#COVID19 Tumsikilize mchungaji Gwajima, tusimbeze. Chanjo zote zina bechi tofauti na kuna nchi hukataa baadhi ya bechi na nyingine ni zile zilizobakia


Haya kwa kuwa tunakupenda, angalia na huyu hapa. Kamab vipi, kwa kuwa mnaweza, waueni wote mkiwamaliza, mwende na mataifa mengine yanayopinga hiki kitu, nao muwaue, mbaki ninyi na billgates peke yenu.

 
Magufuli amewaharibu sana,hivi mwafrika utamkwepaje mzungu akidhamiria kukuua?
Unakataa chanjo ya corona,vipi kuhusu chanjo ya polio,ndui na surua?
Hivi ni nani aliyewaroga kiasi cha kushindwa kujua hata uji unaokula kila siku unaweza kukumaliza? Mnashinddwa nini kuelewa kuna watu wallipendana lakini baada ya muda wapenzi hao waka chomeana ndani ya nyumba na kuuana? Nikweli hujawahi kuona mtoto au mzazi akiua mtoto wake? Mbona mnakuwa kama hamko duniani? Matamshi ya Billy Gates na wenzake kuhusu mtumizi ya chanjo kupunguza idadi yawatu duniani hamjayasoma? Mbona yako kila kona? Hivi ninyi ni watu gani kama hamjui habari za new word order? Nini ni watu waina gain msiojua kuna agenda ya kudepopulate dunia ambayo iko dhahiri? Ni nini kifanyike ili muone? Kwa nini mnaishi kwa kukariri matukiio?

Kwa kuw mzugnu hashindwi kukuua , ndipo upeleke shingo yako Kibra?
Mbona mnatoa hoja za watu primitive sana? Hii ni ishara kwmba ujinga bado ni tatizo kubwa hapa tulipo?
 
Shida kubwa ya waTanzania walio wengi ni kutumia mahaba baada ya akili........

Yaani mtu kabla hajaangalia content ya habari kwanza anatazama hii habari imeletwa na nani kuanzia hapo ndio akili yake itaamua kwamba aipinge au aikubali habari........

Akili zetu tumewakabidhi wanasiasa, hakuna tena mwenye kufikiria nje ya maoni na utashi wa wanasiasa......

Siku waTanzania watapoanza kutumia akili zao baada ya kuabudu fikra za wanasiasa ndio safari ya mabadiliko ya kweli itakapoanza.........
 
Wanajua lugha ya kibeberu tusaidieni hii forum inasema?

 
Mkuu ili uwe na fikra kama hizi jambo la kwanza unatakiwa huru kifikra.......jambo ambalo waTanzania wengi hawana.....

Yaani hapo mpaka aje kuelewa ni mpaka kiongozi wake wa kisiasa abadili fikra zake ndio na yeye anaji update.......

Kwa lugha nyepesi wanasiasa wametengeneza kizazi cha mazezeta wa fikra.....ndio maana haishangazi kumuona mtu hata tukio la kudai haki yake anangoja kauli ya mwanasiasa.......

Haya mambo yako mbali na fikra za waTanzania kwa kuwa hayajawahi kusemwa na wanasiasa...............
 
Kwanini serikali ikatae kuwajibika kwa usalama wa chanjo wanayodai ni salama kwa asilimia 99.99.....???

Kutatokea nini endapo nitachanjwa ambacho serikali haitawajibika.......??

Na kwanini serikali isiwajibike hali ya kuwa ndio iliyoleta chanjo.....??
 
Mnamtukuza tu huyo gwajima.toka alivyomtukana pengo sijawahi muona wa maana na u team tu unaendekezwa TZ.
 
Utangulizi- Nawaomba Mods msihamishe uzi huu.

Mchungaji Josephat Gwajima asimamia maeneo mawili katika hoja yake.

Kwanza, kilichomo kwenye chanjo na pili chanjo dhidi ya wanajeshi na walinda usalama wa nchi.
Mkuu Richard , kwanza asante sana kwa bandiko elimishi, mabandiko kama haya they add value kwa jf and to the society, thanks for this.

