Do you have any? Please dont shout, convince me!Don't insult my intelligence.
Richard, I hope that's your name, wewe ni mtu wa siku nyingi humu, ongea kama veteran wa JF. Simply put ulichoandika hapa juu does not make any sense. Unavyojibu nakuwa na wasi wasi na uwezo wako kwani huna tofauti na viwavi vilivyosukumizwa humu na status quo kutetea kila tendo la watawala wetu.Nimeshauri mara nyingi humu kuwa Mbowe abadili strategy na haijawa hivyo miaka nenda rudi.
Kisha awe na strategists kumsaidia.
Siasa ni sayansi na yahitaji pia kusoma alama za nyakati kama kweli kuna nia thabiti ya kukiondoa chama kilichoshika dola kwa miongo kadhaa.
Vinginevyo kila anachofanya hata kama kina nia thabiti kinaonekana si sawa na anakumbana na madhila ya vyombo vya dola.
elimu yako kwanza mkuu ,tuijue,maana tunaweza tukawa tunabishana humu kumbe hata fani ya medicine huijui,kumbe wewe ni makenika.Kumbe na wewe hauna akili kama Gwajima? Umeandika utopolo mtupu! Kwanza hizo chanjo hazidhuru DNA kama wewe na Gwajiboy mnavyowadanganya watu.
Chanjo ya COVID-19 haibadili au kuingiliana na DNA yako kwa njia yoyote. Chanjo zote za mRNA na virusi vya virusi vya COVID-19 hutoa maagizo kwa seli zetu ili kuanza kujenga kinga dhidi ya virusi vinavyosababisha COVID-19. Lakini, nyenzo hizo haziingii kamwe kwenye kiini cha seli, ambayo ndio huhifadhiwa DNA yetu.
Pia Gwajima anasema hiyo COVID-19 itaisha yenyewe na hataki mwananchi yeyote apate chanjo. Hilo la kusema zipimwe “chemicals” zake, ni kama tu tayari keshaaminisha watu kuwa chanjo ni mbaya na kuzipima ni ili kusapoti hoja yake. Labda angesema zipimwe kwanza ndiyo maamuzi yafanyike, lakini yeye anaongea as if tayari keshafahamu kuwa chanjo ni mbaya. Angeacha kauli ambayo imeshatewa kuwa chanjo ni hiyari na siyo lazima. Lasivyo atakuwa responsible kwa watakaopoteza maisha yao kwasababu ya vitisho vyake.
Kuna wale wanaosema kuwa chanjo haizuii kupatwa tena na COVID-19. Ni kweli, lakini imetokea zaidi kwenye wimbi hili la “Delta variant”, hata hivyo, chanjo bado inasaidia wale waliochanjwa wasipate madhara makubwa yanayosababishwa na virusi hivyo ikiwemo kupelekwa hospitali na hata kupoteza maisha yao.
Muwe munajishughulisha kufanya viji “research” vidogo vidogo ili kuweza kuelewa jambo badala ya kukurupuka tu.
Na Kama yote hayo jibu ni ndiyo,Sasa hiyo inayosisitizwa watu wachanje ni NINI!? NA NI KWA NINI!???1. Ukipata chanjo unaweza kupata corona? = Ndiyo
2. Ukipata chanjo unaweza pia kufa kwa corona? = Ndiyo
SWALI:
Kwanini upate chanjo?
Wazifahamu gharama za kurusha Drone na kuiweka angani?Nimesoma mpaka hapa nikaacha!! Hivi kweli US haina uwezo wa kutupiga na jeshi letu hili la sahivi mpaka kwanza watufanye ''mazombie''???
Kwani wakituma drone 5 tu mbona zinatosha kutumaliza. Hawahitaji mabiliom ya chanjo ili tu kutumaliza ni kujipa sifa zisizokua na uhalisia.
Mfano madawa 90% yanatoka nje yote hayo wasiweke sumu ila eti chanjo pekee ndio sumu iwepo?? Are we serious? Hivi kuna silaha gani ya kivita imetengenezwa bongo? Kwanini usiwaze kwamba hta hizo silaha ma ndege vita zimepuliziwa elements za kuwamaliza wanajeshi wetu??
Yaani bidhaa moja tu ndio ina sumu? Ila bidhaa zote ambazo tuna import kila mwaka ndio zipo safe?? Are you serious
Hiyo ni fomu ya ruhusa/hiari kwa mchomwaji sindano mtarajiwa na mhudumu wa afya na mchomaji sindano.
