Tumuenzi Rais Magufuli kwa kubana matumizi yasiyo ya lazima

Binafsi sioni kumzunguusha hivi ni kumheshimu sana mwenzetu hasa keenye kipindi hiki cha mlipuko,
, bali ninaiona kama njia ya kuhatarisha maisha ya watanzania wake kwa misingamano na kueneza magonjwa ya njia ya hewa. Lakini pia kutumia hela ambazo hatunazo nyingi na muda wa kufanyakazi "hapa kazi tu" ambayo yrye alikuwa muumini wake. Naona kama tunaanza vibaya kitaifa na kimataifa msidha bila magufulu rip
 
Msafara wa Magufuli ulikua na magari 60, ni matumizi gani aliyoyabana? Tunamuenzi jinsi alivyoishi kasoro tu hakuna wa kugawa pesa barabarani sasa hivi.
Kama ni hivyo ilikuweje Bank ya dunia (WB) ikaiingiza Tanzania kwenye uchumi wa kati? mbona haikuwa hivyo vipindi vya nyuma? wewe una chuki tu isiyojulikana.
 
Kama ni hivyo ilikuweje Bank ya dunia (WB) ikaiingiza Tanzania kwenye uchumi wa kati?
Mkuu kavulata , ngoja nikupe shule ndogo kwanza uelewe uchumi wa kati ni nini maana unataka kumchosha dada angu Sky Eclat.

Uchumi wa kati ni nadharia mojawapo inayotumiwa na benki ya dunia katika kupima maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali duniani. Benki ya dunia inazo nadharia 4 za kupima uchumi.

Ya kwanza ni Uchumi wa chini/Fukara (Low income economy). Hizi ni nchi ambazo wastani wa pato lake kwa mtu mmoja mmoja ni chini ya $1,035 (kama TZS 2.3M) kwa mwaka.

Pili ni uchumi wa kati wa chini (Lower-middle income economy). Hizi ni nchi ambazo wastani wa pato la mtu mmoja mmoja ni kuanzia $1,036 hadi $4,045 kwa mwaka. Kama TZS 2.3M hadi 9.2M.

Tatu ni uchumi wa kati wa juu / ulioimarika (Upper-middle income economy). $4,046 hadi $12,535 kwa mwaka. Sawa na TZS 9.2M hadi 30M kwa mwaka.

Nne ni uchumi wa juu (High income economy). $12,536 (Yani TZS 30M) na kuendelea.

Sisi tumeingia uchumi wa kati wa chini baada ya kufikia $1080, yani tumevuka mstari wa chini ($1036) kwa $44.

Kigezo gani WB hutumia kupima uchumi wa nchi?

WB inachukua pato ghafi la nchi (GNI) gawanya kwa idadi ya watu wote katika nchi. Yani unachukua kipato cha watu kama Bakhresa, Rostam, Mo Dewji, Diamond Platnumz, Bashite unachanganya na kipato cha mama ntilie wa Yombo Buza, fundi vibatari wa Irangi Kondoa, fundi makanika wa Ngudu Kwimba, halafu unagawanya kwa watanzania wote hadi aliyezaliwa leo. Kinachopatikana ndio kinaitwa wastani wa Pato la mtu mmoja mmoja (Per capita income).

So, kama nilivyosema kabla Tanzania iliingizwa uchumi wa kati wa chini baada ya GNI per capita kufika $1080.

mbona haikuwa hivyo vipindi vya nyuma? wewe una chuki tu isiyojulikana.
Kila awamu imechangia lakini serikali ya awamu ya 5 imechangia kidogo zaidi kuliko awamu zilizotangulia. Yani serikali ya awamu ya 5 imefanya kumalizia tu kazi iliyofanywa na waliotangulia. Kama kumsukuma mlevi.

Kama kuna pongezi kidogo basi ziende awamu ya 4. Wakati Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 wastani wa pato la mtu mmoja mmoja lilikua $597. Mwaka 2010 akafikisha $740 (ongezeko la $143 kwa miaka mitano ya kwanza). Mwaka 2015 wakati anakabidhi madaraka lilikua $980 (ongezeko la $240 kwa miaka mitano ya pili).

Serikali ya JPM imepokea kijiti wastani wa pato la mtu mmoja mmoja likiwa $980 mwaka 2015. Na amefanikiwa kufikisha $1,080 , (sawa na ongezeko la $100 kwa miaka mitano). Hivi hapa anayepaswa kupongezwa zaidi ni nani? Aliyeongeza $240 kwa miaka mitano au aliyeongeza $100 kwa miaka mitano?

