#COVID19 Tumsikilize mchungaji Gwajima, tusimbeze. Chanjo zote zina bechi tofauti na kuna nchi hukataa baadhi ya bechi na nyingine ni zile zilizobakia

#COVID19 Tumsikilize mchungaji Gwajima, tusimbeze. Chanjo zote zina bechi tofauti na kuna nchi hukataa baadhi ya bechi na nyingine ni zile zilizobakia

Mbona kwenye chanjo ya surua au polio mbona hizo side effects hazikutokea mpaka sasa; kwani chanjo ya corona?
Tafuta historia ya chanjo ya Polio walochanjwa waCongo ( enzi za mfalme Leopold wa pili) miaka ya 50-60.

Na pia makoloni yake mengine ya rwanda na Burundi.

Na hiyo ilikuwa baada ya miaka kadhaa ya majaribio.
 
Richard, soma kidogo changamoto zilizoandama juhudi za kupambana na gonjwa lililowafyeka binadamu zaidi ya 300,000,000 miaka zaidi ya100 iliyopita. Gonjwa hilo lilijulikana kama small pox.

Katika juhudi za kulitokomeza, soma upinzani ambao juhudi hizo zilipitia hadi dawa ya kwanza kabisa ya chanjo kupatikana na ilipatikanaje. Soma upinzani mkali uliandama matumizi ya chanjo hiyo.

Soma jinsi mtu moja alivyofungua kesi hadi makama kuu nchini Marekani (Supreme Court) kupinga chanjo hiyo na soma maamuzi ya mahakama hiyo na hatua zilizochukuliwa kuhakikisha chanjo inatolewa.

Soma wahubiri na manabii uongo walivyohusisha chanjo hiyo na mafundisho ya dini kama anavyofanya Gwajima hadi nguvu kutumika kwa kupita nyumba hadi nyumba kutoa chanjo hiyo kwa nguvu.

Watu wenye uelewa mdogo na wasiojua historia wanafikiri hii ni chanjo ya kwanza kupata upinzani mkali wa chanjo na wanatumia ujinga wao kupinga hii chanjo kwa sababu kama hizo hizo za karne zilizopita.

Hebu pitia hapa kidogo... https://www.washingtonpost.com/history/2021/04/01/vaccine-supreme-court-smallpox-covid/
Hiyo nimeisoma.

Hata ule ugonjwa wa mafua kule Hispania au Spanish Flu nimeusoma pia hivyo naelewa.

Na huu ugonjwa ulisambaa duniani kwasababu ya vita kuu ya kwanza ya dunia na ni wanajeshi ndoi walisambaza ugonjwa.

Lakini pamoja na kutokuwepo dawa za kuua virusi (antiviral) na antibiotics wakti ule dawa za asili ziliweza kutumika.

Je, leo dawa za asili ni mbaya au tu kwasababu ya maendeleo ya kiteknolojia ndo yameleta dawa za chanjo kuwa tayari na kuidhinishwa mara tu ugonjwa unapolipuka?
 
shida ni ujuaji mwingi...we umeshaambiwa chanjo ni hiari unahamasisha watu ujinga yani wataalamu na watafiti wapitishe maoni ambayo wamegaramika elimu na muda wao wewe uje tu na conspiracy za hearsay,gwajisay without any official utafiti...hata hivyo ndio domokrasia bt use it kwa manufaa na sio kupotosha
Mawazo haya ya kijinga ya kupuuza sauti ya Mungu ndiyo yaliyowaangamiza kwa gharika ya maji watu wote wa dunia ya wakati wa Nuhu...

Walikuwa na arguments kama zako kuiweka "human science" juu ya NGUVU ZISIZOPIMIKA ZA MUNGU aliye hai...

Wakati Nuhu na wachache walio na imani na hekima wakijenga Safina ya kuwakoa na gharika ya maji kwa maelekezo ya Mungu Mwokozi wao, "wajinga wengi na wenye hekima ya kibinadamu walikuwa busy kubeza na kusema;

"... oooh mwana Sayansi gani ame - approve mawazo ya ujenzi wa meli/Safina hiyo...!!"

AU

"....ooh, wanajenga safina kwa hearsay na kutosikiliza sauti za wanasayansi waliokwenda shule kwa gharama kubwa....!"

MATOKEO YAKE NINI?

