#COVID19 Tumsikilize mchungaji Gwajima, tusimbeze. Chanjo zote zina bechi tofauti na kuna nchi hukataa baadhi ya bechi na nyingine ni zile zilizobakia

Watu wanaogopa ushirikina wa kanda ya ziwa.

Wajaribu Kumgusa Watanuka wote hakuna wa kumfukuza Gwajima CCM.

CCM hawamuwezi Gwajima kwa sababu Gwajima ana'watu'. Waseme su waone moto wa Askofu Rashid Gwajima.

 
Wangemvua uanachama halafu wanatangaza jimbo lipo wazi akili ingemkaa sawa. Utampingaje M/k wako tena hadharani.

kwa hyo mwnyekiti akisema tembea uchi utatembea kwa sababu ya kulinda kibarua na mwenyekiti hapingwi
 

Unalalama tu boss bila justification...

å Matusi gani alitukana viongozi?

å Kauli gani chafu na matusi alitoa?

Kama ambavyo Freeman Mbowe na CHADEMA wasivyokuwa na makosa yoyote licha ya kukamatwa na kumbakikiwa makosa ya jinai, vivyo hivyo Bishop Rev. Josephat Gwajima hana kosa lolote...

Kumkamata, kumtia korokoroni na kumfungulia mashtaka yoyote eti tu kwa sababu ametoa maoni yake ya kutokukubaliana na mpango wa chanjo ya serikali na kuahawishi wengine waelewe na kukataa mpango huo, itakuwa ni uonevu mbaya na usiovumilika...

Lakini lililo jema ni kuwa, hiyo ni sauti ya mtu aliaye nyikani akikemea watawala kwa kuwaambia waziwazi kuwa, itengenezeni njia ya Bwana maana ufalme wa Mungu umekaribia...!!!

Kama hawatasikia, wataumia wenyewe...
 
Gwajiboy na elimu yake ya kuunga unga asipotoshe Wananchi juu ya Covid 19. Anapaswa kubaki kwenye dini yake asipingane na serikali yake.
 
Hakuna kitendawali kutoka kwa Gwajima
Ushauri wangu inabidi ufahamu msimamo wa Gwajima kuhusu Corona Na Chanjo kabla ya kuwa Mbunge Na baada ya kuwa Mbunge.
Msimamo wake haujabadilika ni ule ule.

kama unajipanga kusikiliza mahubiri ya Jumapili ni vizuri ukaendelea na majukumu yako
 
Gwajima ni mpotoshaji anatumia kila njia kubaki relevant. Nadhani akiongea tena aje na ushahidi wa study aliyofanya maana kwa uelewa watanzania Wana mwamini kuliko wataalamu wa afya.
Nadhani anayo haki ya kutoa maoni yake....
 
Huyo Gwanjima atachanja kisirisiri awe na cheti chake cha kwenda Marekani kama alivyoahidi kuwapeleka Wana kawe Marekani.
 
Kwenye vutana vutana inayoendelea nchini kuhusiana na chanjo ya UVIKO-19, nimepata nafasi ya kuwafahamu viongozi wetu wanaotuongoza na maneno yao wanayosema kila siku.

Hayati JPM alijua siri ya Corona na akatwambia ukweli mtupu kwa nia njema kabisa. Kipindi chote alichokuwepo hakuwahi kamwe kupindisha maneno yake katika kile alichokijua na kukielewa, alitahadharisha watanzania kuhusu vitu vinavyotoka nje. Msimamo wake ndio uliolivusha taifa na kuonekana la tofauti na kipekee ulimwenguni, na kuchochea maendeleo mpaka taifa likaingia uchumi wa kati. Hapa nchini, shughuli ziliendelea kama kawaida utadhani korona haikuwepo kabisa.

Rais Samia ameonesha kutokuwa na msimamo katika maneno yake. Alipokuwa makamu wa rais, msaidizi wa kwanza wa rais JPM, alionesha kuwa na uelewa kwenye jambo linaloendelea duniani na alisisitiza watu kumtegemea Mungu. JPM hayupo, amepiga kona ya nyuzi 180; amemwacha Mungu na ameamua kuwategemea wazungu, mabeberu ambao awali alisema walikuwa wameanza kumtegemea Mungu kama sisi. Watu tuliokuwa tunaishi vizuri ameturudisha kwenye mijadala ya Corona na chanjo.
Unaweza kumwamini kiongozi kama huyu anayebadilika? Kiongozi wa hivi si anaweza kuuza nchi na watu wake kabisa? Kama kweli ni rais wa nchi, aliyeapa kuilinda nchi na watu wake, kwa maslahi gani hasa anayafanya haya? Huyu kweli ni mzalendo kwa taifa lake? Tafakari.
SAMIA AMETUKOSEA SANA WATANZANIA