Awamu ya tano propaganda nyingi sana. Ndio maana alitaka asikike yeye tu ili haya msiyajue.
 
Comments reserved
 
Ndugu yangu aliyemalizia mbio wa kwanza kwenye round ya mwisho ndiye mshindi, haijalishi ulikuwa ukiongoza round zote. Kwani JK na JPM nani alikuwa akikusanya kodi kodi kuliko mwenzake? kigezo kimojawapo cha kukuza uchumi ni kukusanya kodi. GDP na GNP vitakuaje kama hukusanyi kodi, hilo pato utalipaje? wacha upotoshaji
 
Tata kongole kwako maana watu hawakuona ufujaji wa wazi wa pesa ambao mkulu alikuwa anaufanya kwa kisingizio cha uzalendo.
 
 
Tata kongole kwako maana watu hawakuona ufujaji wa wazi wa pesa ambao mkulu alikuwa anaufanya kwa kisingizio cha uzalendo.
Misafara ya Dar mpaka Chato magari ya kutosha, mafuta, posho, yaani ikulu 3, Dar, Dodoma na Chato. Zote zinaendeshwa na kodi za wanyonge!
Jamaa alibania wengine na yeye kujiachia kutumia apendavyo.

Ninasubiria binafsi hiyo Mfugale terminal kuiona ikipokea ndege na wageni watalii wa kutosha kwenda Chato pine & cypress forest!
Unafiki wa ATCL kupeleka route huko kwa sababu za kisiasa, tutaushuhudia.

Huyu Mfugale huyu, tutasikia mengi jamaa kaondoka. Inashangaza structure za zipewe kitaifa zipewe majina ya maswahiba.

Otherwise R.I.P mahali alipojiandalia.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Jamaa wanatibu njaa zao za miaka 6 chini Magufuli, nina mashaka hata Rais Samia kama ameushitukia mkakati huo wa matumizi makubwa yenye harufu ya ufisadi na kuhatarisha maisha ya wanyonge kwa kukanyagana na Covid 19
 
Matumizi yasiyo ya lazima ya kununua wabunge na kurudia uchaguzi kwa mwamvuli wa kuunga juhudi mkono
 
...

Kama hayo ni ya kweli, wale wanaofurika, kulia na kutandika nguo zao barabarani kwenye msiba wa JPM ni akina nani kama hajafanya kitu kwao? Wanalia nini? Ni wanafiki? Wanadanganya? Ebhanae!!!
Walilipwa hujui hili pole sana
 
Alinunua wapinzani na kufadhiri magenge ya kigaidi dhidi ya wapinzani wake
 
Hujui kama kubana matumizi ndo kunaleta umaskini mana pesa hazitakuwa zinazunguka!
 
Kujenga uwanja wa ndege na kuweka traffic light Chato, ni matumizi ya ovyo ya pesa za umma!
Kuna watu walisambaza umeme hata kwenye migomba yao vijijini wakati makao makuu mikoa mingine haina umeme, je, hayo yalikuwa matumizi sahihi? kama uwanja wa chato ungekuwa umejengwa Hai kusingekuwa na maneno. KUMBUKENI kuwa kulikuwa na mkoa ambao ulikuwa na shule nyingi sana za msingi na serikali ambazo zilikuwa zinahudumiwa na serikali kwa walimu, ruzuku, mitihani, ukaguzi, nk, yaani kodi nyingi za wananchi zilikuwa zinaelekezwa huko kwa kisingizio kuwa walijenga shule wenyewe kwa kujitolea, lakini wakasahau kuwa serikali inaingia ghalama nyingi kwenye shule hizohizo za kujengwa na wananchi.
 
Jibu hoja kwa hoja mkuu.

Hao watu waliojazwa propaganda za mtu aliyetaka aongee peke ake, media zimsifu wakati wote, wasaidizi wamtaje kila sentensi ndio ushahidi wa mambo makubwa aliyofanya?
Hatushangai, hata gadaffi aliuawa na watu wake aliowapenda sana.
 
Airport ya Chato ilikuwa na faida gani kwa Taifa Kama Magufuli alikuwa akibana matumizi?
Acheni kulisifia Hilo jizi la majizi

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada ni Zezeta la Lumumba, Magufuli was a concrete Devil [emoji48]

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…