#COVID19 Tumsikilize mchungaji Gwajima, tusimbeze. Chanjo zote zina bechi tofauti na kuna nchi hukataa baadhi ya bechi na nyingine ni zile zilizobakia

Self declared Askofu wa ufufuo na uzima na Mh Mbunge wa CCM jumapili alitoavkauli chafu na matusi dhidi ya viongozi wa kitaifa hadharani kuhusu suala la chanjo la ugonjwa wa corona.Cha ajabu hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake.Kwa matusi yake alimjumuisha na Mh.RAIS NA MWENYEKITI WA CHAMA CHAKE.Sasa sisi walalahoi tunauliza ikiwa Mwenyekiti Mbowe alikamatwa kwa shutuma mbalimbali,Kwa nini huyu anayejiita Askofu na pia Mh mbunge hakamatwi na kuswekwa ndani kisha akapelekwa mahakamani.SWALI TUNALOLIULIZA NI KWA SABABU ASKOFU WA KANISA HAGUSIKI (UNTOUCHABLE),AU SABABU NI MH MBUNGE WA CCM ?IKIWA KUNA SHERIA MBALIMBALI ZA MAKOSA YANAYOSTAHILI KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA,YA KIWEMO YA HUYU ZIMEWEKWA NA HUYU ASKOFU /MHESHIMIWA HAJACHUKULIWI HATUA ZOZOTE,JE NCHI HII NI YA AINA GANI?NARUDIA KUULIZA KWA NINI ?TUAMBIWE UKWELI.

IMG-20210726-WA0028.jpg
 
Ukisikiliza hoja za serikali kuhusu chanjo hazikati kiu ya walaji!

Ni kweli chanjo ni hiari lakini je wananchi wana taarifa sahihi?

Yamkini chanjo ni salama kabisa, lakini kama serikali inabidi ijitathimini namna yake ya kutoa taarifa kwa wananchi ili wasiwe na mashaka!

Namna bora ya kutoa taarifa inayoaminika ni kuepuka kutumia watu waliowahi potosha umma kwa uongo!

Kuna viongozi walichangia sana kueneza uongo hapo awali, kuna kauli nyingi sana za uongo zilizotolewa na viongozi wakuu ikiwemo ile taharuki ya wananchi walivyohoji juu ya afya ya Rais Magufuli wakati ule na kujibiwa you buheri wa afya na baadae alipofariki walewale wakatangaza alikuwa mgonjwa na alilazwa Mzena!

Hivyo kutumia viongozi walewale kutangaza usalama wa chanjo inachangia sana kuwagawa wananchi!

Ikumbukwe hata ile barua ya wizara ya afya kuhusu wananchi kuchanjwa chanjo ya corona ilikuwa ni barua ambayo inatia mashaka!

1. Kwanza iliandikwa kwa Kingereza
2. Ilisema wazi kwamba serikali haitawajibishwa na side effect zitakazojitokeza
3. Haikuweka bayana ni chanjo aina gani tumeipokea kati ya zile mataifa mengine waliyoikataa!
4. Ile kamati haikuweka wazi ni chanjo ipi na ipi wamechunguza na kujiridhisha itakuwa bora kuliko zingine etc

Hivyo kutumia watu walewale walioaminisha kupuuzia barakoa na sayansi ya corona kwa kujifukiza, halafu walewale kuwatumia kuhamasisha chanjo ni makosa!

Rais angefanikiwa zaidi hili kama angepiga chini waziri wa afya na badala yake amteue yule (aliyekuwa Naibu Afya wakati ule, aliyesimama na sayansi tangu corona ya kwanza) ndugu Faustine Ndugulile.

Huyu ndiye angefaa kuitetea chanjo kama waziri wa afya!

Pia baadhi ya mawaziri wangewekwa kando ili kuleta imani, tatu waliokuwa mawaziri enzi za awamu ya tano wangenyamaza kimya kutokana na mlengo wao ulivyopotosha umma hapo awali!

Mwisho, Kutokana na kofia mbili za mchungaji Gwajima, Hawezi kubadili upepo wa waumini wake, anafahamu madhara ya kuwa na ndimi mbili madhabahuni, Hususani kipindi hiki ambapo idadi ya waumini wake wengi wamemkimbia kwa ujio mpya wa Mwamposa!

Kitendawili kwa Gwajima ni either anyamaze ili kulinda kibarua au apambane ili kulinda waumini!

Majibu yake Jumapili, ingawa Gwajima atambue siku hiyo hatutacheza mbali na hapo kwasababu tutamuomba tukatete nae kidogo kumuweka sawa baada ya ibada!
 
System awamtaki alafu hoja yake haina ushawishi wala mazara kwenye nchi ukitaka upotezwe hoji kuhusu huu muungano (anglia mashekh huwamsho) na katiba mpya (mbowe na chadema)
 
Gwajima ni mtu mdogo sana ndani ccm na ndani ya serikali hana chochote cha kumuogofya yeyote na kama akihitajika atashughulikiwa kiwepesi tu wala msimkweze kinafiki wakati tunamfahamu vyema kabisa.
Gwajima ana'watu'
 
CCM hawawezi kumfanya kitu mbunge yeyote yule maana wote wamekamata bakuli la mboga.
 
Gwajima ana wafuasi wa kanisa ambao kama akifanyiwa zengwe ujue ccm itakosa wafuasi wake.

Hakuna watu siwapendi kama walokole maana wanaendeshwa na mtu mmoja kwenye imani zao!
 