Pili hongera kwako binafsi, kutumia muda wako, uwezo wako na elimu yako kuwaelimisha wengine. Ni kupitia bandiko lako hili, mimi ndio nimejua na kuelimika kuhusu batch no. Hivyo maana yake kama Tanzania tumepatiwa hizo chanjo milioni 1, za JJ, ina maana hizo chanjo zitachanja watu 500,000 ili kuepuka kuisha na wengine kulazimika kutumia a different batch.

Suluhisho ni kuepuka chanjo za double jabs ni kutumia chanjo za single jab kama hii ya JJ huku bara, na ile Sputnik ya Urusi inayotumiwa Zanzibar, zote ni single jab, ukichanjwa, umechanja, you are done.

Nikirudi kwa Mchungaji Gwajima, kwa vile yeye ni kiongozi wa umma, ni mbunge kupitia CCM na pia kiongozi wa kiroho kwa waumini wa kanisa lake, hivyo ni mtu mwenye big influence, chochote atakachosema kina big impact, badala ya kupinga chanjo, nafuu akae kimya.

Kitendo cha Mwenyekiti wake, rais Samia kuhamasisha chanjo, halafu yeye kutoa maoni tofauti na kuhamasisha watu wasichanje,ni usaliti
P
 
Kwahiyo avue ubongo kama nguo, auweke chini ili asiwe msaliti?
Your browser is not able to display this video.
 
Wasabato masalia mnatabu sana,endeleeni kusubiri pasi zakusafiria kwa maombi muende ulaya.
Sasa mwendazake kilichomuua ni chanjo ama korona?
 
Siku Gwaji boy atakapo hitaj kwenda ktk makanisa ya nje ya nchi ndionatajua chanjo inadhuru DNA au lagasha
 
Gwajima ni wa kupuuza, hajui chochote kuhusu sayansi, muongo na elimu yake ya kuunga unga , tena ya dini yake.
Swali la msingi je Corona virus vaccine inabidili DNA ya mtu?
Jibu HAPANA.
Chanjo ya corona haina muingiliano wowote katika utendaji wake kazi na DNA. Ikutoshe tu wewe msomaji kujuwa kuwa, vinasaba vya chanjo (viral vector COVID-19) na mesenja RNA za mwili ( mRNA) hutuma maelekezo (genetic material) kwa seli za mwili zianze kutengeneza mfumo wa kujilinda dhidi ya virusi vinavosababisha COVID-19.
SASA HAPA PIGIA MSTARI.
HATA HIVYO MADAWA NA KEMIKALI HIZO KAMWE HAZIINGII NDANI YA NUKILIA YA SELI, SEHEMU AMBAYO NDIO DNA HUPATIKANA.
Biology ya O level hapa inahusika sasa kujua seli ya mwanadamu na sehem zake, wapi inapatikana mRNA, tRNA, Ribosome, mitochondria na Nucleus.
Huhitaji shahada ya virology kujua kuwa vinasaba chanjo( viral vector COVID-19) havina muingiliano wala kamwe haviwezi athiri DNA ambayo inapatikana ndani ya nukilia ya seli. Hazipenyi kwenye nukilia kuta mbili za ukuta wa nukilia.
Source kwa hisani ya taasisi ya kudhibiti na kuzuia maradhi ya Marekani.
(COVID-19 Vaccine Facts)
 
Utangulizi- Nawaomba Mods msihamishe uzi huu.
Mchungaji Josephat Gwajima asimamia maeneo mawili katika hoja yake.
Gwajima yupi anaongelewa hapa? Kama ni huyu hapa chini sina la kuongeza...

Your browser is not able to display this video.


Hapa ndipo unapojua Watanzania ni viumbe wa pekee duniani. Richard, huu utafiti wako wote umeupata kwa kuungaunga vyanzo vya huko huko Marekani na kwingineko ambako wapo watu aina yako tena si wachache, ni wengi.

Laiti ungejua kuwa original vaccine deniers ndio wale wale waliokuwa original covid-19 deniers. Je unajua kitu gani kinawatokea hivi sasa? Wanapigana vikumbo kuwahi chanjo kwa sababu Covid-19 ikiwapigia hodi hakuna tena cha mswalie mtume.

