Tunafanya kazi saa moja hadi saa saa 12, Kuna watu wanataka wagome

Kazi Si masaa8 hapo wanawanyonya mnatakiwa mlipwe overtime
 
Ndo maana Tanzania inakuwa masikini
 
Hamkusaini mikataba? Au mlikua na wenge la kupata kazi hamkusoma terms mkakimbilia kutia Saini tu?
Mkataba tumesaini na Mimi binafsi Sina shida, maana mkataba niliuelewa


Mkataba unasema kwamba " Mwajiriwa atafanya kazi ndani ya muda ataopangiwa na mwajiri"


Pia unasema kwamba, " unatambua haki zote za watumishi za JMT"


Hizo hoja mbili ndio tatanishi katika mkataba huo huo
 
Ndo maana Tanzania inakuwa masikini
Solution ndio muhimu kuliko lawama, kama unajua elimisha watu

Kuna watu watanufaika kupitia mchango wako unless mchango wako ni valueless
 
Kazi ni masaa nane au masaa yasiyozidi 12 kwa siku na masaa hayo yafanye jumla ya masaa yasizidi 45 kwa wiki.
 
Hope wataalam watafafanua zaidi
 
Pole mkuu wajuaji wengi sana wakati hawajui kitu ndo maana wataalmu wanaamua kukaa kando kwa kuogopa kutupiwa maneno ya kashfa
Ok, JF ni shida sana, watu baada ya kuja na solution. Unakuta wanakuja na lawama na kukosoa.

Baada ya kuelimisha wao wanajua kukosoa bila kutoa elimu.
 
Kazi Si masaa8 hapo wanawanyonya mnatakiwa mlipwe overtime
Weka vizuri wananyonywaje.. na wananyonywa na nini weka wazi.. neno kunyonywa si dogo mkuu..
 
Shida ya Tanzania mfanyakazi anamuhitaji sana mwajiri kuliko mwajiri anavyomuhitaji mfanyakazi. Kama unafanya kazi masaa zaidi ya nane na unaitegemea hiyo kazi jikaze tu otherwise utapata haki yako ila mahusiano na boss yatakuwa hafifu na pengine atakubadilisha
 
Ujinga wa kuajiriwa niliachaga siku nyingi baada ya kugundua unakuwa mtumwa kiakili, kifedha na kimwili yaani aliyekuajiri ndio anakupangia muda ,fedha akili yako anaicontrol na mwili wako anaushughulisha atakavyo na muda mwingi unautumia kukutumikisha. Kijana sanuka acheni kulialia
 
Kazi ni masaa nane au masaa yasiyozidi 12 kwa siku na masaa hayo yafanye jumla ya masaa yasizidi 45 kwa wiki.
inategemea na aina ya kazi, kuna kazi zingine wanafanya kazi masaa 12, ndani ya masaa 12 masaa manne wanalipwa overtime.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…