Wote wakikufa na waliokuwa wanamwona mjinga (Nuhu) hajaenda shule na wenzake wachache wakapona....!!

Sikiliza ndugu...

God, The Almighty owns science. He is bigger than science...

Rev. Bishop Josephat Gwajima is the voice of the Almighty God. He sees beyond human science....

Shauri menu...
 
Mbona kwenye chanjo ya surua au polio mbona hizo side effects hazikutokea mpaka sasa; kwani chanjo ya corona?
Soma historia, fanya tafiti, usikurupuke...wapo ambao si side effect tu, wapo waliougua na kufa baada tu ya kupewa chanjo. Hakuna dawa yoyote isiyo na side effect!
 
Msikilizeni.

Kuna mambo yamo ndani ya yale anayoyaongea.
Mkuu wewe ni mtu makini sana hivi kweli mtu asiye na elimu ya virology au Epidemiology ndio achambue effectiveness ya chanjo??

Mfano anasema mpaka ifanyiwe uchunguzi..... Hvi ina maana TMDA au Mkemia Mkuu au ile Kamati ya Covid 19 wote hawana idea na hiko??
 
BIOLOGY TEST.

Jibu swali lifuatalo

1. Ukipata chanjo unaweza kupata corona? = Ndiyo

2. Ukipata chanjo unaweza pia kufa kwa corona? = Ndiyo

3. Ukipata chanjo unaweza kutembea bila barakoa? = Hapana

SWALI:
Kwanini upate chanjo?
 
Soma historia, fanya tafiti, usikurupuke...wapo ambao si side effect tu, wapo waliougua na kufa baada tu ya kupewa chanjo. Hakuna dawa yoyote isiyo na side effect!
Wapi huko Sisi tumepigwa chanjo miaka 50 imepita na kaka zetu,atukuona side effects,na tulipona wote labda waliokuwa wameathilika,huko Kongo ulikwenda lini kufanya utafiti?
 
Maswali ya kitoto! Mtu mzima haishii kuangalia hayo tu!! Kwa makusudi hujasema ambaye hajachanjwa anaweza kupata corona na anaweza pia kufa!!

Twende mbali zaidi - je ni wangapi kati ya wangapi waliochanjwa wanapata covid na hta kufikia tu kuumwa, achilia mbali kufa!

Kwa taarifa yako - hata ulipochanjwa polio. Walikusudia ikikupata isikuathiri - sio isikupate kabisa!!!
Nenda ukachanje sasa
 
Jifunze kutumia lugha ya kiungwana. Sie kila alie na maoni tofauti na weye hana akili.

Nimetoa maoni Mchungaji asikilizwe na si kubezwa.

Hayo pia ni maoni yangu haimaanishi kuwa naunga mkono ila nami pia nametoa maoni.
 
Mkuu wewe ni mtu makini sana hivi kweli mtu asiye na elimu ya virology au Epidemiology ndio achambue effectiveness ya chanjo??

Mfano anasema mpaka ifanyiwe uchunguzi..... Hvi ina maana TMDA au Mkemia Mkuu au ile Kamati ya Covid 19 wote hawana idea na hiko??
Sasa, kwa mfano wataka niambia dawa zimefika jumatatu zikapokelewa JNIA halafu kisha zikaenda maabara kuchunguzwa na kuangaliwa ubora wake?

Huwa yachukua muda upi?

Au TMDA, Mkemia Mkuu na kamati walienda hukohuko iliko chanjo na wakaifanyia upembuzi?

Lakini hata hivyo chanjo tayari ipo nchini, hivyo ni hiari kukudungwa sindano au mtu waacha.
 
Mawazo haya ya kijinga ya kupuuza sauti ya Mungu ndiyo yaliyowaangamiza kwa gharika ya maji watu wote wa dunia ya wakati wa Nuhu...

Walikuwa na arguments kama zako kuiweka "human science" juu ya NGUVU ZISIZOPIMIKA ZA MUNGU aliye hai...

Wakati Nuhu na wachache walio na imani na hekima wakijenga Safina ya kuwakoa na gharika ya maji kwa maelekezo ya Mungu Mwokozi wao, "wajinga wengi na wenye hekima ya kibinadamu walikuwa busy kubeza na kusema;

"... oooh mwana Sayansi gani ame - approve mawazo ya ujenzi wa meli/Safina hiyo...!!"

