaa
Ruvuma ndani kabisa Kijiji kinaitwa Liganga wanalima Mahindi balaa.

Nipo huku Sasa ni kama nyumbani na nimeoa mngoni.maisha yanasonga.
Dah 🥴
Mkuu nimejitela hapa kununa eneo kigamboni milioni 2.5 mwez uliopita mwez huu kazin nimetimuliwa 😂
Najiuliza hapa nifanyeje Bora ile hela ningekuja nayo huko kulimisha mkuu
 
Binafsi nilihitimu Shahada 2016 nikakosa ramani mtaani ikanibidi niingie VETA kusoma fani ya Umeme wa majumbani Kwa miaka miwili(kozi ndefu). Namshukuru Mungu Kwa Sasa nimejiajiri na nimeajiri vijana. Kwa Sasa nimerudi VETA kusoma umeme wa viwandani mwaka wa 3.

Jiongeze kutafuta ujuzi, hujachelewa.
Kwa uzoefu wako kazi ya rangi imekaaje mana mm naiweza ile mchawi vyeti tu. Nataka nifanye mpango mwakani nizamiepo huko
 
Chakuwashauli vijana,, kwanza wakubali kujifunza wafundishike,, wavumilie maneno makali,, wapunguze mizigo ya kujiona wakubwa na mabishoo wa tafute muda wakuutumia kufanya kufanya kazi muda ni mwingi Sana ukiwanao kazi na ndio maana wanaofanya kazi wanaupata mpka wakupumzika,, sasa kijana asubui yupo vijiweni usiku club..
 
ok sawa, sory mkuu,
Mshauri basi jamaa afanyeje,
hana mishe tangu amalize chuo miaka ya nyuma huko na alikua anatumaini kuajiriwa lakina mpaka sasa bila bila, umri unaenda na muda unasonga pia
Mkuu mbona umekadhania sana swala la ushauri? Nitashauri nini ikiwa maswali niliyouliza kwenye comment yangu ya kwanza hujayajibu? Au umehisi hayana mantiki?
 
Amemaliza chuo kikuu ngazi ya Shahaada mathalani 2015. Amejitahidi kusaka ajira serikalini na kwenye sekta binafsi tangu wakati huo, mpaka sasa bila bila, na anaelekea kukosa sifa za kuajirika kwa mujibu wa sheria kutoka na kigezo cha umri na uzoefu.
Mambo ni mengi na ni Magumu, na muda ni mchache.

Uzuri wa kijana huyu, ni kwamba hajakata tamaa hata kidogo, ila anaelekea huko taratibu maana mvi zimemzonga hasa.

Na kinachomchochea kukata tamaa ni kwamba, anajiuliza hana hata ka plot au shamba, kijijini kwao wala mjini, hana mchumba wa uhakika wala hata mtoto wa kusingiziwa, faraja yake kwa muda mrefu huenda ni ilikua kujichua tu. Alikua na matumaini ya kupata ajira awe na kipato na mchumba mzuri pia.

Umri umesonga, fedha ngumu haoni cha kufanya, kodi ni shida, kula ni shida, anakwepa hata kushiriki mambo ya kijamii kama vile ndoa na misiba. Ni mnyonge sana hana ujasiri kabisa.

Kijana anasononeka mno, anajuta, ananung'unika na kujisemea mwenyewe moyoni alikosea wapi, mbona kama ni yeye pekeyake tu, anapitia masaibu haya.

Kijana anaona haya na aibu hata kurudi kijijini kwao kwenye maziwa na asali za kutupwa. Rika lake na wadogo zake wa shule, wameoa na kuolewa, wana nyumba nzuri, maisha mazuri, biashara kubwa, kipato kikubwa, wamezaa watoto wazuri, wakubwa wanawasomesha maeneo mbalimbali. Hili linampasua kichwa zaidi kijana huyu.

Kijana akitafakari hayo, moja haikai wala mbili haikai. Umri umesonga, mvi ndio kama zote, anaanza kuchuja na kukongoroka. Anahisi kama ana mkosi, hapendeki wala haitajiki tena kwenye jamii, roho ya kukata tamaa ina mnyemelea na kumkaribia zaidi....

Wapendwa maisha hayana Extra time.
Hebu tusaidiene, tuelimishane, tuelekezane, tupeane moyo na njia katika hili, tumkwamue kujana huyu mpendwa alipokwama.

Asipotee bali apate mwanga na Nuru ya kutoka kimaisha Salama.

Wasalam.
Tatizo la wasomi wengi huwa wanaenda shule Hadi vyuo kusoma ili wasjiliwe Sasa linapotokea suala la ajila kukosekana Basi hawana la kumfanya wanabski kujuta kwa Nini walisomaea gani hizo ebu kwa mtazamo wa Sasa niwashauli wasomi wanapoenda vyuoni wawe Kama JKT hata Kama hamna ajira wajiajili wenyewe pia ishu sio mtaji ishu Ni akili ya mtu na kujiona kwamba wa Levo furani hawazi fanya kazi furani kaxi nzuri zipo Kama vile bodaboda bajaji vibarua nk unajuwa na uhakika wa kutunza pesa Kila siku 10000 hujapata mtaji ndani ya miezi mitatu ukafsnya mambo yako yanaenda leo hii Kuna watu wsnzfanys hixo kazi hawatamani hata kuajiliwa wasalaam
 
Ajaribu kazi za vibarua viwandani na Katika miradi ya ujenzi, huko ndiko mimi kulikonilea. Ingawa asione aibu kupokea 2500 mpk 7000 kwa siku na akikuta anatumwa na watu wa standard 7 na pia wanakula mshahara mnono kuliko yeye. Mi nilichekwa sana ati msomi unafanya kazi moja na asiyesoma, nilivumilia ila mwishowe nilizoea na wakaanza niita professor
 
Back
Top Bottom