Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Si vizuri ubaguzi kuupoza kwa lugha za kidiplomasia au kuufumbia macho kwa jicho la mshikamano.

Dawa ya ubaguzi ni kuuondoa, ili tuwe na taifa lenye fairness na haki kwa wote.

Ngoja nikuulize swali, leo hii rais akateua Wazanzibar watupu kwenye ukatibu mkuu, utaona tatizo au utaona ni sawa tu!?
Ikiwa watakidhi vigezo mimi binafsi sioni shida kwani tunataka watu wa kuwatumikia watanzania na si vinginevyo. Mbona wakati wa uchaguzi maaskari na wanajeshi kutoka bara wanakwenda Zenj kuimarisha usalama?
 
[emoji1542]Kama umewahi kusoma, kuanzia elimu ya msingi, sekondari mpaka elimu ya juu (zingatia madarasa yako husika katika hizo hatua zote), utagundua kuwa hata kwenye madarasa yako uliyowahi kusoma wakristo ni wengi.

[emoji1542]Angalia matokeo ya kidato cha nne na sita, angalia wanafunzi 10 bora kitaifa,angalia waalimu wengi mashuleni,utagundua kuwa wakristo ni wengi.

[emoji1542]Angalia mikoa inayoongoza kwakuwa na wasomi wengi (Kilimanjaro, Bukoba) kote huko wakristo wametawala.

[emoji1542]Angalia idadi ya shule za kidini Tz, utagundua kuwa ni za kikirsto.

NB:Kwa hapa Tz, wasomi wengi ni wakristo, hilo ni hakika. Hata hivyo katika swala la uteuzi,ni vyema tukazingatia weledi na uchapakazi kuliko udini.Kwangu mimi mkristo au mwislam wote ni sawa tu.
Muulize Jasusi Evarist Chahali kuhusu idadi ya waislamu na Wakiristu nchini na ishu ya imbalance katika teuzi hizi zinazoinvolve watu wa dini hizi—Alikuwa, anafanyia PhD suala hili.

By the way, huwezi kujua idadi ya Waislamu na Wakiristo nchini bila sensa

Sensa ninayoifahamu mimi iliyokuwa na kipengele cha dini za watu ni sensa ya mwaka 1954 iliyoonyesha Waislamu ni wengi zaidi.

Kwa sasa ni vigumu kujua idadi ya waislamu na wakiristo nchini mpaka labda ingekuwepo sensa inayoangalia kipengele hicho!
 
Mama alishasema sifa za mtu hasa utendaji( mzuri / mbaya) ndo inampa nafasi zaidi ya kuwa sehemu fulani
 
Nami leo nitie neno hapa,,,,katiba yetu haizungumzii mambo ya dini. Eti katika nafasi flani au uongozi swala la dini lizingatiwe wala ukanda wala ukabila. Haya mambo jamii yetu ikianza kuyazingatia tunapokwenda tunaenda kuligawa taifa. Mtu anayeona teuzi au ungozi wa nchi akaanza kugikiria maswala haya ya dini, ukabila, ukanda huyu ni hatari kuliko hata neno lenyewe. Mteuliwa au kiongozi akianza kufikiria haya mambo katika utendaji wake ni hatari zaidi. Viongozi wajikite kuwahudumia wananchi kwa usawa bila kujali dini, kabila, ukanda au jinsia. Juzi aliteuliwa kiongozi flani watu wa eneo lile alikotoka na watu wakabila lake wakaanza kufurahia kwamba na sisi tumekumbukwa, nilishangaa sana. Inamaana kwa kipindi ambapo hapakuwa na kiongozi mkubwa kuyoka kwenye mlinyanyaswa? Tuache fikra hizi zitatugawa kama Taifa. Tuangalie umoja wetu usivurugwe na fikra kama hizi

Rais muislam
Waziri mkuu Muislam
Katibu mkuu kiongoz Muislam
Jaji mkuu Muislam
Bado unalalamika.... Ulitaka viongoz wote wawe waiaslam!?.. Mlitaka mpewe nini ili nyie binadam mlizike!? Mbona Hamna confidence hivyo... Haya kwa mfano serikali ya mapinduz Zanzibar INA wakristo wangap kwenye idara zake na nini cha ajabu kinatokea kwa kuwa na waislam wengi ktk serikali ya zanzibar.. Embu mlete vitu vya msingi basi tujadili basi na sio ujinga kama huu... Basi tufanye ateue waislam wote wewe utafaika nini kwa mfano...

