Tuna Waziri wa Nishati asiyefaa hata kidogo. Huwezi kulazimisha Watanzania kupikia gas wakati purchasing power yao ni duni

Tuna Waziri wa Nishati asiyefaa hata kidogo. Huwezi kulazimisha Watanzania kupikia gas wakati purchasing power yao ni duni

Kwani mkuu, lengo la mjadala wa kitaifa ni nini kwa ufahamu wako ?

Si ni kujua changamoto zilizopo na kuzitafutia namna bora ya kuziondoa ili mfanikishe jambo lenu kama taifa ?

Kama shida ni bei, tutajua tufanyeje ili kupunguza hiyo bei ili kila mmoja aweze kumudu bei. Kama changamoto ni usambazaji (coverage), kama taifa tujue tunafanyaje kulitatua.

Ni kwanini mnataka kulifanya hili suala lionekane kama haliwezekani kabisa ?
Lengo ndo hilo mkuu lakini sijui uelewa wa watu ukoje.
 
Na mama yenu kaanza kupigia chapuo.
Eti nishati safi amtue mama kuni.
Kuna hela hizi za mikopo-tozo zitapigwa vizuri sana hapo.
Kisa kumtua mama kuni
 
Kwamba asilimia 80 ya watanzania wanaoishi maisha ya kubangaiza waweze kupikia gas?

Hii ni ndoto. Yaani mtu anaishi chini ya dola moja halafu unapigia debe Taifa gas?

Huku ni kuwatukana raia masikini.
Ni kweli. Ameonyesha jinsi maisha mazuri aliokulia yalivyomuathiri. Hajui hali halisi ya Watanzania. Yaani mtu hana uhakika wa chakula na malazi, halafu unajifanya kuhamasisha kutumia gesi? Ni kichekesho. Tena hamasa ya domo, sio ya kiuchumi.
 
Mazao ya chakula wameshindwa kuthibiti bei, ndio wataweza kuwashawishi watu maskini kutumia nishati ya gesi?
 
Kuna viwanda vinatumia kuni kwenye boiler badala ya makaa ya mawe au mafuta. Waanze nao kwanza.
 
Huyu kijana mnamraumu bureeeeeeeeee .......kila makamba anachokifanya kina baraka zote kutoka juuuuu, juuuuuuuu, juuuuuu, juuuu kabisa
 
Kwamba asilimia 80 ya watanzania wanaoishi maisha ya kubangaiza waweze kupikia gas?

Hii ni ndoto. Yaani mtu anaishi chini ya dola moja halafu unapigia debe Taifa gas?

Huku ni kuwatukana raia masikini.
Yawezekana Serikali ikaweka ruzuku kwenye gesi, ushauona mpango mkakati wa Waziri?

Wananchi wakishaanza kuhoji utendaji wa Serikali kuu basi ni tatizo kubwa, mipango yote unayoletwa na CCM wananchi tunakuwa na wasiwasi nayo sababu historia inawahukumu, ina longo longo kibao.

Mipango ya maji safi toka Mzee Lowassa akiwa Waziri hadi leo hamna kitu, hatuna mpango wa maji ya uhakika mijini.
Mipango ya Umeme toka ile kampuni ya kitapeli ya SA chini ya Rais mstaafu Mkapa hadi leo hamna kitu.

Ni kweli wananachi wanakuwa na wasiwasi na haya mambo mengine ya Gesi ya kupikia kwa wote pamoja na hili la Bima ya afya kwa wote- tunaona kama magumashi na kupotezea muda ili tufike 2025 kwenye uchaguzi tukiwa na matumaini hewa.

Kifupi CCM haiaminiki kwa ujumla wao na kama kweli kuna nchi ya ahadi basi watanzania tutafika tukiwa tumechoka sana.
 
Kwamba asilimia 80 ya watanzania wanaoishi maisha ya kubangaiza waweze kupikia gas?

Hii ni ndoto. Yaani mtu anaishi chini ya dola moja halafu unapigia debe Taifa gas?

Huku ni kuwatukana raia masikini.
Yaani ni vichekesho tupu, huku mjini hadi wenye kazi za mishahara wanashindwa kununua gesi kwa wakati kutokana na bei kuwa juu na bajeti zao kuwa tight.....mtu wa kijijini ambaye kuipata jero tu ni mtihani ndo apate pesa ya kujaza mtungi wa gesi kweli!?
 
Mwanzoni nilimtetea kaulizake oor tunatengeneza miundominu sasa muda umekuwa mrefu hakuna umeme wa kutosha inchi nzima kila siku kata kata. Rais furumusha huyu hakusaidii, mrudishe kwenye chama kwani ni organiser mzuri wa sarakasi za kupata/kutengeneza kura atakusaidia 2025. Otherwise hafai kabisa
 
Na mama yenu kaanza kupigia chapuo.
Eti nishati safi amtue mama kuni.
Kuna hela hizi za mikopo-tozo zitapigwa vizuri sana hapo.
Kisa kumtua mama kuni
Anamtua mama kuni kwa lipi?
 
Kabla ya kuendelea na mjadala lazima tujiulize haya:
-Kupaa kwa gharama ya gas ghafla

- Nani mmiliki wa Taifa Gas?
-Kwanini January anapromote Taifa Gas na Sio Lake gas au Oryx?
Ukipata majibu ya haya maswali utajua kwamba Kuna Jambo ambako lipo nyuma ya hii campaign.

Siku zijazo tutarajia mjadala juu ya maswla ya mawasiliano;
Maswali haya yanahitaji majibu:
-kwanini waziri alisimama upande wa makampuni tulipolalamika juu ya Upandaji wa gharama za mawasiliano ikiwemo internet?
-Kwanini TCRA imekaa kimya licha ya kupanda kiholela kwa gharama za vifurushi?
-Kwanini sasa hivi hatuoni makampuni ya mawasiliano yakiwavutia wateja wake kiushindani kwa kutangaza ofa mbali mbali?
-Kwanini gharama za vifurushi ziko karibia Sawa katika makampuni yote ya mawasiliano?
-je wamiliki wakubwa wa haya makampuni ni akina Nani?
-kwanini makampuni haya hayajasajikiwa DSE? Kuna nini nyuma ya pazia?
Ukipata majibu katika wizara zote hizo mbili utagundua kuwa Magufuli alikua sahihi kuwafukuza uwaziri watu hao wawili!
Adios
 
Maisha yake yote toka kuzaliwa mpaka Leo hajawahi kukutana na kitu kinaitwa shida, leo hii utegemee atajua shida za watu wa Hali ya chini na mahitaji yao? Yeye anacjojua ni kumfurahisha boss wake na harakakati zake alizozianzisha 2015. Lile jitu la kazi kalemani lenyewe halikutokea masaki na osterbay lilikuwa linapiga kazi ya kueleweka kimyakimya.
 
Back
Top Bottom