Pre GE2025 Tumshauri Rais Samia aachie madaraka 2025 au agombee?

Pre GE2025 Tumshauri Rais Samia aachie madaraka 2025 au agombee?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM kuendelea kubaki madarakani haitegemei kupigiwa Kura na mtu yoyote yule ktk Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania.

Anyway, hata kama Rais SSH ataamua kuacha kugombea Urais, bado matatizo yote ya Kiutawala yaliyopo hivi Sasa hapa Tanzania yataendelea kuwepo kwa sababu kiini Cha kuwepo kwa matatizo hayo siyo Rais SSH bali yanatokana na uwepo wa Katiba mbaya ya nchi ambayo ipo pamoja na kuwa na Chama tawala kibaya na kisichofaa, the presence of bad ruling party of CCM.
Umenena vyema. Na ndio maana nikasema, uchaguzi huu Samia atarudi ila hadi damu.
 
Hata huko kijijini hawamtaki huyu mama. Fuatilia
Kijijini wengi Huwa wanapewa kanga wanasahau shida zao.

Ila ukienda huko Sasa hivi watakwambia matatizo ya nchi hii yanaletwa na utawala wa mwanamke.
 
1. Hana Maono,

2.Uwezo wa kujenga HOJA na kutetea HOJA ni mdogo,

3. Usimamizi wa raslimali za umma ni mdogo,

4. Uwezo wa Kupambana na RUSHWA ni chini.

5. Uwezo na uthubutu wa kufanya maamuzi Kwa wakati uko chini .

6. Hashauriki, issue ya Ngorongoro, Bandari, Tume huru na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi, ni baadhi tu ya mifano michache.

Tuweke vyama pembeni, 2025 ni Bora akapumzika mchakato ukafanyika apatikane mtu sahihi.
Una point. Usikilizwe.
 
Vitu vilivyomwangusha sana Rais Samia mpaka kufikia kuvhukiwa na watu wengi, hasa ni:

1) kuwadanganya watu na kisha kupuuza suala la katiba mpya, na uwepo wa tume huru ya uchaguzi

2) kugawa hovyo rasilimali za nchi, kwa.mgongo wa uwekezaji wakati kiuhalisia hao waarabu ni wavunaji. Fikiria mtu anapewa mbuga ya wanyama au hifadhi ya msitu, halafu anaitwa mwekezaji, amewekeza nini?

3) Mikataba ya hovyo yemye hila ndani yake, inayowafanya watanganyika kuwa watu duni mbele ya wageni.

4) Uundwaji wa timu za siri za Wazanzibari ili kurahisisha uporwaji wa rasilimali za Tanganyika. Fikiria uporwaji wa bandari, Watanganyika wote waliondolewa kwenye nafasi ambazo zingewafanya washiriki kwenye huo mchakato wa uporwaji bandari. Wote waliondolewa, wakawekwa Wazanzibari, na kisha wakakamilisha uporwaji wa bandari na DP World.

5) Upendeleo wa wazi kwa Wazanzibari. Ameteua wazanzibari mpaka kwenye nafasi zisizo za Muungano. Wakati bandari za Zanzibar hazihusiki kwenye mkataba wa kishenzi wa DP, lakini Wazanzibari wapo kwenye nafasi za maamuzi kwa bandari za Tanganyika. Amezilinda bandari za Zanzibar, akaamua kuziangamiza za Tanganyika.

6) Kuwafukuza wamasai kutoka maeneo yao ya asili, na kisha kuyagawa maeneo hayo kwa waarabu.

Rais Samia alianza vizuri. Wengi mwanzoni walimuunga mkono, wapinzani na wanaCCM, walimuunga mkono. Lakini siku zilivyoenda alizidi kuwakera wananchi wengi. Sasa hivi amebakia na MACHAWA tu yanayopigania matumbo yao. Nashangaa, kati ya watu ambao hawamtaki kabisa, zaidi ni wanawake na watu wa vijijini. Wengi wanalalamikia ugumu wa maisha.
 
CCM kuendelea kubaki madarakani haitegemei kupigiwa Kura na mtu yoyote yule ktk Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania.

Anyway, hata kama Rais SSH ataamua kuacha kugombea Urais, bado matatizo yote ya Kiutawala yaliyopo hivi Sasa hapa Tanzania yataendelea kuwepo kwa sababu kiini Cha kuwepo kwa matatizo hayo siyo Rais SSH bali yanatokana na uwepo wa Katiba mbaya ya nchi ambayo ipo pamoja na kuwa na Chama tawala kibaya na kisichofaa, the presence of bad ruling party of CCM.

Na bahati mbaya kwa Samia, hiyo katiba mbaya hajaifanyia kazi kuiondosha, jambo ambalo lingempa credit kubwa.
 
Akiingia huyo mnayemtaka mtamkubali miaka yake yote ya utawala wake? Mbona Magufuli mlimkataa?

Kuhangaika tu

Sasa hivi Rais anayehitajika ni yule atakayehakikisha yafuatayo yanafanyika:

1) kusimamia ukamilishaji wa katiba mpya yenye rejea ya tume ya Jaji mwenye hekima, akili na uzalendo mkubwa, Jaji Warioba.

2) kusimamia upatikanaji wa muundo mzuri wa Muungano kwa kuzingatia maoni ya umma kwa tume ya Warioba.

3) kusimamia uundwaji wa mifumo imara ya utawala, uchumi na kodi.
 
Jinsi mambo yanayoelekea sina la kusema na hasa haya ya Lissu yakikuzwa na ya Ngorongoro sina la kusema.
 