Mkuu ww udini unakusumbua hilo kwanza ukili tu.....Hii nchi hakuna mtu anachaguliwa kwa udini wake bali kwa uwezo wake.Sikatai wakristo wanakua wengi husikii watu wanalalamika kua waziri mkuu na Rais na katibu mkuu ni waislam na hivo ni vyeo vikubwa sana mbona wakristo hawalalamiki au kuna mkristo kalalamika kua kwa nn Rais katoka zanzibar na ni muislam.Mimi ndo hua nasema uislam hua unaharibiwa na watu km nyinyi maana ww ubinafsi unakusumbua sana na udini.

Haya maswala ya udini sijui kila teuzi tuangalie waislam wangapi na wakristo wangapi huu ni upumbavu na ujinga wa hali ya juu. Hawa watu wanao kua wanaleta huu ujinga ni wa kupuuza kunawatu wengi sana hawana dini nao walalamike na kuna siku hata hao waislam watasema mbona washia ndo wengi wanachagulia kuliko sunni na kuna siku wakristo watasema mbona wakatoliki wanachaguliwa kuliko walokole na hapo ndo tutakua tumefika pabaya.Huu upuuzi ni wa kukemea mapema .Mm naona ni upumbavu na ujinga kuaangali kila teuzi kidini hii Tanazanian ni ya kwetu sisi watanzania sio ya wakristo ama waislam na babu zetu walikua wapagani tu huu udini hautatusaidia.

Mkuu#@Missile of the Nation...kabla atujaendelea jibu hoja hizi zilizoibuliwa na wadau kutokana na uzi wako.mim ntataja 1 tuuuu...
a)kigezo cha uwiano wa kidini zanzibar haupo,je hili unalizungumziaje? Je unakubali dini zingine zianze kudai uwiano?na kama ndivyo matokeo yake unadhani yatakuwa na faida kuliko hasara KWA ustawi wa nchi yetu?....mkuu na hapa kwenye faida na hasara ya unachosisitiza..... mifano hai tunayo so ni vizuri ulete facts(nakukumbusha tuuu).....

mkuu kumbuka udini,ukabila,ukanda ni watoto wa baba na mama mmoja CHUKI NA MATENGANO

Jibu la swali lako:tukisema tuesabu watu KWA njia ya udini ni mwanzo wa machafuko KWA sababu
itajenga chuki:dini moja inaweza kukuta inawawakilishi wengi au wachache katika nafasi mbalimbali za nchi nakujiona inatengwa,inabaguliwa au kunyanyaswa kitu ambacho KWA hali ya tanzania si kweli.... na dini ambayo itakuwa na wawakilishi wengi inaweza kudharau dini nyingine na kuibua haki ya kuwa na dini moja....minorities au majorites(dini) wenyewe nao wanaweza kutaka kujitenga(mkuu mifano tunayo kwani hakuna jipya chini ya jua)

Ndio maana nyerere alikemea sana ukabila udini ukanda unzanzibari na utanganyika KWA kuwa alijua kuwa huo ni mwanzo wa taifa kuanguka na kama si hivyo ndo itakuwa ni fursa nzuri wa maadui wa nje na ndani kuibia na kunyonya utajiri wa nchi usika na kuwaacha wazawa kwenye mapambio ya unzanzibari utanganyika udini ukabila

Dunia kuwa moja imeshindikana,imebaki utaifa..tukitoka kwenye utaifa na kuingia udini na ukabila...dunia hapatakalika...

Mkuu hoja yako si mbaya sanaa...najua ni KWA nia nzuri tu ILA angalia negative impacts zilivyokubwa...ndo maana wadau humu wanakupinga KWA kuwa mwisho wa siku tutaingia kama mkuu ngosha wa mwanza alivyosema kwenye komenti yake ya pili...

NB:JIBU HOJA YA HAPO JUUU ILI TUNAPOKUJIBU TUJUE UELEWA WAKO UPO LEVEL GANI MKUU WANGU
 
Ukiondoa waislamu na wakiristo, hao wa dini nyingine ni wachache sana nchini, by the way hata nao wakiwa included serikalini haina shida tena ni jambo zuri tu.