Pasco hapo nadhani ni swala la kofia.Amepinga chanjo kwenye madhabahu ya kanisa katika nafasi ya uaskofu wake na sio kama Mbunge.....Mkuu Richard , kwanza asante sana kwa bandiko elimishi, mabandiko kama haya they add value kwa jf and to the society, thanks for this.
Pili hongera kwako binafsi, kutumia muda wako, uwezo wako na elimu yako kuwaelimisha wengine. Ni kupitia bandiko lako hili, mimi ndio nimejua na kuelimika kuhusu batch no. Hivyo maana yake kama Tanzania tumepatiwa hizo chanjo milioni 1, za JJ, ina maana hizo chanjo zitachanja watu 500,000 ili kuepuka kuisha na wengine kulazimika kutumia a different batch.
Suluhisho ni kuepuka chanjo za double jabs ni kutumia chanjo za single jab kama hii ya JJ huku bara, na ile Sputnik ya Urusi inayotumiwa Zanzibar, zote ni single jab, ukichanjwa, umechanja, you are done.
Nikirudi kwa Mchungaji Gwajima, kwa vile yeye ni kiongozi wa umma, ni mbunge kupitia CCM na pia kiongozi wa kiroho kwa waumini wa kanisa lake, hivyo ni mtu mwenye big influence, chochote atakachosema kina big impact, badala ya kupinga chanjo, nafuu akae kimya.
#COVID19 - Kama Taifa limekubali chanjo ndio maslahi ya Taifa, Viongozi wote wanakuwa Bind na A Collective Responsibility Clause. Must support, Shut up or quit!
Wanabodi, Nimemsikia Mbunge wangu Mhe. Askofu Gwajima akipinga chanjo ya Covid na sio tu kuhamasisha watu waikatae bali hadi kutishia kwa kuwahukumu kifo, wote watakao wachanja watu! Askofu wetu anahitaji kuelimishwa, kwanza yeye, kama Mbunge, ni mtumishi wa umma wa Watanzania wote, kisha ndio...www.jamiiforums.com
Kitendo cha Mwenyekiti wake, rais Samia kuhamasisha chanjo, halafu yeye kutoa maoni tofauti na kuhamasisha watu wasichanje,ni usaliti
P
Kaka, I'm humbled.Mkuu Richard , kwanza asante sana kwa bandiko elimishi, mabandiko kama haya they add value kwa jf and to the society, thanks for this.
Pili hongera kwako binafsi, kutumia muda wako, uwezo wako na elimu yako kuwaelimisha wengine. Ni kupitia bandiko lako hili, mimi ndio nimejua na kuelimika kuhusu batch no. Hivyo maana yake kama Tanzania tumepatiwa hizo chanjo milioni 1, za JJ, ina maana hizo chanjo zitachanja watu 500,000 ili kuepuka kuisha na wengine kulazimika kutumia a different batch.
Suluhisho ni kuepuka chanjo za double jabs ni kutumia chanjo za single jab kama hii ya JJ huku bara, na ile Sputnik ya Urusi inayotumiwa Zanzibar, zote ni single jab, ukichanjwa, umechanja, you are done.
Nikirudi kwa Mchungaji Gwajima, kwa vile yeye ni kiongozi wa umma, ni mbunge kupitia CCM na pia kiongozi wa kiroho kwa waumini wa kanisa lake, hivyo ni mtu mwenye big influence, chochote atakachosema kina big impact, badala ya kupinga chanjo, nafuu akae kimya.
#COVID19 - Kama Taifa limekubali chanjo ndio maslahi ya Taifa, Viongozi wote wanakuwa Bind na A Collective Responsibility Clause. Must support, Shut up or quit!
Wanabodi, Nimemsikia Mbunge wangu Mhe. Askofu Gwajima akipinga chanjo ya Covid na sio tu kuhamasisha watu waikatae bali hadi kutishia kwa kuwahukumu kifo, wote watakao wachanja watu! Askofu wetu anahitaji kuelimishwa, kwanza yeye, kama Mbunge, ni mtumishi wa umma wa Watanzania wote, kisha ndio...www.jamiiforums.com
Kitendo cha Mwenyekiti wake, rais Samia kuhamasisha chanjo, halafu yeye kutoa maoni tofauti na kuhamasisha watu wasichanje,ni usaliti
P
Huyo atakuwa MATAGA, anajaribu kulinda legacy kwa angle ya taalumaUmesema vyema mtaalamu, ni matumaini yangu hufungamani na chama chochote cha siasa, kinyume na hivyo, usingeweza kufikiria hata moja ya hoja ulizoainisha hapo.
