- Thread starter
- #181
Habari Jf.
Nikiwa kama mdau wa maswala ya maji, nimepata wazo na kuona jamii inapaswa kulifikilia pia kwa kuzingatia haya mabadiliko ya kimazingira na kiuchumi.
Leo tunashuhudia kuongezeka kwa bei za mafuta ya petrol na diesel, tunashuhudia kuongezeka kwa ukame kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, n.k.
Sasa nafikilia kwa wale wanaoendesha uchumi wao kwa kutumia vyanzo vya maji ni muda wa kwenda kutumia mfumo endelevu wa solar water pump. Badara ya kupata changamoto za umeme kukatika kila wakati na kwa wale wanaotumia pampu za maji zinazotumia nishati ya diesel au petroli ambazo nimekuwa na mfumuko wa bei kila wakati. Muda sasa unaongea inapaswa kuhamia kwenye nishati ya jua.
Huko vijijini wakulima wengi wanatumia pampu za diesel na wengine wanakodisha pampu hizi,kwa sasa gharama za kuendesha pumpu hizi zitaongezeka na kuathiri kilimo kwa ujumla.
Kuna kila sababu sasa kwa wakulima na watumiaji wengine wa pampu za maji kufikilia kuingia kwenye mifumo ya nishati ya jua.
Kutokana na uzoefu wangu kwenye maswala ya pampu za maji, Changamoto niliyoona kwenye solar water pump ni gharama katika kununua na kufunga, ila ni mfumo ambao ukifanikiwa kufunga umemaliza kila kitu, sasa kutokana na changamoto hizi, nazihita taasisi ambazo zinauwezo wa kukopesha hawa wakulima na watumiaji wengine wa mifumo ya maji waweze kuona fursa ya kuwawezesha kundi hili la wajasiliamali kumudu gharama za kununua na kufunga mfumo mpya wa solar water pump.
Ombi langu kama kuna member wa jamiiforum anayemiliki microfinance , aangalie namna ya kuwasaidia kundi hili, wahitaji ni wengi sana , wapo wakulima, wajasiliamali wenye viwanda vidogo vidogo,viwanda vikubwa, wafugaji, taasisi za elimu,afya, malazi, n.k.
Kwa wastani kwa sasa gharama za kununua na kufunga mfumo wa solar water pump ambao utaleta tija kwa mkulima, mfugaji, au mjasiliamali na kuanzia 3,700,000/= (milioni tatu na laki saba ya kitanzania).
Karibuni kwa maoni.
+255699 494650
Evigt Instagram
QR Code Evigt Twitter