Hata hivyo hoja yako haiwezi kuwa kigezo cha kufanya teuzi ambazo kiajabu sana zinalalia mno upande mmoja mpaka inaraise alarm
Mkuu tuwainclude kivipi?unamaanisha tuwachukuwe wote ama?
Maana nachokijua ni kuwa ndani ya serikali hawapo wakristo na waislamu tu... Baliinclusion imejumuisha dini zote dini nyingine
Labda mwenzetu unanjia ya kuinclude tofauti na hii..ebu tujulishe
 
Mkuu usituletee udini hapa ,tunacho taka ni kwamba mtu ateuliwe bila kujali ,dini,ukabila jinsia ,chamsingi awe ana uwezo na nafasi husika, mbona nafasi kubwa za juu kitaifa zipo KWA ndugu zetu na wakiristu hawajapiga kelele,huko Zanzibar vipi mbona wakiristu hawalalamiki ali Hali Hili ni taifa moja , tutolee udini hapa
Yap....Naunga mkono hoja
 
Wapumbavu nyie kwani dini ni 2 tu ukristo na uislam.

Mbona Kuna wapagani hawalalamiki?

Mbona kuna watanzania Budha hawalalamiki?

Mbona Kuna watanzania wanaabudu mizimu kama yeriko Nyerere hawalalamiki kutokuteuliwa ?

Hivi kwanini Nyie wakristo na waislam huwa mnajiona so special kwa kila kitu?

Iweje dini zingine hazilalamiki kutokuteuliwa ila Nyie kila siku vilio ?

Watu wangapi nchi hii hawana dini na Wana sifa za kuteuliwa lakini hawana makelele Kama Nyie wanafiki. Mnaenda misikitini na makanisani ila mkiambiwa msaidie wasio na ajira mnaanza kelele.

Acheni unafiki msijifiche kwenye kimvuli Cha dini.
Mimi kwangu awe Muislamu,Mkristo, Hindu e.t.c ninachopenda kuona ni
1.Katiba kuheshimiwa
2.HAKI isiwe jambo la hisani ya Kiongozi
3. Taasisi imara zisizoingiliwa na mhimili wowote kimaamuzi.

Kubwa zaidi watu waishe kwa furaha.
Kweli mkuu mambo ya udini hayatuhusu
 
K
MADA HII IMEJIKITA KATIKA TEUZI ZA MAKATIBU WAKUU ULIOFANYIKA TAREHE 4/4/2021

Mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye anaishi katika nchi inayoongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninayo haki ya kutoa maoni juu ya mustakbali wa nchi hii.

Katiba yetu inatambua kuwa, palipo na binadamu hapawezi kukosekana mapungufu ya kibinadamu ikiwemo ubaguzi, uonevu upendeleo n. k, ndiyo maana Katiba ikapiga marufuku vitu hivyo.

Sasa kwa muda mrefu, nimekuwa hapa JF nakemea teuzi ambazo haziakisi demografia ya nchi yetu, nilikemea teuzi zilizokaa kidini, kijinsia na kikanda. Kuna watu humu JF wako comfortable kukemea teuzi zilizokaa kikanda, au kikabila lakini wanafumba macho teuzi zilizokaa kidini, na wanakuwa wakali kwelikweli pindi ukilisemea. Kuna wengine wanakua comfortable kukemea teuzi zilizojaa ujinsia lakini wanaogopa kukemea teuzi zinazonuka udini. Na Tupo wengine tuko tayari kukemea kila viashiria vya teuzi zenye sura ya udini, Ukanda, Ujinsia, Ukabila n. k

Sasa kuna Pattern ninayoiona katika Teuzi hizi kuanzia serikali ya Magufuli na ninaona zimeanza kujitokeza katika utawala wa Samia

Kwanini overall teuzi nyingi zinakuwa na Ratio zaidi ya (75-80%) Wakiristo na only( 20%-25%) Waislamu, Hii ratio inakuwaje fixed, Hii imetokea tu kwa nasibu au imewekwa by design?

Kwanini pattern hii inajirudiarudia kila mara, pindi uteuzi unaoinvolve watu wengi unapofanyika?

Mimi kama Mwananchi, mpenda mshikamano wa Kitaifa, ninaona kuna harufu ya ubaguzi wa makusudi katika kugawa keki hii ya Taifa, na kwangu mimi binafsi naamini na naamini pia maelfu ya Watanzania wenzangu wengi wapenda haki bila kujali dini zao hawalipendi hili, kwa hiyo ninasema wazi kuwa hili halikubaliki hata kidogo.