Sijamtetea mtu yoyote nimeshauri tu kuwa Mchungaji asikilizwe.Richard, I hope that's your name, wewe ni mtu wa siku nyingi humu, ongea kama veteran wa JF. Simply put ulichoandika hapa juu does not make any sense. Unavyojibu nakuwa na wasi wasi na uwezo wako kwani huna tofauti na viwavi vilivyosukumizwa humu na status quo kutetea kila tendo la watawala wetu.
Maoni gani? Gwajima yeye anasema mtu yeyote asichanjwe. Wewe unasema asikilizwe kwa hilo?
Chanjo zenyewe ni hiyari, lakini mnaleta taharuki ambayo lazima itali cost Taifa. Subiri uone hii delta variant itavyowanyoosha ndiyo watie akili wenyewe.
Pia wewe umeona tu hapo pa kukosa uugwana, umeshindwa kujitetea uongo wako mwingine kuwa chanjo inaingia kwenye DNA.
Pia unataka tujifananishe na Urusi, China sijui na wengine waliotengeneza chanjo zao wenyewe. Hujui hayo mataifa kila kitu yanatengeneza vya kwao wenyewe? Unataka ionekane kuwa ni kwenye chanjo peke yake? Acheni kuleta taharuki, mna manufaa gani na wakati ni wazi kuwa chanjo ni hiyari?
Umeandika sana but hayo yote ni mawazo ya Kichawi.Utangulizi- Nawaomba Mods msihamishe uzi huu.
Mchungaji Josephat Gwajima asimamia maeneo mawili katika hoja yake.
Kwanza, kilichomo kwenye chanjo na pili chanjo dhidi ya wanajeshi na walinda usalama wa nchi.
La kwanza kuhusu kilichomo kwenye chanjo au (content).
Mchungaji Gwajima anadai ni lazima madaktari wajiridhishe kuwa kilichomo katika chanjo nyingi zilizowasili Tanzania jana ni sawa na kilichomo katika chanjo walopewa raia wa nchi zilizoendelea.
Itakumbukwa kuwa mapema mwaka huu nchi nyingi zilizoendelea zilipokea idadi kubwa ya chanjo za Covid-19 na kufikia mwezi Juni mwaka huu Marekani pamoja na Uingereza zikaanza kusema kuwa zitapeleka dawa zilizobakia katika nchi maskini.
Ahadi hiyo ilitolewa na Raisi Biden na Boris Johnson wa Uingereza katika mkutano wa nchi tajiri 7 au G7 ulofanyikia katika mji wa Cornwall nchini Uingereza.
Covid vaccine: UK and US to give leftover doses to poorer countries kupitia BBC Covid vaccine: UK and US to give leftover doses to poorer countries - CBBC Newsround
Lakini siku moja kabla ya mkutano huo raisi Biden aliahidi kutoa msaada wa dawa za chanjo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500-
US to donate 500 million Pfizer COVID-19 vaccine doses globally: Report- US to donate 500 million Pfizer COVID-19 vaccine doses globally: Report
Sasa tukirudi katika hoja ya mchungaji Gwajima kwamba lazima tuangazie kilichomo (Content) katika chanjo hizo zote ni ya kuzingatiwa.
Wenzetu wazungu wao walikwishajipanga vilivyo katika suala zima la kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO -19 na kwa muktadha huo waliweza kutengeneza vipeperushi na vielelezo vingine ambavyo zinalenga kumuelimisha mchanjwaji mtarajiwa kuwa ni aina ipi ya chanjo anaweza kupata, imetengenezwa vipi kwa kutumia nini, na inabeba vitu gani na kisha madhara yake baada ya kudungwa au "side effects"
Hivyo taarifa zoote kuhusu UVIKO-19 zimo katika tovuti za serikali za nchi zote zilizoendelea na mtu aweza kusoma na kuelewa bila shida.
Serikali ya Tanzania ingeweza kabisa kufanya hili ilipokuwa ikijiandaa kupokea chanjo na kuondoa uwezekano wa mijadala ambayo yaonekana wazi kuwa haiwezi kuzuia utekelezaji wa kudunga watanzania chanjo hizo.
Sasa hizo chanjo zina namba maalum au bechi au kwa kiingereza batch number hivyo pfizer yaweza kuitwa BNT163C1 au 161C2 na kadhalika.
