Tuna akiba ya pesa dollar bilion 5.3

Huo ndo mpango so far...hata idadi ya sample zinazopimwa zinapanda,though hatujawekwa wazi....Japo na maombi si ya kubezwa pia

Maombi tumeomba kabla hata ugonjwa haujaingia ili usije, lakini bado umekuja. Sasa hatua ya maombi iachiwe viongozi wa dini wahamasishaji, rais yeye ni kutoa fedha ili vinunuliwe vipimo vya kukidhi uhitaji wa sehemu mbalimbali za nchi. Mbona kwenye ndege zilitolewa hela haraka haraka, ni kipi kinafanya serikali iwe wazito kwenye hii dharura inayokula maisha ya wananchi? Kwahiyo ndege ni muhimu kuliko uhai wa watanzania?

Kwa haya yanayoendelea bado nazidi kuamini Magufuli ni rais wetu, lakini sio rais sahihi kwa nchi yetu. Ingekuwa wapinzani wanasema wataandamana ungeona askari wakijazana mitaani ili kulinda madaraka yake, lakini watu kufa kwa ugonjwa sio tatizo maana hakuathiri madaraka yake.

Cc: Chagu wa malunde
 
Hiyo Akiba ndio muda wake huu kutumika, au hujui kuwa hiyo akiba ni ya kutumika kwa mazingira haya? Je kama hazitatumika sasa, hizo fedha ni akiba kwa ajili ya hali gani?
Huyo ndio JIWE. Always meticulous! Hatoi maamuzi kwa mihemuko!
 
Kwahiyo unataka hela yote ya hazina itumike kutibu korona?
fedha zikiisha na korona akazidi kupamba moto kipi kitafuata?
Tujaribu kutumia akili na sio mihemko ya kisiasa hasa kwenye mambo ya Kitaifa.

Rubbish. Kutaja “taifa” katika utetezi wako hakufanyi uwe na point. Point hapa ni kuwa nchi ichukue hatua za kuokoa uchumi SASA HIVI!! Na si kwa kungoja mkopo kutoka kwa mabeberu!! Tutumie pesa za ndani sasa!!
 
Alikuwa amelewa mataputapu siku hiyo akajkuta anabwatuka kauli za uongo
 
Kwa hiyo sababu ya chuki na mkuu wa nchi ndio ukaamua kuunganisha ujumbe wako na kichwa cha habari! Alafu mpaka sasa kuna mapungufu yoyote katika kuhudumia hawa waliougua kwa bahati mbaya mpaka anyofoe toka akiba iliyopo?

Chuki ipi, ukweli ni kuwa rais ndio mwenye uwezo wa kutoa pesa hazina bila kusubiri ruhusa kwa mtu au taasisi yoyote, na ameshafanya hivyo zaidi ya mara moja. Ndio maana kuna kilio kuwa rais anajali vitu kuliko watu. Kwenye huu ugonjwa uzito wake kwenye maamuzi unazidi kudhibitika.
 
Hiyo Akiba ndio muda wake huu kutumika, au hujui kuwa hiyo akiba ni ya kutumika kwa mazingira haya? Je kama hazitatumika sasa, hizo fedha ni akiba kwa ajili ya hali gani?
Zitatumika kuhonga wakati wa uchaguzi mkuu
 
Huyo ndio JIWE. Always meticulous! Hatoi maamuzi kwa mihemuko!

Sema kuwa hatoi pesa kwenye mahitaji ya watu, ila ingekuwa ni kwenye vitu angefanya hivyo. Hapa sio suala la mihemko, rais badala ya kutoa pesa vinunuliwe vifaa tiba kwa ajili ya ugonjwa unaoshika kasi, yeye anataka watu wasali ili ugonjwa uishe! Una akiba ya $5.3b kama 12t tshs, kisha una kipimo kimoja cha ugonjwa nchi nzima, unaokula maisha ya wananchi wako kisha useme hafanyi maamuzi ya mihemko! Huu sio utetezi bali ni wendawazimu.
 
Ngoja tuone mwisho wake
 
Kwani hujaona amehamisha pesa za sherehe za Muungano wa Tanzania zikatumike Zanzibar kupambana na hili janga. Au ulitaka atoe maamuzi gani? Au zile kwa ajiri ya sherehe za Mwenge hujaona kama ni hatua amechukua?
 
Chuki zako zinavuka mipaka rafiki. Had I unatia kinyaa...!! Endelea kuabudu wakoloni
 
Weka kwanza ushahidi unaoenesha kuwa alisema atawashighulikia nafisadi na wanyonyaji wanakula jasho la walahoi kisha uniambie katika kipindi chache cha miaka mitano nani kashughulikiwa Kati ya fisadi na mlalahoi?
 
Chuki zako zinavuka mipaka rafiki. Had I unatia kinyaa...!! Endelea kuabudu wakoloni
 
Chuki zako zinavuka mipaka rafiki. Had I unatia kinyaa...!! Endelea kuabudu wakoloni
 
Kwani hujaona amehamisha pesa za sherehe za Muungano wa Tanzania zikatumike Zanzibar kupambana na hili janga. Au ulitaka atoe maamuzi gani? Au zile kwa ajiri ya sherehe za Mwenge hujaona kama ni hatua amechukua?

Kuna kipimo kimoja mpaka sasa nchi nzima cha huo ugonjwa. Je huko Zanzibar nako kuna kipimo cha huo ugonjwa baada ya hiyo pesa ya muungano kupelekwa? Ni kweli kuna hatua amechukua, lakini hatupimi hatua tu, bali tunapima hatua stahiki.
 
Rekebisha kauli yako. Kuna maabara moja tu ambayo ni maabara ya taifa sio kipimo.Ukisharekebisha rudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…