Tunachimba visima vya maji popote Tanzania

Tunachimba visima vya maji popote Tanzania

Mkuu kwa kisima cha urefu 120m naweza pata Pump yake? Na ni bei gani?
 
Mkuu kwa kisima cha urefu 120m naweza pata Pump yake? Na ni bei gani?
Pump ipo full set kwa mita 120 unapata kwa 6.5 M
Kama utahitaji pump tupu ni 2.5M
Hii pump ina watts 550
 
Control pump unayo? Nina pump ya kw 7.5, so nahitaji control pump ili iwe inajiwasha na kujizima(automatically)

Bei?
 
Naomba uwakala Mkuu, nipo lake zone.. Kama upo tayari njoo PM unipatie contacts tuangalie namna ya kupanua soko wote tupate..
 
Kuna vifaa ambavyo vinategemeana katika kufanikisha maji yanatoka kwenye chanzo cha maji. Bila vifaa hivi bado lengo la kupata maji kwa matumizi yako halijatimia.

Karibu ujipatie bomba, kamba, waya, mifuniko,control box, pump,n.k
Sms/call/WhatsApp 0699494650
Kariakoo, DSM
Delivery service available
images (9).jpeg
PVC-Corrugated-Conduit.jpg
images (8).jpeg
images (12)~2.jpeg
images (10).jpeg
images (11)_1649298870174.jpeg
IMG_20220216_182053_3.jpg
 
Habari wadau

Huduma ya utafiti na upimaji upatikanaji wa maji unaendelea sasa Tupo mkoani Tanga, kama upo mkoa wa Tanga au jirani na mkoa huu na unahitaji huduma hii basi sasa ndio wakati muafaka wa kuwasiliana nasi sasa. Kumbuka kuchimba kisima bila kufanya vipimo ni sawa na anayecheza bahati nasibu.

0699494650
Tanga
 
Maeneo ya wilaya ya Mkinga mpaka kuelekea Boda ya Horohoro maji ya visima yanachumvi kali sana

Je, mnaweza kuwa na solution ya tatizo ilo la maji kuwa na chumvi sana, maana kampuni nyingi zimeshindwa kutatua tatizo ilo
 
Maeneo ya wilaya ya Mkinga mpaka kuelekea Boda ya Horohoro maji ya visima yanachumvi kali sana

Je, mnaweza kuwa na solution ya tatizo ilo la maji kuwa na chumvi sana, maana kampuni nyingi zimeshindwa kutatua tatizo ilo
Zipo desalination machine tunaweza kufunga, wengi wanashindwa tu kumudu gharama ya kununua hizi machine ila zipo na mchakato wa kununua lazima kwanza maji yako yachukuliwe sample na kupelekwa maabara kisha kiwango cha chumvi au madini mengine yasioitajika kwenye maji ikishajulikana ndipo inajulikana aina ipi ya mashine itakusaidia na gharama ndo utazijua hapo lakini kwa uzoefu wangu sijaona mashine chini ya milion saba.
 
Habari Jf members.

Kichwa cha habari ni swali mahususi kwa kuanzia ili kupata baadhi ya maarifa kuhusu uchimbaji wa visima kulingana na uzoefu wangu wa zaidi ya miaka 5 katika biashara hii.

Kwa wadau wa uchimbaji wa visima ni kawaida kukutana na swali la namna ya kutambua gharama za uchimbaji wa kisima, kwa ujumla ni vigumu kuwa na jibu la moja kwa moja kwa swali kama hilo, kwa sababu ya namna ya tofauti kubwa za miundo ya miamba katika maeneo mbalimbali ndani ya Tanzania au njee ya Tanzania.

Tofauti zingine zinazo pelekea gharama za uchimbaji wa kisima kutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine ni: miundo mbinu ya eneo husika, umbali, upatikanaji wa materials, aina ya kisima, urefu wa kisima, n.k.

Aina ya visima na uchimbaji wake.

