Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

"Haiwezekani"..? ww kama nani nchi hii kupinga serikali ? kupinga teuzi za muheshimiwa rais? kwamba ww uko right kuliko hizo tume za vetting?

"Kuna mchezo mchafu tunachezewa"

Kumbe tayari una majibu yako kichwani tayari.

Uzuri mmoja sheria za nchi ziko wazi. ajira ziko wazi. qualifications huwa zinawekwa wazi.

Kama huna vigezo huna,kama unavyo unavyo tu.

Dini haikupi kazi baba.
 
Kama tunaweza kukemea bila hofu teuzi zilizokaa kikabila na kikanda ni muhimu pia tukakemea na zile zenye muelekeo wa udini, kwa sababu tusipokemea kuna watu wanaweza kutumia loophole hiyo ya Watanzania kugwaya kukemea ubaguzi wa kidini katika teuzi na ajira kutekeleza ubaguzi huo. Ni lazima tukiona viashiria vya ubaguzi wa kidini tuviseme, tusivinyamazie. Ni kuliponya taifa kutaka Fairness katika nchi
 
Hapo inabidi uanze kuangalia kuanzia ngazi za chini za serikali hali ipoje ndio utapata jibu
 
Hapo inabidi uanze kuangalia kuanzia ngazi za chini za serikali hali ipoje ndio utapata jibu
Kote huku chini kwa maDAS, maRAS, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi mashirika ya umma, mabalozi etc, Waislamu namba yao iko chini sana—Hili linahitaji majibu maana siyo fair
 
We mtoa mada ,sasa kwa Tanzania Wakristo ndio wengi unatoka akawaazime waislam kutoka Saud Arabi aje awape vyeo.

Hivi wewe huangalii hata huko unaopoishi mtaa/kijiji kina weza kukawa na Makanisa 5 lakini msikiti 1.Waislam kwa Tanzania ni 10% ya Wa Tanzania wote waliobaki ni wakristo.
 
Mada yako ina uchochezi na ni hatari kwa umoja wa taifa. Umetaja kuhusu dini mbili, lakini umejifanya hujui kuwa nchi hii ins dini zaidi ya hizo, kuna wapagani ambao ni kama theluthi hivi, wahindu, budha, sikh, n.k Je hao nao wakidai uwiano kwa dini zao? Pia hao waislamu kuna sunnni, shia, ismailia, bohora nk. Unaweza kuteua kwa mlengo wa kidini halafu wote wakawa dhehebu moja.

Wakristo ndio usiseme wana madhehebu lukuki kuanzia yake ya kitaasisi kama Catholic, lutheran, anglican na morovian mpaka yale ya mfukoni ambayo ni mali ya mtu mmoja mmoja lakini yanesajiliwa.

Nao wakidai uteuzi kwa uwiano je itawezekana? Kuna makabila 120 maana unaweza kuteua kwa kufuata dini lakini wote wakawa kabila moja.

Je utaweza kulipa kila kabila waziri? Kuna jinsia mawaziri wanaweza kuwa wa hizo dini mbili lakini jinsia moja au unaweza kubalansi jinsia lakini wakawa wa dini na dhehebu moja.

Haya mambo ndiyo yanapelekea kuwa na baraza kubwa la mawaziri kama kule sudan kusini, ambapo nchi ndogo maskini inajitwisha mzivo mkubwa kuhudumia mawaziri lukuki pasipo ulazima.

Rais anateua watu wa kumsaidia kazi kutokana na uwezo wao na mahitaji ya wakati.

Hoja yako kuwa uwaziri ni kipato ni sawa lakini ni kwa yule mtu mhusika sio kipato kwa ajili ya dini yake au kabila lake.


Hoja yako haina mashiko zaidi ya uchochezi na kutaka kumyumbisha Mheshimiwa Rais.
 
Ukiondoa waislamu na wakiristo, hao wa dini nyingine ni wachache sana nchini, by the way hata nao wakiwa included serikalini haina shida tena ni jambo zuri tu.

Hata hivyo hoja yako haiwezi kuwa kigezo cha kufanya teuzi ambazo kiajabu sana zinalalia mno upande mmoja mpaka inaraise alarm
 
Changamoto ni hiyo balance. Imagine wewe ndio rais unawaambiaje wasaidizi wako, nileteeni watu watano wa dini A na watano wa dini B?
 
Islam mmeishapewa Raisi,sasa mnataka nini?

Amiri jeshi mkuu ni islam,akiamua hata leo,ofisi zote za umma ziwe zinafungwa mara tano kwa siku Ili mpige Swala inawezekana.Nchi hii imeishakuwa na Maraisi watatu waislam,sasa kama hawawezi kutatua kero Zenu,mnataka nini?si huwa mnakutana nao huko masijid
 
Mkuu usituletee udini hapa ,tunacho taka ni kwamba mtu ateuliwe bila kujali ,dini,ukabila jinsia ,chamsingi awe ana uwezo na nafasi husika, mbona nafasi kubwa za juu kitaifa zipo KWA ndugu zetu na wakiristu hawajapiga kelele,huko Zanzibar vipi mbona wakiristu hawalalamiki ali Hali Hili ni taifa moja , tutolee udini hapa
 
Mambo ya dini, kabila na jinsia katika uteuzi ni sensitive lakini hayapo kikatiba.

Ili kupunguza malalamiko inabidi kuwe na watumishi wa namna mbili wa Kuchaguliwa na wengine waombe nafasi za kazi na kufanyiwa usaili
 
Haya maswala ya udini sijui kila teuzi tuangalie waislam wangapi na wakristo wangapi huu ni upumbavu na ujinga wa hali ya juu. Hawa watu wanao kua wanaleta huu ujinga ni wa kupuuza kunawatu wengi sana hawana dini nao walalamike na kuna siku hata hao waislam watasema mbona washia ndo wengi wanachagulia kuliko sunni na kuna siku wakristo watasema mbona wakatoliki wanachaguliwa kuliko walokole na hapo ndo tutakua tumefika pabaya.Huu upuuzi ni wa kukemea mapema .Mm naona ni upumbavu na ujinga kuaangali kila teuzi kidini hii Tanazanian ni ya kwetu sisi watanzania sio ya wakristo ama waislam na babu zetu walikua wapagani tu huu udini hautatusaidia.
 
nothing but truth brother. akikujib nitag
 
Hao 20 percent Muslims bado kuna watu wanamuona mama mdini.

Walitaka Muslim ikiwezekana wawe 1 percent I guess.

Hii nchi ngumu sana
Hilo liko wazi

Na mama asipokuwa na kukaza moyo majungu yatamuathiri sana
 
Wewe umelazimishwa kuwa mwislamu? tuna angalia utendaji kazi na siyo dini, hata wakiwa waislamu wote sawa tu
 
Sure, Zanzibar CABINET nzima ni waislamu tupu, inamaana Zanzibar hakuna wakristo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…