Mzozo dhidi ya chanjo ni mjadala wa Dunia nzima.

Hatua tuliyopo sasa ni chanjo ya hiari. Huko tuendako Wale wasio na chanjo ya uviko-19 watabaguliwa Kwa misingi ya kunyimwa ama kukataliwa huduma Fulani.

Vivyo hivyo nchi ambazo raia wake waliochanjwa ni wachache zitapoteza fursa za biashara ikiwamo utalii.

Hivyo wakati huu ni wakati sahihi kukata shauri ya ama tuunge mkono program ya chanjo Kwa faida za sasa na kesho ama tuipinge huku tukujipanga Kwa madhara ya uamuzi huu siku chache zijazo.
 
Self declared Askofu wa ufufuo na uzima na Mh Mbunge wa CCM jumapili alitoavkauli chafu na matusi dhidi ya viongozi wa kitaifa hadharani kuhusu suala la chanjo la ugonjwa wa corona.Cha ajabu hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake.Kwa matusi yake alimjumuisha na Mh.RAIS NA MWENYEKITI WA CHAMA CHAKE.Sasa sisi walalahoi tunauliza ikiwa Mwenyekiti Mbowe alikamatwa kwa shutuma mbalimbali,Kwa nini huyu anayejiita Askofu na pia Mh mbunge hakamatwi na kuswekwa ndani kisha akapelekwa mahakamani.SWALI TUNALOLIULIZA NI KWA SABABU ASKOFU WA KANISA HAGUSIKI (UNTOUCHABLE),AU SABABU NI MH MBUNGE WA CCM ?IKIWA KUNA SHERIA MBALIMBALI ZA MAKOSA YANAYOSTAHILI KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA,YA KIWEMO YA HUYU ZIMEWEKWA NA HUYU ASKOFU /MHESHIMIWA HAJACHUKULIWI HATUA ZOZOTE,JE NCHI HII NI YA AINA GANI?NARUDIA KUULIZA KWA NINI ?TUAMBIWE UKWELI.
Mkuu kuchanganya herufi kubwa na ndogo kitaalumu unakuwa kama unapiga kelele.
 
Ww una chuki binafsi! Askofu Gwajima katumia haki yake ya kikatiba kuhoji maswala ambayo bado hayana majibu juu ya chanjo uchwara hizi ambazo hazina tija na hata usalama wa muda mrefu haujurikani! Kama kusema ukweli kwako ni matusi basi hujielewi na hata ule uhuru wa kujieleza mliokuwa mnaushadadia hamuelewi maana yake! Pia napenda utambue hayo Gwajima amehoji na kuyasemea yana watz wengi sana nyuma yake! Hivyo kwa ufinyu wako wa upeo wa kuelewa mambo, ww unamwangalia askofu pekee!
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Mzozo dhidi ya chanjo ni mjadala wa Dunia nzima.

Hatua tuliyopo sasa ni chanjo ya hiari. Huko tuendako Wale wasio na chanjo ya uviko-19 watabaguliwa Kwa misingi ya kunyimwa ama kukataliwa huduma Fulani.

Vivyo hivyo nchi ambazo raia wake waliochanjwa ni wachache zitapoteza fursa za biashara ikiwamo utalii.

Hivyo wakati huu ni wakati sahihi kukata shauri ya ama tuunge mkono program ya chanjo Kwa faida za sasa na kesho ama tuipinge huku tukujipanga Kwa madhara ya uamuzi huu siku chache zijazo.
Kwa ndimi mbili
 
Gwajima ni mpotoshaji anatumia kila njia kubaki relevant. Nadhani akiongea tena aje na ushahidi wa study aliyofanya maana kwa uelewa watanzania Wana mwamini kuliko wataalamu wa afya.
 
Wangemvua uanachama halafu wanatangaza jimbo lipo wazi akili ingemkaa sawa. Utampingaje M/k wako tena hadharani.
 
Wangemvua uanachama alafu wanatangaza jimbo lipo wazi akili ingemkaa sawa.Utampingaje M/k wako tena hadharani.
Hapa itamaanisha kuwa chanjo Ni lazima. Jambo linapokuwa hiari yafaa watu waachwe huru kujadili kwa mitazamo yao, ili wafanye pia maamuzi kulingana na mitazamo yao.

Kama wananchi hawana taarifa sahihi na wanapotoshwa , in maana wajibu wa serikali Ni kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi, na huyu anaetajwa kupotosha anapingwa kwa hoja , Wala si kwa kutumia nguvu na ubabe. JamiiForums tumekwama wapi?

Mbona itikadi yetu siku zote huwa Ni kupinga hoja kwa hoja?
 
Miye nabaki kumpinga M/k hadharani na hoja ya chanjo bado ni hiari hata madame kalisemea kuwa ni hiari na siyo mara moja.
 
Ila tusimsahau Gwajima wa upande wa serikali anayesema yeye ameshachanjwa kwa hiyo yeye hachanjwi hadharani hata kama ni waziri. Yaani wenye majina ya Gwajima inabidi kuwa nao makini sana.
 
Gwajima ni mpotoshaji anatumia kila njia kubaki relevant. Nadhani akiongea tena aje na ushahidi wa study aliyofanya maana kwa uelewa watanzania Wana mwamini kuliko wataalamu wa afya.
Wataalam gani unawaamini wewe, ni hawa madaktari walotuambia juzi tujifukize?
 
Back
Top Bottom