AU

"....ooh, wanajenga safina kwa hearsay na kutosikiliza sauti za wanasayansi waliokwenda shule kwa gharama kubwa....!"

MATOKEO YAKE NINI?

Wote wakikufa na waliokuwa wanamwona mjinga (Nuhu) hajaenda shule na wenzake wachache wakapona....!!

Sikiliza ndugu...

God, The Almighty owns science. He is bigger than science...

Rev. Bishop Josephat Gwajima is the voice of the Almighty God. He sees beyond human science....

Shauri menu...
duh...aise pole sana,hivi na mimi nikikwambia nimeambiwa na Mungu mtaangamia kwa kukosa maarifa utabisha au nikikwambia mimi ni nabii utabisha...usikubali kulishwa kila unachokisikia,Mungu ametujalia wanadamu utashi..chain ya utume ilishamalizika kitambo hao kina kibwetere watawaangamiza...amini amini nakwambia ataangamia yeyote yule anayemtukuza mwanadamu badala ya Mungu.
 
You must be joking ndugu.

Unamwongelea Gwajima yupi? Huyu huyu aliyedai anafufua wafu lakini akashindwa kumfufua rafiki yake kipenzi Magufuli?
Gwajima aliongea huku mishipa ya Mungu imemsimama kwamba corona haitaingia Tanzania Leo hii kabadilisha gia angani ni muongo sana
 
duh...aise pole sana,hivi na mimi nikikwambia nimeambiwa na Mungu mtaangamia kwa kukosa maarifa utabisha au nikikwambia mimi ni nabii utabisha...usikubali kulishwa kila unachokisikia,Mungu ametujalia wanadamu utashi..chain ya utume ilishamalizika kitambo hao kina kibwetere watawaangamiza...amini amini nakwambia ataangamia yeyote yule anayemtukuza mwanadamu badala ya Mungu.
Ajabu Mungu ametupa akili Kuna mjinga anaitwa gwajima anataka tuweke akili mfukoni, Ila atufanye fulsa, wafanyabiashara wa kiroho kama gwajima hofu yao ni kukosa ela endapo watu wataamin chanjo ndo hofu yao
 
1. Ukipata chanjo unaweza kupata corona? = Ndiyo

2. Ukipata chanjo unaweza pia kufa kwa corona? = Ndiyo

SWALI:
Kwanini upate chanjo?
Na sio tu corona kwanin unywe dawa mfano ukiumwa malaria, au typhoid kwanin unakunywa dawa na wakati kufa kufa utakufa, in short ukiumwa usinywe dawa yeyote kwa sababu utakufa tu
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
Hiyo nimeisoma.

Hata ule ugonjwa wa mafua kule Hispania au Spanish Flu nimeusoma pia hivyo naelewa.

Na huu ugonjwa ulisambaa duniani kwasababu ya vita kuu ya kwanza ya dunia na ni wanajeshi ndoi walisambaza ugonjwa.

Lakini pamoja na kutokuwepo dawa za kuua virusi (antiviral) na antibiotics wakti ule dawa za asili ziliweza kutumika.

Je, leo dawa za asili ni mbaya au tu kwasababu ya maendeleo ya kiteknolojia ndo yameleta dawa za chanjo kuwa tayari na kuidhinishwa mara tu ugonjwa unapolipuka?
Dunia ya leo ukiwa na opinion tofauti na wakubwa wewe ni uahini.
Ndiyo mana dawa za asili kipindi kile zilifanya kazi lakini hupati kumbukumbu kwamba zilifaa.

Turudi Tanzania, tena juzi tu, 2020! Juhudi za uongozi wa serikali kipindi hicho zilipelekea watu kutumia matunda na dawa za asili(kufukiza, tangawizi, etc) mbinu za kuondoa woga na tukaishinda korona! Lakini cha ajabu tusivyo na akili tumesahau kabisa kwamba ni jana tu tulivushwa kwenye janga hili hili!

Nchi jirani walifuata WHO protocals lakini korona iliwapelekesha sana tofauti na Tz tuliofuata Magufuli protocals .

Siyo bure akili zetu zilishachezewa uhenda kupitia chanjo kama ndui au vyakula vya GM nk
 
Back
Top Bottom