jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Nipende kusema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji vya watu wa kipekee wenye kuasisi mambo mengi ambayo baadaye huchukuliwa na watu wengine duniani na kuwa sehemu ya ufanisi wa matarajio ya wanadamu.
Ukiweka pembeni unafiki basi hutaacha kuona namna gani mteule wa Mhe.Rais ndugu Makonda Paul Christian anavyoendelea kuonesha jitihada na kuishi kipaji chake au karama aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu inayosindikizwa na busara kubwa za Viongozi wetu wenye maono ambayo iliona yupo mtu huyu ambaye anaweza kuwa ni msaada kwa Taifa.
Paul Makonda kama tulivyo binadamu wote ni mtu mwenye asilimia zake za mapungufu na asilimia zake za mema.
Tumemuona kama wanadamu katika mapungufu yake na katika mazuri yake.
Leo nichukue fursa ya kumpongeza kwenye mema yake anayojitahidi kuyafanya na nimtie moyo kusimama katika mstari wa mema hayo.
nimuase pia katika kuyatafajari mabaya yake halisi na yale yote yaliyompelekea kutuhumiwa ayafanyie kazi ,akiri ama kuomba radhi katika nyakati zinazofaa na mazingira staatabu tunayoyatambua.
Zaidi nipende kumuombea kwa Mungu aendelee kumuongoza katika hekima kubwa ya kiroho, kidini, kimila na zaidi kizalendo.
Niendelee kumuombea awe na kiasi, usikivu, tulivu na subra.
Niwasihi wasiompenda wabadili mioyo na hulka na historia ..lakini zaidi wamuombee na kumsamehe kama kweli alipitiwa na kukosea.
lakini itoshe kusema kama Taifa ipo haja ya kuendelea kumjenga vyema MWAMBA MPYA HUYU WA KASKAZINI.
Mada hii inakuja baada ya mfuatano wa matukio ya kipekee anayoyafanya sasa kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
kila la kheri comrade SAUL CRISTIANO MAKONDA.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Pia Soma: Paul Makonda: Tutakachofanya Tarehe 9 Arusha hata wakisema ni uchawi poa tu