Habari Jf members.
Kichwa cha habari ni swali mahususi kwa kuanzia ili kupata baadhi ya maarifa kuhusu uchimbaji wa visima kulingana na uzoefu wangu wa zaidi ya miaka 5 katika biashara hii.
Kwa wadau wa uchimbaji wa visima ni kawaida kukutana na swali la namna ya kutambua gharama za uchimbaji wa kisima, kwa ujumla ni vigumu kuwa na jibu la moja kwa moja kwa swali kama hilo, kwa sababu ya namna ya tofauti kubwa za miundo ya miamba katika maeneo mbalimbali ndani ya Tanzania au njee ya Tanzania.
Tofauti zingine zinazo pelekea gharama za uchimbaji wa kisima kutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine ni: miundo mbinu ya eneo husika, umbali, upatikanaji wa materials, aina ya kisima, urefu wa kisima, n.k.
Aina ya visima na uchimbaji wake.
Visima vya mkono/mviringo
Visima vya mkono, ndio visima vilivyozoeleka kuchimba kwa kutumia vifaa kama majembe, n.k.
Visima hivi vinaweza kuwa na urefu wa futi 50 hadi 60,na hutoa maji ikiwa ardhi ina asili ya umaji maji au kipindi cha mvua, na mara nyingi hukauka au kupungua sana kipindi cha kiangazi.
Maji utolewa kisimani kwa kutumia kata au unaweza kufunga pump ya maji inayotumia nishati.
Visima hivi ni hatari kwa mchimbaji asiye na uzoefu anaweza kupoteza maisha kwa kuteleza, joto , kukosa hewa akiwa chini ya ardhi au kumong'onyoka (collapsed).
Aina hii ya kisima ni gharama nafuu zaidi kuchimba, changamoto yake ni kuwa, maji ni rahisi kuchafuka na kukauka.
#kisimachamkono
Visima vifupi vya mashine
Zipo mashine ndogo ambazo zinachimba visima vifupi ambavyo vinawekwa plastic za upvc ili kuzuia kumong’onyoka(well collapse).
Visima hivi mara zote vinakuwa na urefu wa futi 150 hadi 200, na vinatumia pampu ya mkona kutoa maji chini ya ardhi.changamoto ya visima hivi pia ni ukaukaji au kupungua kwa maji kipindi cha kiangazi.
Gharama za uchimbaji ni nafuu ila inategemea na mji au mkoa , kwa maana kwa baadhi ya mikoa na miji hapa Tanzania, tayari zipo taasisi zilizojikita kuwasaidia kuwachimbia visima hivi wanannchi wa mkoa husika. Mfano mkoa wa morogoro lipo shirika lijulikanalo MSABI, na nyanda za juu kusini lipo shilika la SHIPO.
#handpump
Visima virefu vya mashine
Hivi visima huchimbwa na machine au mitambo mikubwa na wakati mwingine huenda hadi futi 900 chini ya ardhi.Ili kufanikisha kutoa maji katika kina kirefu lazima pampu inayotumia mota ifungwe, hii inaweza kuendeshawa kwa umeme wa maji/jua/generator.
Pia lazima kuweka miundo mbinu ya kuhifadhi maji, mipira ya kusambaza maji, n.k. Mambo yote haya yanachangia gharama za uchimbaji wa visima virefu kuwa kubwa huku vikiwa ndio visima vyenye tija zaidi duniani kwa kuwa na uwezo wa kutoa maji mengi zaidi kwa muda mfupi na kwa nyakati zote za majira ya mwaka.
Kwa leo ni hayo tu niliyonayo, mwenye nyongeza ruksa kutililika.
keep in-touch
0699494650
twitter
Instagram