Hizi namba zinatofautina na ukiwa umedungwa BNT163C1 basi ni lazima uje udungwe dozi ya pili ambayo ni kutoka katika bechi hiyohiyo yaani yaweza kuwa BNT163C3 lakini haiwezi kuwa BNT200b1 ambayo yaweza kuwa ndo inoleta madhara kama kuganda kwa damu.
Ni hivyohivyo kwa chanjo za Moderna, Johnson &Johnson na Moderna ambazo pia zinatumia bechi tofauti.
Moderna inayoyumika kwa mtu A yenye bechi namba 3001729 ndo hiyohiyo itayotumika kwa mtu huyohuyo A lakini itafuatia kidogo na kuwa 3001830.
Mtu anechanjwa Pfiser BioNTech ni lazima achanjwe dozi hiyohiyo ya chanjo hiyohiyo.
Nchi kadhaa za Ulaya na Marekani wakiangalia namba ya bechi ambayo msafiri amechomwa kuna ambao wanakataliwa kuingia katika nchi hizo kwa kuwa amechomwa chanjo ambayo ni ya kutoka kwenye bechi ambayo ina matatizo ya kuleta kuganda kwa damu na homa kali isokwisha.
Katika chanjo zote chanjo ya Oxford Astra Zeneca ndo chanjo ambao haihitaji baridi kali kuitunza hivyo kuifanya iwe rahisi kuihifadhi katika jokovu la kawaida kama yale ya majumbani.
Chanjo zingine zote huitaji majokovu maalum ambayo pia ni lazima yawe katika mazingira ya kutoweza kuvurugwa na waswahili au kuwa "compromised".
Hivyo hapa nina imani pia kuwa Serikali imewekeza vilivyo katika idara ya uhifadhi na ugavi wa chanjo hizi na hakutakuwa na dalili za kuzivuruga chanjo hizo.
Sasa basi, mchungaji Gwajima anadai ni lazima tujiridhishe kuwa dawa hizi za chanjo zina kiwango kilichomo (content) sawa na chanjo walochomwa wazungu huko Ulaya na Marekani.
Kwenye hili ana hoja kwani hatufahamu dawa hizi za chanjo zimepitia wapi, zimehifadhiwa vipi, zitabadilika vipi kiubora (yaani quality) na je zitaleta madhara yepi mwilini?
Lakini kwa kuwa dawa za chanjo zimekwishatua nchini na pamoja na maoni kadhaa yakiwemo niliyowahi kuyatoa huko nyuma kuwa tuwe waangalifu na chanjo hizi cha msingi ni kuanza na wale wananchi ambao wako hoi mahospitalini na wengine ambao wameathirika zaidi.
Kisha kama nilivyowahi kupendekeza huko nyuma ni kwamba serikali itengeneze makundi ya wataochanjwa na kuweka utaratibu kulingana na mahitaji yaani wazee, wale wenye hali tata kiafya na kisha wale wanotaka kusafiri kwenda nchi zingine ambako wanataka msafiri awe amechanjwa dozi mbili.
Nikija kwenye suala la pili kuhusu wanajeshi, watu wa usalama na wengine wenye majukumu mazito ya kuilinda nchi hii, hapa pia Mchungaji Gwajima ana hoja.
Tusishabikie tu kuwa kwa kuwa wanajeshi watachanjwa basi ni sawa, inatubidi kama taifa tuangalie maslahi ya taifa hili, usalama wake na mstakabali wake kwa miaka 5 na kuendelea.
Tujiulize ni kwanini Russia, Iran, Israeli, China na nchi zingine makini kwanini wao wametengeneza chanjo zao?
Vita ya sasa duniani imehamia kwa muda katika madawa, biolojia (bilogical warfare) kutoka kwenye vita ya kukimbilia silaha zingine.
Tukumbuke hakuna silaha mbaya sana kama silaha ya kibaolojia ambayo hukaa mwilini kwa muda mrefu usojulikana.
Hivyo viwanda vya madawa navyo vimeamua kujikita katika sekta hivyo ya vita kwa kushindana kutengeneza dawa za chanjo.
Si kwamba dawa hizi za chanjo hazikuwepo, bali kilichotokea ni kwa wenye viwanda hivi kufanikiwa katika kuomba fedha za ufadhili katika kufanya tafiti zao na suala la UVIKO-29 lilipoingia wote wakahamia huko.
Chanjo zote hizi zinatumia teknolojia maalum ili kuweza kutumwa kwenda mwilini na kukutana na chembechembe za damu, baada ya hapo ni utaratibu wa kubadili chembechembe hizi pamoja na Vinasaba au DNA na kutengeneza kitu kingine.