Waziri wa Afya ni kigeugeu na mtu hatari sana kwa taifa letu. Wizara inaongozwa na mtu ambaye kipaumbele chake ni ajira yake. Amenukuliwa mara nyingi akilalamika kwamba watu wanaojaribu kumchallange wanahatarisha ugali wake. Huyu ni mchumia tumbo tu huyu. Anajua jinsi chanjo zilivyo hatari lakini amepiga U-turn na kuzikumbatia kwasababu tu anataka kumfurahisha rais ili alinde kibarua chake hata kama watanzania wataangamia. DR DOROTH BORA UBWAGE MANYANGA WEWE NI MNAFIKI

Mtu pekee nchini ambaye tangu ameanza kuongea hajawahi kabisa kupindisha maneno yake ni ASKOFU GWAJIMA. Binafsi sikuwa nimemfuatilia sana enzi za nyuma kabla ya kuwa mbunge. Lakini nimegundua msimamo wake juu ya korona na chanjo ni ule ule kabla ya kuwa mbunge na baada ya kuwa mbunge. Maneno ya Askofu Gwajima sio ya kuandikiwa na mtu, sio ya kusoma kwenye karatasi, sio ya kumfurahisha mtu. Maneno yake yanaonesha anajua kitu fulani ambacho muda wote yuko tayari kuhatarisha hata maisha yake ili kuokoa kundi kubwa lililo hatarini ambalo halijui undani wa korona na chanjo. Amedhihirisha kuwa mtu thabiti asiyeyumba.

Ukifuatilia kwa karibu, utagundua Askofu Gwajima ameanza kuongea mambo yanayotokea hivi sasa tangu mwaka juzi. Na aliyoyaongea, taratibu yanaanza kutokea, ingawa watu wengine waliyapuuzia na kuyabeza. Anayatoa wapi mambo haya? Mtu wa namna hii ni vizuri kumsikiliza na kuwa makini naye kwa sababu inaonekana vyanzo vyake vya taarifa ni vya uhakika.
Aliwahi kusema itafika mahali kama mtu hajachanjwa hataruhusiwa kuuuza au kununua vitu. Jana tu taarifa inazunguka inayoonyesha rais wa Ufaransa akisema mtu ambaye hatachanjwa hataruhusiwa kununua vitu. Tunaelekea wapi?

Askofu Gwajima mwanzoni kabisa wa korona alisema Tanzania itachukua msimamo wa tofauti, na huo msimamo tofauti utaipaisha juu kiuchumi. Haikupita mwaka, Tanzania iliingia Uchumi wa Kati na watalii walikuwa wanakuja kwa wingi kipindi ambapo nchi nyingi zilikuwa zimefunga mipaka yake.

KAMA ALIYOYASEMA ASKOFU GWAJIMA YAMETOKEA, MANGAPI ANAYAJUA AMBAYO HAJAYAWEKA WAZI BADO?
Watanzania wa leo sio wa jana; ukisoma maoni ya watanzania wengi, utagundua kuwa walisubiri mtu atakayejitoa muhanga kuwanasua kutoka kwenye mikono ya viongozi wao wanaotaka kuwachanja kitu kilichokataliwa na waliokileta.

Gwajima anajua kuwa hiari inayosemwa ni mtego, baadaye chanjo itakuwa lazima kama waliotayari kuchanja kwa hiari wataisha; dawa ni kila mtu kugoma kuchanja.

Lakini pia Gwajima ameshauri serikali ianze kufanyia utafiti wa kutengeneza chanjo hapa nchini, maana hata wale wanaosukumiza chanjo huku Afrika hawaamini chanjo za mataifa mengine.

KWA NINI SERIKALI ISIZINGATIE USHAURI WA KUTENGENEZA CHANJO HAPA HAPA NCHINI?
Serikali isipambane na Askofu Gwajima, nyuma yake kuna mamilioni ya watanzania ambao hawana mtetezi na wote wamekuja nyuma yake waliposikia anasema anapinga kinachoendelea. Badala yake isikilize ushauri anaotoa na kuufanyia kazi.

Kama serikali inasema wazi haitahusika na madhara yoyote yatokanayo na chanjo kwa mtu atakayechanjwa...je, ni nani atawajibika kwa madhara yatakayosababishwa na chanjo? Ni nani atamsaidia atakayepata madhara hayo.? Tafakari.

Kama serikali haitaki kubeba lawama, basi tuisaidie kwa kugoma kupokea chanjo. Kunipa chakula halafu ukasema kikinidhuru usiulizwe... maana yake lazima hicho chakula kitaleta madhara na hutaki kuwajibika kwa madhara hayo!!

Naomba watanzania kwa pamoja tusikubali kuwa sehemu ya majaribio. Hata mtu akiamua kuchanja mbele ya TV hiyo haitoshi kutuaminisha maana anaweza kuchanja kitu kingine chochote ambacho sio chanjo ya UVIKO-19 anayotaka wengine wachanjwe.

KATAA CHANJO NA KWA PAMOJA TUSIMAME NA ASKOFU GWAJIMA.

CHANJO NI HATARI!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…