Nimeangalia leo teuzi za makatibu wakuu, naona kuna ratio kama ya waislamu Watatu au Wanne katika timu nzima ya makatibu wakuu Ishirini walioteuliwa hii ikiwa ni ratio ile ile ya 20% Waislamu na 80% Christians. Ningependa kujua, hii ni by design au kuna mchezo mchafu?

Kuna watu wanajenga hoja kuwa, hii ishu haina maana bali uchapakazi wa mtu —Hii hoja yangu bado ni muhimu kwa sababu zifuatazo

1. Hizi teuzi ni chanzo cha kipato, ni keki ya Taifa, Unapokuwa na watu janii moja wanaenjoy keki hii kuliko wengine maana yake unawaandalia hata vizazi vyao elimu bora zaidi, huduma bora zaidi za afya, nyumba bora zaidi kwa hiyo maana yake vizazi vya hawa wanaoenjoy sehemu kubwa ya keki ya Taifa leo, wana nafasi ya vizazi vyao kuendelea kuwa tabaka la juu katika nchi wakati hawa wengine wakiendelea kuwa kama raia wa daraja la pili!. Hili hakikubaliki.

2. Lakini teuzi za hivi zinazolalia upande mmoja ni hatari kwa umoja, amani na mshikamano wa Kitaifa—Haiwezekani teuzi za hivi zilalie upande mmoja halafu udhani kuwa wale wengine ambao wako marginalized wafurahi, hilo haliwezi kutokea

Kwa hiyo natoa wito sasa Kwa mamlaka za juu za serikali.

1. Lazima uchunguzi ufanyike kwa timu nzima inayohusika na kupeleka majina ya teuzi mbalimbali kwa Rais, Je hakuna udini katika kuchuja kwao majina?, na kama hakuna udini kwa nini hii pattern ya 20% by 80% inajirudiarudia, Kwa nini kwa mfano hatujawahi kuona teuzi zenye wauslamu 80% na Wakiristo 20%?

2. Tunataka kujua, je ni kweli hakuna waislamu wa kutosha kushika nafasi za juu kwa ratio nzuri? —Kama hawapo kwa nini? Na kama wapo kwa nini ratio inaendelea kuwa katika mtindo huo wa ALWAYS WAISLAMU NAMBA ZAO ZIWE Chini?

Suala la pili ni suala la Jinsia
Nimeona pia idadi ya wanawake walioteuliwa katika nafasi za makatibu wakuu ni almost negligible. Je, kwa utaratibu tuliokuwa tumeanza kukubaliana wa kufanya women empowerment, teuzi za namna hii zinasaidiaje katika ajenda hii?

Mada hii nataka iwafikie wafuatao

1. Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3. Mkurugenzi Mkuu wa TISS
Kiongozi kuna mambo bado hujayachambua kwa kina... MIMI SIO MDINI ila naandika kile kilichopo katika jamii yetu kwa sasa...
1. Wanafunzi wengi waliopo shule za kata niwa dini ya Kiislamu.... kwa shule za binafsi asilimia kubwa ni wakristo... ( tafakari hapo kiongozi)
2. Idadi kubwa ya vijana wakike na kiume waliopo mtaani niwadini ya kiislamu... matokeo yake Vijana wa kike wanazalishwa wengi wao wakiwa shuleni au mtaani ili hali hawana mafanikio yoyote ya kiuchumi kuweza kujikwamua au kuwapeleka shule nzuri watoto... wanaishia shule za kata....
3. Hata huku kwenye roots ya elimu kuanzia elimu msingi na vyuo, walimu wengi staff niwa kristo.
4. Kibaya zaidi hata hao wachache iwe ni walimu, madaktari etc huwa hawana misimamo mikali ya imani iwe kuangalia eti huyu mkristo au muislam ( big up Mama Samia chagua kwa kuangalia utendaji wa mtu)
5. Mfano Mazingira ninayoishi, majirani zangu kila siku visomo na mambo mengine ya ushirikina... kiongozi haya yana athiri sana... elimu ya vijana mashuleni.
6. Fuatilia mashuleni haswa msingi na sekondari kila siku watoto wanadondoka mashetani 100% niwa wanafunzi wa kike wa dini ya Kiislamu... hii ina athiri sana elimu ya watoto....
Kwa ufupi kiongozi elimu ndio kila kitu... pamoja na utendaji wa mtu. Naamini watu hao wapo kwa dini zote mbili... ila ukweli ni kuwa wakristo mpaka sasa wanaongoza kwa wasomi....
Note: Shule nyingi za wakoloni ( zilikuwa zipo kikristo zaidi) viongozi wako mfano Mzee Makamba alisoma shule za mission.... lakini mzee makamba sio mdini... Kiongozi Achana na Mawazo ya Udini angalia utendaji wa mtu anafaa mpe kazi hafai achana naye. ACHA UDINI.
 
