Mkuu
kavulata , ngoja nikupe shule ndogo kwanza uelewe uchumi wa kati ni nini maana unataka kumchosha dada angu
Sky Eclat.
Uchumi wa kati ni nadharia mojawapo inayotumiwa na benki ya dunia katika kupima maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali duniani. Benki ya dunia inazo nadharia 4 za kupima uchumi.
Ya kwanza ni Uchumi wa chini/Fukara (Low income economy). Hizi ni nchi ambazo wastani wa pato lake kwa mtu mmoja mmoja ni chini ya $1,035 (kama TZS 2.3M) kwa mwaka.
Pili ni uchumi wa kati wa chini (Lower-middle income economy). Hizi ni nchi ambazo wastani wa pato la mtu mmoja mmoja ni kuanzia $1,036 hadi $4,045 kwa mwaka. Kama TZS 2.3M hadi 9.2M.
Tatu ni uchumi wa kati wa juu / ulioimarika (Upper-middle income economy). $4,046 hadi $12,535 kwa mwaka. Sawa na TZS 9.2M hadi 30M kwa mwaka.
Nne ni uchumi wa juu (High income economy). $12,536 (Yani TZS 30M) na kuendelea.
Sisi tumeingia uchumi wa kati wa chini baada ya kufikia $1080, yani tumevuka mstari wa chini ($1036) kwa $44.
Kigezo gani WB hutumia kupima uchumi wa nchi?
WB inachukua pato ghafi la nchi (GNI) gawanya kwa idadi ya watu wote katika nchi. Yani unachukua kipato cha watu kama Bakhresa, Rostam, Mo Dewji, Diamond Platnumz, Bashite unachanganya na kipato cha mama ntilie wa Yombo Buza, fundi vibatari wa Irangi Kondoa, fundi makanika wa Ngudu Kwimba, halafu unagawanya kwa watanzania wote hadi aliyezaliwa leo. Kinachopatikana ndio kinaitwa wastani wa Pato la mtu mmoja mmoja (Per capita income).
So, kama nilivyosema kabla Tanzania iliingizwa uchumi wa kati wa chini baada ya GNI per capita kufika $1080.
Kila awamu imechangia lakini serikali ya awamu ya 5 imechangia kidogo zaidi kuliko awamu zilizotangulia. Yani serikali ya awamu ya 5 imefanya kumalizia tu kazi iliyofanywa na waliotangulia. Kama kumsukuma mlevi.
Kama kuna pongezi kidogo basi ziende awamu ya 4. Wakati Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 wastani wa pato la mtu mmoja mmoja lilikua $597. Mwaka 2010 akafikisha $740 (ongezeko la $143 kwa miaka mitano ya kwanza). Mwaka 2015 wakati anakabidhi madaraka lilikua $980 (ongezeko la $240 kwa miaka mitano ya pili).
Serikali ya JPM imepokea kijiti wastani wa pato la mtu mmoja mmoja likiwa $980 mwaka 2015. Na amefanikiwa kufikisha $1,080 , (sawa na ongezeko la $100 kwa miaka mitano). Hivi hapa anayepaswa kupongezwa zaidi ni nani? Aliyeongeza $240 kwa miaka mitano au aliyeongeza $100 kwa miaka mitano?
Awamu ya tano propaganda nyingi sana. Ndio maana alitaka asikike yeye tu ili haya msiyajue.