Pre GE2025 Tumshauri Rais Samia aachie madaraka 2025 au agombee?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Umenena vyema. Na ndio maana nikasema, uchaguzi huu Samia atarudi ila hadi damu.
 
Hata huko kijijini hawamtaki huyu mama. Fuatilia
Kijijini wengi Huwa wanapewa kanga wanasahau shida zao.

Ila ukienda huko Sasa hivi watakwambia matatizo ya nchi hii yanaletwa na utawala wa mwanamke.
 
Una point. Usikilizwe.
 
Vitu vilivyomwangusha sana Rais Samia mpaka kufikia kuvhukiwa na watu wengi, hasa ni:

1) kuwadanganya watu na kisha kupuuza suala la katiba mpya, na uwepo wa tume huru ya uchaguzi

2) kugawa hovyo rasilimali za nchi, kwa.mgongo wa uwekezaji wakati kiuhalisia hao waarabu ni wavunaji. Fikiria mtu anapewa mbuga ya wanyama au hifadhi ya msitu, halafu anaitwa mwekezaji, amewekeza nini?

3) Mikataba ya hovyo yemye hila ndani yake, inayowafanya watanganyika kuwa watu duni mbele ya wageni.

4) Uundwaji wa timu za siri za Wazanzibari ili kurahisisha uporwaji wa rasilimali za Tanganyika. Fikiria uporwaji wa bandari, Watanganyika wote waliondolewa kwenye nafasi ambazo zingewafanya washiriki kwenye huo mchakato wa uporwaji bandari. Wote waliondolewa, wakawekwa Wazanzibari, na kisha wakakamilisha uporwaji wa bandari na DP World.

5) Upendeleo wa wazi kwa Wazanzibari. Ameteua wazanzibari mpaka kwenye nafasi zisizo za Muungano. Wakati bandari za Zanzibar hazihusiki kwenye mkataba wa kishenzi wa DP, lakini Wazanzibari wapo kwenye nafasi za maamuzi kwa bandari za Tanganyika. Amezilinda bandari za Zanzibar, akaamua kuziangamiza za Tanganyika.

6) Kuwafukuza wamasai kutoka maeneo yao ya asili, na kisha kuyagawa maeneo hayo kwa waarabu.

Rais Samia alianza vizuri. Wengi mwanzoni walimuunga mkono, wapinzani na wanaCCM, walimuunga mkono. Lakini siku zilivyoenda alizidi kuwakera wananchi wengi. Sasa hivi amebakia na MACHAWA tu yanayopigania matumbo yao. Nashangaa, kati ya watu ambao hawamtaki kabisa, zaidi ni wanawake na watu wa vijijini. Wengi wanalalamikia ugumu wa maisha.
 

Na bahati mbaya kwa Samia, hiyo katiba mbaya hajaifanyia kazi kuiondosha, jambo ambalo lingempa credit kubwa.
 
Akiingia huyo mnayemtaka mtamkubali miaka yake yote ya utawala wake? Mbona Magufuli mlimkataa?

Kuhangaika tu

Sasa hivi Rais anayehitajika ni yule atakayehakikisha yafuatayo yanafanyika:

1) kusimamia ukamilishaji wa katiba mpya yenye rejea ya tume ya Jaji mwenye hekima, akili na uzalendo mkubwa, Jaji Warioba.

2) kusimamia upatikanaji wa muundo mzuri wa Muungano kwa kuzingatia maoni ya umma kwa tume ya Warioba.

3) kusimamia uundwaji wa mifumo imara ya utawala, uchumi na kodi.
 
Jinsi mambo yanayoelekea sina la kusema na hasa haya ya Lissu yakikuzwa na ya Ngorongoro sina la kusema.
 
Uongozi ni karama. Aliyekuwa na uwezo wa kusimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba ,kwa mtazamo wangu ni hayati Magufuli kwasababu ya ujasiri wake aliokuwa nao. Magufuli haikuwa kipaumbele kwake

B.T.W Wakenya wana katiba mpya ila tabu iko pale pale
 
Saa hundred asigombee urais hii ni ajili ya usalama wa ccm vinginevyo kifo Cha ccm kitawahishwa, kaharibu sana Kila kiongoz ktk serikali yake anafanya atakavyo halafu zile familia za tangu enzi na enzi waliojilimbikizia ukwasi wa kutisha ndo mama huyo kawaachia wafanye wapendavyo Hadi kupelekea bidhaa zote muhimu kupanda bei mara dufu.

Ikumbukwe hizo familia zimegawana keki ya taifa mfano zipo familia zinajihusisha na uingizaji mafuta, IPO familia iliyoshikiria tenda ya ununuzi wa magar ya serikali, IPO familia yenye tenda ya kuagiza vifaa vya kijeshi kuanzia kombati Hadi makombora, IPO familia imeshikiria manunuzi ya vifaa vya nishati n.k Kwa kifupi Kila manunuzi au ujenzi unaofanyika hapa ndani Kuna familia inahusika hata kama Haina uwezo wa kujenga mradi flani wao ndio watakao mtafuta mkandarasi na familia inabaki kuwa madalali.

Wakati wa mjomba Magu kidogo hizi famili zilitaitiwa lakini huyu mkojani kawaachia kiasi ya kwamba watanzania wote sasa hivi ni vibarua wa hizo familia, lakini pia viongozi wengi wamo kwenye usafirishaji abiria na mizigo Kwa kuitumia mabasi na malori mtawalia ndo maana mradi wowote wa reli hauwezi kufanya kazi ktk mazingira haya, mfano IPO familia Moja ya huko pwani pamoja na kwamba wamejirundikia tenda nyingi za kitaifa Bado wanachimba madini hasa dhahabu karibu Kila mkoa wa nchi hii, mkoa wa Morogoro peke yake ninayajua machimbo kadhaa ya dhahabu na hakuna wa kuwabughudhi, siyo kwamba ccm kule juu hawajui. Na ikumbukwe kuwa sasa hivi wapo watu wanauwezo mkubwa sana wa kujenga hoja na hawaogopi kitu wapasua humohumo kwenye puputura nikimtazama mama uwezo wake upo chini sana pia ikumbukwe kuwa wakati wa kampeni mgombea atahusika kujenga hoja huyu mama hawezi najua anamtegemea BASHITE ambae mweupeee kichwani
 
Uongozi ni karama. Aliyekuwa na uwezo wa kusimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba ,kwa mtazamo wangu ni hayati Magufuli kwasababu ya ujasiri wake aliokuwa nao. Magufuli haikuwa kipaumbele kwake

Wakenya wana katiba mpya ila tabu iko pale pale
Sio kweli .
Tabu iko pale pale kivipi?
Acha kupotosha watu.
 
Asome alama za nyakati, kuna kundi kubwa ndani ya chama chake hawako naye ila hajawajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…