If moderators hamuwezi kumfungia huyu punguani na mada zake za uchochezi?
Kila akijamba ni udini,
Fungieni huyu mpuuzi anayeangalia jina la mtu kujua dini ya mtu.
Hajui kuna jamaa yangu Hamisi Khalfani ni mgalatia na kuna Jesse Joseph ni mjahidina.
Ndugu acha upuuzi.
Najua unatumwa na wenzako wa ndani ya sistim
 
Unajua ni vigezo gani watu wa vetting wanaangalia?

Au unalalamika tu?

Oh rais aangalie demography,sijui aangalie nini.

Hizo mamlaka ziko kisheria. lazima vetting ilalie qualifications only. na ndicho wanachofanya.

No qualifications no rights. simple as thats. dini tupa kule
Unarudi pale pale kwanini qualifications ratio yake ni biased? Je! Kuwepo na empowerment ya upendeleo ili pawepo na balance.
 
Si vizuri ubaguzi kuupoza kwa lugha za kidiplomasia au kuufumbia macho kwa jicho la mshikamano.

Dawa ya ubaguzi ni kuuondoa, ili tuwe na taifa lenye fairness na haki kwa wote.

Ngoja nikuulize swali, leo hii rais akateua Wazanzibar watupu kwenye ukatibu mkuu, utaona tatizo au utaona ni sawa tu!?
Ubaguzi ni hali/kitendo cha kumnyima/kutompa mtu kitu/haki yake au huduma anayostaili kutokan na hali yake yaweza kuwa ya kisiasa(minajili ya kichama,kiideology),kijamii(ukabila udini ukanda ) au kiuchumi(masikini tajiri)....Ndo maana hilo swala halipo na halijawahi kutokea kuchangu wote wa dini moja...so mfano wako ni mfu na si hai....hauakisi ualisia wa mambo
 
K

Kiongozi kuna mambo bado hujayachambua kwa kina... MIMI SIO MDINI ila naandika kile kilichopo katika jamii yetu kwa sasa...
1. Wanafunzi wengi waliopo shule za kata niwa dini ya Kiislamu.... kwa shule za binafsi asilimia kubwa ni wakristo... ( tafakari hapo kiongozi)
2. Idadi kubwa ya vijana wakike na kiume waliopo mtaani niwadini ya kiislamu... matokeo yake Vijana wa kike wanazalishwa wengi wao wakiwa shuleni au mtaani ili hali hawana mafanikio yoyote ya kiuchumi kuweza kujikwamua au kuwapeleka shule nzuri watoto... wanaishia shule za kata....
3. Hata huku kwenye roots ya elimu kuanzia elimu msingi na vyuo, walimu wengi staff niwa kristo.
4. Kibaya zaidi hata hao wachache iwe ni walimu, madaktari etc huwa hawana misimamo mikali ya imani iwe kuangalia eti huyu mkristo au muislam ( big up Mama Samia chagua kwa kuangalia utendaji wa mtu)
5. Mfano Mazingira ninayoishi, majirani zangu kila siku visomo na mambo mengine ya ushirikina... kiongozi haya yana athiri sana... elimu ya vijana mashuleni.
6. Fuatilia mashuleni haswa msingi na sekondari kila siku watoto wanadondoka mashetani 100% niwa wanafunzi wa kike wa dini ya Kiislamu... hii ina athiri sana elimu ya watoto....
Kwa ufupi kiongozi elimu ndio kila kitu... pamoja na utendaji wa mtu. Naamini watu hao wapo kwa dini zote mbili... ila ukweli ni kuwa wakristo mpaka sasa wanaongoza kwa wasomi....
Note: Shule nyingi za wakoloni ( zilikuwa zipo kikristo zaidi) viongozi wako mfano Mzee Makamba alisoma shule za mission.... lakini mzee makamba sio mdini... Kiongozi Achana na Mawazo ya Udini angalia utendaji wa mtu anafaa mpe kazi hafai achana naye. ACHA UDINI.
Africa ya kusini: elimu nzuri ya vyuo vikuu wanayo wazungu na ufundi wanao wazungu! Weusi kazi zao ni kucheza ngoma na kuoa wake wengi hivyo. Unapo Ajiri ajira zote uwape wazungu tu waafrika was ipewe maana walikuwa wapi wakati wazungu wanasoma? Ukielewa hilo utaelewa na ubaguzi wa hapa Tanzania
 