Yeye Gwajima, askofu na mbunge, tapeli wa kidini na kisiasa, shetani katika umbo la binadam, kibwetere wa nyakati hizi ataondoka na wengi tu. Ajabu mwendakuzimu aliposalimu amri kwa corona, baunsa alijifungia asije akapewa tenda ya kumfufua!
 
Hivi kwa utaalamu gani mlionao?yani kutengeneza chanjo hamuwezi halafu ndio muweze kufanya analysis? Yani Magufulu alipowaambia ninyi ni donor country mnakubali!
Kwa maana hiyo ni sawa tu kopokea chochote tunachopewa, siyo?
 
Kwa maana hiyo ni sawa tu kopokea chochote tunachopewa, siyo?
Mtapokea tu hakuna namna!
Hio simu inayokutia kiburi wamekutengenezea wazungu unaosema wanataka kukuua!
Ngozi nyeusi tatizo sana,yani teknolojia pekee unayoitegemea kupambana na korona ni nyungu then unaleta kibesi.
 
Don't insult my intelligence.

When you insult someone intelligence is when you tell them how to think and say things.

Waweza kuona nimeweka mifano hai ndani ya mada yangu wapi shida?

Hata ufanyapo utafiti si waweka references?

Na hiki ndicho kinachoendelea kwa waafrika kwa ujumla hawana "independent mind" kufikiria nje ya boksi, I repeat we are vulnerable na tunatumiwa kwa udhaifu huo, period.

Tuna wasomi wengi tu nchini lakini wawapi leo hii tupo katika shida ya ugonjwa? Weye wagonjea dawa ya chanjo kutoka nje, kisha wajisifu umesoma?

Sifahamu kiwango cha elimu yako na weye hiyo twaweza kuwa level moja au nimekuzidi au umenizidi who knows.

Mchungaji Gwajima na haki ya kutoa maoni/ fikra na mtazamo wake.

Mind you, mimi si mfuasi wa Mheshimiwa Gwajima, wala si mfuasi wa chama chochote, niliondoka kuwa mfuasi wa vyama na nikahamia kuwa mfuasi wa serikali itayojaribu kuwa na nguvu lakini fair katika maamuzi yake na utendaji wake wa kazi.

Wasema nimeungaunga jaribu kukubali kuwa nimefanya utafiti na kuna ambao wamenikubali maoni yangu, sidhani kama mtizamo wako ni upi.

Serikali ni lazima iwe na "Scientific advisory board" ambayo inampa brief mheshimiwa raisi ya kila kinachoendelea nchini.

Hivi nikuulize kamati iloundwa kumshauri raisi juu ya UVIKO-19 hadi leo imetoa taarifa yoyote baada ya ile ya kushauri watu wachanjwe?

Sisi tumsikilize tu kama tuwezavyo kuwasikiliza wengine.

Naamini tumechelewa kama taifa na ni jukumu la serikali kuhakikisha yajiandaa kutengeneza dawa ya chanjo ya kitanzania.

Dunia sasa imebadilika kila mtu ana uwezo wa kufikiri kwa makini na kwenda ndani zaidi.

Hizi si zama za kufuata upepo tu.

Huu ndio ushauri wangu.
 
Kwa hiyo nawe unaamini baunsa anafufua watu waliokufa au siyo. Kama ni hivyo basi usiwe na wasi wasi, Covid-19 ikikupigia hodi tapeli Gwajima yupo, atakufufua ila sijui alishindwaje kumfufua yule dhalimu mwendakuzimu. Na mimi huo ndio ushauri wangu.

Swali kwako: Je Mbowe na wenzake nao wana hiyo haki ya kutoa maoni/fikra na mtizamo wao?
 
Nimeshauri mara nyingi humu kuwa Mbowe abadili strategy na haijawa hivyo miaka nenda rudi.

Kisha awe na strategists kumsaidia.

Siasa ni sayansi na yahitaji pia kusoma alama za nyakati kama kweli kuna nia thabiti ya kukiondoa chama kilichoshika dola kwa miongo kadhaa.

Vinginevyo kila anachofanya hata kama kina nia thabiti kinaonekana si sawa na anakumbana na madhila ya vyombo vya dola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…