Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Huo ndo mpango so far...hata idadi ya sample zinazopimwa zinapanda,though hatujawekwa wazi....Japo na maombi si ya kubezwa pia
Maombi tumeomba kabla hata ugonjwa haujaingia ili usije, lakini bado umekuja. Sasa hatua ya maombi iachiwe viongozi wa dini wahamasishaji, rais yeye ni kutoa fedha ili vinunuliwe vipimo vya kukidhi uhitaji wa sehemu mbalimbali za nchi. Mbona kwenye ndege zilitolewa hela haraka haraka, ni kipi kinafanya serikali iwe wazito kwenye hii dharura inayokula maisha ya wananchi? Kwahiyo ndege ni muhimu kuliko uhai wa watanzania?
Kwa haya yanayoendelea bado nazidi kuamini Magufuli ni rais wetu, lakini sio rais sahihi kwa nchi yetu. Ingekuwa wapinzani wanasema wataandamana ungeona askari wakijazana mitaani ili kulinda madaraka yake, lakini watu kufa kwa ugonjwa sio tatizo maana hakuathiri madaraka yake.
Cc: Chagu wa malunde