1. SGR tiamaji tiamaji. Miaka mitano SGR iko Moro. Fedha hakuna hadi kakopa.
2. Rada ni mradi wa Kikwete, imefungwa awamu ya 5 baada ya terminal 3 kukamilika.
3. Labda barabara za mitaani. Hakuna mkoa aliojenga barabara ya kufika km 200. Kama ipo itaje.
4. Kajenga uwanja wa ndege mmoja tu, kwao Chato.
5. Ndege kanunua bila mipango ya kibiashara ndio manaa hasara kila siku. Ili kuficha hilo alikataza shirika la ndege lisikaguliwe na CAG. Katika kutapa tapa kibiashara akaona aue mashirika shindani japo haijasaidia.
6. Ujenzi wa vituo vya afya/hospitali- hii ni kweli.
7. Mikopo vyuoni ilikuwepo tangu enzi, tena ndio kaharibu kuliko alivyokuta. Zaidi kawanyima mikopo watoto waliosoma private.
8. Hostel za wanafunzi- hadhi ya urais si ya kujenga hostel mbili za milioni 500 kila mmoja. Rais wa nchi anasifiwa kwa hostel mbili?
Zaidi kaeneza chuki za kisiasa, ukanda, ukabila na kujenga matabaka. Mambo ambayo yalimgharimu sana Mwl kuyamaliza. Alikuwa anatupeleka kwenye mgawanyiko kama uliopo Kenya au Uganda