Richard, soma kidogo changamoto zilizoandama juhudi za kupambana na gonjwa lililowafyeka binadamu zaidi ya 300,000,000 miaka zaidi ya100 iliyopita. Gonjwa hilo lilijulikana kama
small pox.
Katika juhudi za kulitokomeza, soma upinzani ambao juhudi hizo zilipitia hadi dawa ya kwanza kabisa ya chanjo kupatikana na ilipatikanaje. Soma upinzani mkali uliandama matumizi ya chanjo hiyo.
Soma jinsi mtu moja alivyofungua kesi hadi makama kuu nchini Marekani (Supreme Court) kupinga chanjo hiyo na soma maamuzi ya mahakama hiyo na hatua zilizochukuliwa kuhakikisha chanjo inatolewa.
Soma wahubiri na manabii uongo walivyohusisha chanjo hiyo na mafundisho ya dini kama anavyofanya Gwajima hadi nguvu kutumika kwa kupita nyumba hadi nyumba kutoa chanjo hiyo kwa nguvu.
Watu wenye uelewa mdogo na wasiojua historia wanafikiri hii ni chanjo ya kwanza kupata upinzani mkali wa chanjo na wanatumia ujinga wao kupinga hii chanjo kwa sababu kama hizo hizo za karne zilizopita.
Hebu pitia hapa kidogo...
https://www.washingtonpost.com/history/2021/04/01/vaccine-supreme-court-smallpox-covid/