Sasa hivi Rais anayehitajika ni yule atakayehakikisha yafuatayo yanafanyika:

1) kusimamia ukamilishaji wa katiba mpya yenye rejea ya tume ya Jaji mwenye hekima, akili na uzalendo mkubwa, Jaji Warioba.

2) kusimamia upatikanaji wa muundo mzuri wa Muungano kwa kuzingatia maoni ya umma kwa tume ya Warioba.

3) kusimamia uundwaji wa mifumo imara ya utawala, uchumi na kodi.
Uongozi ni karama. Aliyekuwa na uwezo wa kusimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba ,kwa mtazamo wangu ni hayati Magufuli kwasababu ya ujasiri wake aliokuwa nao. Magufuli haikuwa kipaumbele kwake

B.T.W Wakenya wana katiba mpya ila tabu iko pale pale
 
Saa hundred asigombee urais hii ni ajili ya usalama wa ccm vinginevyo kifo Cha ccm kitawahishwa, kaharibu sana Kila kiongoz ktk serikali yake anafanya atakavyo halafu zile familia za tangu enzi na enzi waliojilimbikizia ukwasi wa kutisha ndo mama huyo kawaachia wafanye wapendavyo Hadi kupelekea bidhaa zote muhimu kupanda bei mara dufu.

Ikumbukwe hizo familia zimegawana keki ya taifa mfano zipo familia zinajihusisha na uingizaji mafuta, IPO familia iliyoshikiria tenda ya ununuzi wa magar ya serikali, IPO familia yenye tenda ya kuagiza vifaa vya kijeshi kuanzia kombati Hadi makombora, IPO familia imeshikiria manunuzi ya vifaa vya nishati n.k Kwa kifupi Kila manunuzi au ujenzi unaofanyika hapa ndani Kuna familia inahusika hata kama Haina uwezo wa kujenga mradi flani wao ndio watakao mtafuta mkandarasi na familia inabaki kuwa madalali.

Wakati wa mjomba Magu kidogo hizi famili zilitaitiwa lakini huyu mkojani kawaachia kiasi ya kwamba watanzania wote sasa hivi ni vibarua wa hizo familia, lakini pia viongozi wengi wamo kwenye usafirishaji abiria na mizigo Kwa kuitumia mabasi na malori mtawalia ndo maana mradi wowote wa reli hauwezi kufanya kazi ktk mazingira haya, mfano IPO familia Moja ya huko pwani pamoja na kwamba wamejirundikia tenda nyingi za kitaifa Bado wanachimba madini hasa dhahabu karibu Kila mkoa wa nchi hii, mkoa wa Morogoro peke yake ninayajua machimbo kadhaa ya dhahabu na hakuna wa kuwabughudhi, siyo kwamba ccm kule juu hawajui. Na ikumbukwe kuwa sasa hivi wapo watu wanauwezo mkubwa sana wa kujenga hoja na hawaogopi kitu wapasua humohumo kwenye puputura nikimtazama mama uwezo wake upo chini sana pia ikumbukwe kuwa wakati wa kampeni mgombea atahusika kujenga hoja huyu mama hawezi najua anamtegemea BASHITE ambae mweupeee kichwani
 
Uongozi ni karama. Aliyekuwa na uwezo wa kusimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba ,kwa mtazamo wangu ni hayati Magufuli kwasababu ya ujasiri wake aliokuwa nao. Magufuli haikuwa kipaumbele kwake

Wakenya wana katiba mpya ila tabu iko pale pale
Sio kweli .
Tabu iko pale pale kivipi?
Acha kupotosha watu.
 
Wana JF, wasalaam.

Naenda moja kwa moja kwenye mada.

Kila nikiangalia siasa zinavyokwenda, ni hakika Samia hataweza kutoboa ila kwa njia ya kumwaga damu. Atatumia nguvu sana ili kurudi ikulu.

Kuna vielementi vingi sana ninavyo viona vitakavyo mnyima kura.

1. Hana kambi ya kumpigania kufa kupona. yuko na chawa tu ambao wao wanafuata upepo tu. Kifupi hajatengeneza timu yake kwenye Siasa.

2. Kuna jamii bado kabisa haiamini kutawaliwa na mwanamke, inatawaliwa tu by the way.

3. Bandari, narudia tena, Bandari. Hii ni issue kubwa sana linapokuja swala la kampeni.

4. Wamasai, nawahakikishia hapa napo ni kazi mno. Kanda ya kazikazini hapa wanasema mzanzibari kawafukuza watanganyika kwenye ardhi yao.

5. Kujenga hoja. Samia hana haiba ya kujenga hoja na wananchi wakamsikiliza. Itakuwa ngumu sana kupangua makombola ya wapinzani. Wakati wa uchaguzi watu wanahitaji mzuka yaani, mtu akiongea iwe kwikwi.. ni kama umuone Ester Bulaya ama Mdee wanaongea, utawasikiliza tu. Ila kumsikiliza Samia ni mpaka uwe na maslahi na speech yake..kama May Mosi vile.

6. Muungano; Huu muungano wetu unafanya mgombea kutoka zanzibar aonekane kama mvamizi, Muungano unatakiwa ufanyiwe marekebisho. Bila kuurekebisha mtu kutoka zanzibar ni ngumu sana kupata kura huku bara. Kama anamchanganyiko wa ubara na Uzanzibari anaweza akapata.

Sawali; Je, CCM wamshauri aachie ngazi kimya kimya ama wamupeleke tu hivyo arudi ikulu kwa kumwaga damu?
Asome alama za nyakati, kuna kundi kubwa ndani ya chama chake hawako naye ila hajawajua
 
Back
Top Bottom