Shida ya waislamu huana haya wanapopewa mamlaka makubwa kama hivyo. Huyu Mama sio kama hajui anajua vyema msuguano uliopo baina ya imani hizi, ila basi tuu kapuuzia kwasababu anazozijua yeye mwenyewe. Hivi kweli ndio hakuna waislamu wa kutosha wenye elimu na ujuzi wa kuwekwa ngazi ya utawala wa katibu mkuu walau kufanya ile ratio iwiyana walau kwa 40% hadi 50%. Basi tuu ufedhuli wa wenye mamlaka na dharau. Ndio mwisho yanatokea ya Mozambique halafu mnasema wamekosa ustahamilivu.
 
Mkuu, hebu tutumie common sense na reason.

Sasa hivi Rais ni Muislam, Waziri Mkuu Muislam, mkuu wa Tiss ni Muislam, Katibu Mkuu Kiongozi pia ni Muislam
Hawa watu ndio Wana influence teuzi zinazofanywa na Rais, so hawa wanaweza wakawa wanapendelea Wakristu na kukandamiza Waislam wenzao? Ili iweje? Inakuingia akilini?

Au kuna force nyingine inayowalazimisha kuteua Waislam wachache? kama mnavyodai ni kanisa katoliki, kanisa katoliki Tanzania lina nguvu kiasi hicho? inakuingia akilini?

Mimi nimesoma shule ya bweni inayochukuwa wanafunzi nchi nzima. Kwenye ile shule wanafunzi wa Kiislam walikuwa hawazidi robo, japo ni taifa zima

Pia nimesoma Chuo Kikuu Mzumbe, ambayo ni taasisi inayochukua wanafunzi nchi nzima pia, Wamafunzi wa Kiislam walikuwa hawazidi robo mkuu

Hii inakupa picha gani? kuwa Waislam wanabaguliwa hadi kwenye elimu za msingi? Hapana, Hawazingatii elimu? Hapana. Hii inamaanisha kuwa Waislam Tanzania ni wachache kuliko Wakristo, na wala haliumizi kichwa hili, sababu ni mikoa mingapi hapa Tz ina Waislam hata nusu tu ya wakazi wote? Nadhani ni michache sana, Lindi, Zanzibar, Tanga labda na Dar. So tuache mihemko na tutumie mantiki zaidi tutaepukana na mawazo kama yako
Mkuu...achana na huyu jombaa ni mdini....anashindwa kukontrol hisia na mapenzi kwa dini yake...anataka kutumia kigezo hicho kugawa watu....huwa hatutumii personal feelings kuendesha nchi
 
Mama aliweka wazi kuwa ataangalia record ya mtu, hawa ndugu wanaoteuliwa si kwa ajili ya kusaidia dini flan au kanda flani bali ni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote wa tanzania, merits first.
Ukitaka azingatie hicho kigezo Cha dini utakuta kumbee hizo dini na zenyewe zimegawanyika
Mkuu na si KWA mama tu...nchi zote ambazo azifungamani na dini zina system hiii....huyu jamaa Analake jambo
 
Ha ha ha ha, mkuu, achana na mambo ya Dunia, mtafute Allah uione pepo.
Maana sasa unapinga kwa jazba tu,
Hilo gazeti lako la idadi ya Muslims lilipata kibali kukusanya hizo takwimu au waliangalia prospects za vyuo wakiwa vyumabani?

Tukileta gazeti la wasomi wa kikiristo litakawa na mamilion ya majina.
Tuache hizi mambo
Yap umenena vyemaa....sidhani kama amekuelewa......
 
Back
Top Bottom