Hivyo je, baada ya miaka 5 hado 10 ijayo endapo rasilimali watu ya vyombo hivi vya ulinzi na usalama itaathirika Serikali itakuwa imejiandaa vipi maana hakutakuwa na jeshi imara, lenye uwezo wa kuilinda nchi ipasanyo dhidi ya uvamizi wowote wenye nguvu kubwa.
Hivyo haya Mchungaji Gwajima ana hoja asikilizwe na asibezwe kwani yeye anatumia jicho la tatu katika kuangalia na kusoma alama za nyakati.
Sie wengine wote tunapaswa kutafakari maoni kama hayo na kuyatumia katika kutafuta ukweli zaidi
Nimalizie kwa kusema mimi nilipokuwa nasoma sekondari enzi hizo, somo la jiografia lilikuwa ni moja ya masomo niloyapenda sana.
Kuna siku mwalimu alituuliza darasani nini vyanzo vya mmomonyoko wa ardhi na maporoko yake yaani "Landslide".
Lakini usiku wa jana yake palinyesha mvua kubwa sana na tukasikia kuna mifugo kadhaa imebebwa na na kusombwa na maji na kupotea ziwani.
Pia kulikuwepo na katetemeko kadogo ka ardhi yaani (Earth tremor) ambako kalisababisha nyumba kuyumba kidogo kwa muda wa dakika kadhaa.
Asubuhi katika kipindi mwalimu akasimulia juu ya ile "landslide" na vifo vya mifugo, kisha akauliza nini kinasababisha mmomonyiko wa ardhi khasa lile lilotokea usiku?
Mimi kwa kukumbuka ile hali ya usiku nikajibu kuwa moja ni tetemeko, na pili ni mvua kubwa pamoja na shughuli kama ukataji miti na ujenzi.
Mwanafunzi mwingine kajibu kuwa ni kuyeyuka kwa mapande ya barafu au Glaciers.
Mwalimu akatabasamu na kuinua kichwa kuashiria amekubaliana na majibu yote, lakini akamgeukia mwanafunzi mwenzetu na akamwambia" umesema Glaciers lakini hapa hatupo Greenland au Patagonia Pampas"
Akaendelea, "tujaribu sana kutafuta majibu katika mazingira tuliyopo kabla ya kwenda mbali na ng'ambo huko". akamaliza.
Hii sentensi yake sijaweza kuisahamu hadi leo na imenisaidia sana katika kutafuta masuluhisho ndani ya mazingira niliyopo.
Hivyo pamoja na misaada tuipatayo kutoka nje zikiwemo chanjo cha magonjwa kama UVIKO-19 bado tuna budi kama taifa kujiwekea utaratibu kuwa tunajenga maabara za kisasa na vituo vya kufanya utafiti na kuhakikisha tunamwaga fedha humo kutafuta chanjo ya UVIKO- 19 ya Kitanzania.
Kwa njia hiyo tutakuwa tumejitatulia matatizo yetu wenyewe kwa kutumia wataalam wetu wenyewe na rasilimali zetu wenyewe, huko nje tukazane kuomba misaada ya teknolojia.
Wacha upumbavu.Umeandika sana but hayo yote ni mawazo ya Kichawi.
Kwanza siyo bech ni Batch.
Hakuna mechanism ya ujinga kihivyo.
Ulaya wameoa na kuolewa Africa.
Huwezi kufikiri kwamba batch fulani watachomwa nani na nani hawatachomwa.
Mzalishaji yeyote atafuata taratibu zote zinazostahili.
Hujawahi kujua kwamba Tanzania tuna Mabigwa wa Virology mahiri kwa kiasi gani.
Gwajima is the Jack of all trades..
Hajui medicines na hatakaa ajue kwa sababu hataki kujifunza.
Tanzania ina wasomi wazuri wacha kabisa.
Tuna Machine za kisasa we acha kabisa.
Conspiracy ya Medicine ipo na zitaendelea kuwepo lakini siyo kwenye hali ya taharuki kama sasa.
Ziko Njia milioni kidogo.
Pandemic inatishia Usalama wa kila kiumbe hapa Duniani, plan ni kupambana nayo iondoke.
1. Ukipata chanjo unaweza kupata corona? = Ndiyo
2. Ukipata chanjo unaweza pia kufa kwa corona? = Ndiyo
SWALI:
Kwanini upate chanjo?