Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Missile of the Nation njoo ujibu huku
 
Wahuni wa jiwe wameshampora Urais Mama ili kuendeleza maovu yao na kuyaficha ya awali.
 
Mimi ni mkristu lkn naamini ktk UWIANO ktk nafasi za uteuzi, ni jambo Muhimu sana ktk kujenga Utengamano na Umoja wa taifa letu.
Jambo hili limekuwa likipigiwa kelele mara kwa mara ni muhimu sana likafanyiwa kazi kwa nia njema ya kujenga badala ya kupuuzwa.


Baada ya kuzingatia vigezo vyote vya msingi basi ni muhimu pia kuzingatia UWIANO.
ni htari sana kuendelea kujaza aina moja ya watu ktk nafasi za kuteuliwa halfu wengine wakiwa wachache na sifa za msingi wanazo.
 
Hii hoja ingekuwa na mashiko kama ingetaja waislamu ambao walistahili kushika nyadhfa hizi lakini wakanyimwa na kupewa mmisheni asiyekidhi viwango vinavyotakiwa.

Amandla...
 
Binafsi ningependa suala la udini katika uteuzi liwe na ratio nzur ila unakuta ukichakata wasomi huwakuti waislam kihivo.
Wengi wanaosoma wanajikita kwenye elimu ya dini (theology) badala ya kijikita kwenye elimu dunia (universal education).
So inakuwa vigumu kufanya vetting upande wa wakristo.
Nilipokuwa chuo 98% ya ma-lecturers walikuwa wakrsto sijui waislam wanaendaga wapi?
 
Rais = Muslim
Waziri Mkuu = Muslim
Rais wa Zanzibar na makamu wke = Muslims
Jaji mkuu= Muslim
Katibu mkuu Kiongozi= Muslim

Mtoa mada akili hazikutoshi na inaonyesha una makengeza . Hiyo safu hapo juu ya wafanya maamuzi wakuu wa nchi hii haitoshi kuwawakilisheni? .
Ni kipya unataka kwamba tuingie kuzungumzia uwiano sawa wa kidini hata kama hawana competency zinazotakiwa?. Wakati JK aliwajaza kwenye nafasi za wakuu what difference did you make ? JPM amewajengea hadi misikiti lakini huna shukrani unamwita mdini. Wewew una matatizo.
 
Hajui mipaka ya kimamlaka.

Akiwa anaongea anaongea utadhani yeye ndiye Rais wa nchi hii.
Lakini mtu anaweza kusema kuwa unaona hafai kwa sababu sio muislamu. Angekuwa muislamu ungesema kuwa ni waizi kuwa anaongea kwa niaba ya Rais.

Amandla...
 
Serikali ni dubwana kubwa sana, hao uliowataja ni watumishi wachache tu miongoni wa watumishi wengi wa serikali kwa ujumla wake.

Serikali ina maDAS, naRAS, Wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, makatibu wakuu, nabalozi, mawaziri, wenyeviti wa bodi etc—Sasa huko kooote kukiwa na waislamu wachache, then kwenye hizo nafasi za juu hata wakikaa waislamu watupu bado haiamaanishi waislamu wa kutosha wamo serikalini.

Yaani ni heri hata nafasi za juu zikaliwa na watu wasio waislamu lakini wawe fair kwa waislamu kwenye mgawanyo wa keki ya taifa ikiwemo utumishi ndani ya serikali!
 
Kule Zanzibar vipi teuzi zake zina usawa?
 
Unasemaje kuhusu teuzi za serikali ya mapinduzi?
 
Unasemaje kuhusu teuzi za serikali ya mapinduzi?
Sijawahi kushiriki uchaguzi wowote wa zanzibar, sina hata haki ya kupiga kura huko. Sasa kusemea namna wanavyounda serikali yao nawaachia Wazanzibari wenyewe walalamike au washangilie.

Mimi niko Interested na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hii mimi ndo huwa napiga kura na kulipa kodi, Kiufupi serikali ya JMT ndo nina "mtaji" wangu ndani yake, hiyo serikali nyingine nawaachia wenye serikali yao wao wenyewe.
 
Watanzania wanataka maendeleo,na ww unawaza udini,ukabila,na ukanda na ndio zimekuwa akili kama ulivyo sema,yaani unataka viongozi wakalie ujinga wa kukaa mezani na kusema tuahitaji wakristo kumi na waislamu kumi na kwa mawazo yako suala la utaalamu kwako halina nafasi isipokuwa udini,ukabila na ukanda.Rudi kwenye mawazo yako uone kama uko sahihi yawezekana kuna sehemu utagundua unatereza kila wakati,jaribu vilevile kuo na athari za hayo unayoyataka yatokee kama yana umuhimu kwa nchi au hayana,mwishoni utaelewa vzr na vilevile unaonekana kutaka kusikilizwa haya mawazo yako lkn ww hauko tayari kusikiliza wenzako pia ili na ww ujifunze kitu zaidi na zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…