Visima vya mkono/mviringo


Visima vya mkono, ndio visima vilivyozoeleka kuchimba kwa kutumia vifaa kama majembe, n.k.
Visima hivi vinaweza kuwa na urefu wa futi 50 hadi 60,na hutoa maji ikiwa ardhi ina asili ya umaji maji au kipindi cha mvua, na mara nyingi hukauka au kupungua sana kipindi cha kiangazi.
Maji utolewa kisimani kwa kutumia kata au unaweza kufunga pump ya maji inayotumia nishati.
Visima hivi ni hatari kwa mchimbaji asiye na uzoefu anaweza kupoteza maisha kwa kuteleza, joto , kukosa hewa akiwa chini ya ardhi au kumong'onyoka (collapsed).
Aina hii ya kisima ni gharama nafuu zaidi kuchimba, changamoto yake ni kuwa, maji ni rahisi kuchafuka na kukauka.
#kisimachamkono
summer-2019-blog-4-pic-3.jpg
hand_dug.jpg
hunddug.jpeg


Visima vifupi vya mashine

Zipo mashine ndogo ambazo zinachimba visima vifupi ambavyo vinawekwa plastic za upvc ili kuzuia kumong’onyoka(well collapse).
Visima hivi mara zote vinakuwa na urefu wa futi 150 hadi 200, na vinatumia pampu ya mkona kutoa maji chini ya ardhi.changamoto ya visima hivi pia ni ukaukaji au kupungua kwa maji kipindi cha kiangazi.
Gharama za uchimbaji ni nafuu ila inategemea na mji au mkoa , kwa maana kwa baadhi ya mikoa na miji hapa Tanzania, tayari zipo taasisi zilizojikita kuwasaidia kuwachimbia visima hivi wanannchi wa mkoa husika. Mfano mkoa wa morogoro lipo shirika lijulikanalo MSABI, na nyanda za juu kusini lipo shilika la SHIPO.
#handpump
msabi1.jpg
well_pump_install_2.jpg


Visima virefu vya mashine

Hivi visima huchimbwa na machine au mitambo mikubwa na wakati mwingine huenda hadi futi 900 chini ya ardhi.Ili kufanikisha kutoa maji katika kina kirefu lazima pampu inayotumia mota ifungwe, hii inaweza kuendeshawa kwa umeme wa maji/jua/generator.

Pia lazima kuweka miundo mbinu ya kuhifadhi maji, mipira ya kusambaza maji, n.k. Mambo yote haya yanachangia gharama za uchimbaji wa visima virefu kuwa kubwa huku vikiwa ndio visima vyenye tija zaidi duniani kwa kuwa na uwezo wa kutoa maji mengi zaidi kwa muda mfupi na kwa nyakati zote za majira ya mwaka.

Kwa leo ni hayo tu niliyonayo, mwenye nyongeza ruksa kutililika.
keep in-touch
0699494650
twitter
Instagram
 
Kwa hio hivyo visima virefu vina range kwenye sh. Ngapi, gharama yake
Inategema na mkoa unaotaka kisima kichimbwa, ila kwa takwimu za DSM, bei inarange 50k to 75k inategemea na kampuni na urefu wa kisima.
Kwa Pwani inarange 80k - 100k, onategemea na kampuni na urefu wa kisima pia. Kwa mikoani ya bara mara nyingi 120k - 200k inategemea na umbali, kampuni husika na urefu wa kisima.
Hizo bei ni kwa mita moja,
 
Kwa hio hivyo visima virefu vina range kwenye sh. Ngapi, gharama yake
Wachimbaji wajanja Sana. Gharama kubwa iko kwenye hayo mabomba, yatakuleta maji kutokea ardhini!
Mara nyingi hawakuambii direct. Utasikia in the middle of the project maji tuliyokosa Mita 100, tukaenda Mita 150 chini ndiyo tukapata kwamba WA maji Safi, sasa kunaongezeko la gharama kidogo!
Hapo ushapigwa na kitu Cheney ubapa!
 
Wachimbaji wajanja Sana. Gharama kubwa iko kwenye hayo mabomba, yatakuleta maji kutokea ardhini!
Mara nyingi hawakuambii direct. Utasikia in the middle of the project maji tuliyokosa Mita 100, tukaenda Mita 150 chini ndiyo tukapata kwamba WA maji Safi, sasa kunaongezeko la gharama kidogo!
Hapo ushapigwa na kitu Cheney ubapa!
Sasa ili kukabiliana na hili, inatakiwa kufanya vipimo kabda ujachimba ( topographical survey) hii itakusaidia kuwabana.
 
Back
Top Bottom