Tuna safari ndefu ngumu na ya hatari watanganyika kujinasua toka kwenye makucha ya wana mtandao

Tuna safari ndefu ngumu na ya hatari watanganyika kujinasua toka kwenye makucha ya wana mtandao

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Nilisema kwenye mada zilizopita kwamba kundi la mtandao ni kubwa na lenye ukwasi wa kueleweka walioupata hapa hapa Tanganyika

Hawa ndio wanafaidi keki ya taifa la Tanganyika.. Njia zote kuu za uchumi wamezishikilia wao! Wana sauti na maamuzi kwenye kila kitu.. Huu ni ukweli mchungu na wa kuumiza sana!

Taswira zilizojitokeza pale Mlimani city kwenye hafla ya harambee ya CCM... Lile kundi mliloliona lote, ni nani Kati yao

Atapenda katiba mpya kwa maslahi ya wote?
Atapenda uchaguzi huru wa wazi na wa haki?
Atapenda kuiona ccm inapigwa chini?
Atapenda kuiona CHADEMA chini ya Lissu na Heche inashinda uchaguzi mkuu?

Kushindwa kwa ccm na kushinda kwa CHADEMA kuna maana moja tu kwao! Mwanzo wa mwisho wa kuliibia taifa la Tanganyika!

Mwisho wa rushwa za kutisha
Mwisho wa ufisadi wa kutisha
Mwisho wa kuuza rasilimali za Tanganyika kwa bei sawa na bure! nknk

Kwenye ulaji na kujipata ni heri mara million mia upambane na fukara asiye na kitu kuliko tajiri aliyejipata kwa dhuluma, wizi na ufisadi
CHADEMA chini ya Lissu na Heche kushika madaraka ya Tanganyika kutahatarisha maslahi yao vibaya sana! Hili kundi liko tayari KUFANYA CHOCHOTE KIBAYA ili ccm ibaki madarakani.. !

Kwa hofu ya CHADEMA chini ya Lissu na Heche ndio maana wanafanya kila mbinu chafu kuangamiza hiki chama na viongozi wake.. Barua ya Lissu ya jana toka gerezani inaumiza sana sana!

Kundi la mtandao limejipanga hasa kutoka sasa mpaka 2050 na kuendelea.. Limejipanga toka chini mpaka juu kabisa! Kelele za Watanganyika kwao ni kejeli kubwa

Kuna tetesi zisizokoma kwamba uchaguzi umeshakwisha na nani atakuwa wapi na kwenye nini tayari mikeka imeshapangwa! Hivyo iwe mvua liwe jua ni lazima kundi la mtandao liibuke kidedea kwa mtazamo wao
Wana pesa, wana vibaraka wana chawa kwanini washindwe ? Tumewapoteza ndugu zetu wengi sana waliojaribu kupaza sauti zao kwa ajili yetu.. Wengine wamepitia na wanapitia madhila makubwa kwa ajili ya Tanganyika

Wengine wamepata ulemavu wa kudumu
Wengine wamebambikiwa kesi zisizo na dhamana
Wengine wameacha yatima na wajane nknk.. Yoote kwa ajili ya kuipigania Tanganyika!

Safari ya kuikomboa Tanganyika si lelemama ni ngumu na iliyojaa kila aina ya hatari kwakuwa inapora ulaji na madaraka ya walafi wasio na chembe ya uchungu na hili taifa!

Mungu pekee ndiye anaweza kuamua huu ugomvi! Tuzidishe maombi maana kukichwa kutambazuka..!!!
 
IMG-20250814-WA0039.jpg
 
Maombi bila hatua ni umbumbumbu, hata Mungu anatuambia kujipigania wenyewe, Hakuna Taifa ambalo lilikombolewa kwa maombi pasi na kuchukua hatua.

Mauaji, utekaji, uzandiki, ufisadi na kuonea watu hakuondolewi na maombi, ni kuchukua hatua dhidi ya mamlaka. Wakenya hawapiganii Taifa lao kwa maombi, ni kupinga kwa vitendo kwa kuugomea utawala uliopo madarakani kwa vitendo.

Wapigania uhuru wetu wangesema wakeshe makanisani na misikitini wafanye maombi ili mkoloni aondoke sidhani kama tungekuwa hapa leo hii. Mfumo hasi hupingwa kwa uasi dhidi ya mfumo wenyewe.

Yaani kakikundi ka watu 1000 wanaitafuna Nchi na watu zaidi ya 70M tupo tu tunawaangalia, Alieturoga sisi k*mamake zake huko aliko.
 
View: https://www.facebook.com/share/v/1CSQxfUbi6/
 
Hakuchunga athari ya akitoacho kwenye ndimi yake, Uchawa na kujipendekeza kukuzidi matokeo yake ndio haya.

Ameitumia nembo ya Yanga vibaya sana, Yeye kwa niaba ya Yanga ndio anatakiwa kuomba radhi kwa upuuzi aliofanya na kuahidi kuwa hatorudia tena.
Sio yanga tu hata simba zote hizi ni timu zinazotumika kupumbaza watu
 
Sukuma Ganga hawakuwa smart kama waliruhusu Magufuli aondoke kirahis that was a mistake.
Nyinyi si mlimpinga na kumwita dictator...haya yanayo tokea ni FUNZO KWA WAPUMBAVU WOTE NCHINI ...JPM ALITAKIWA KUWA DICTATOR MARA 7 YA ALIVYO KUWA ILI KUNYOSHA NCHI ...nchi inaibiwa wapumbavu wanasema tutashitakiwa MIGA....Tulionya kuhusu mwanamke kuwa viongozi wapumbavu wakaleta kauli zao za kipumbavu na kianithi kuwa
👉mama ana akili kwa sababu amekuzaa .
👉bora unitukanie baba yangu kuliko mama yangu.
👉mwanamke ni mungu wa pili.
👉hakuna kama mama.
👉laana ya mama ni kali kuliko baba
HIZI KAULI ZILISIKIKA KUTOKA VINYWANI MWA WATU WAPUMBAVU WENYE UANITHI WA AKILI
 
Ni kweli alikuwa dictator uchwara na alikuwa na akili ndogo Sana .
 
Back
Top Bottom