Tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu umri sahihi wa mtu kuitwa kijana

Binafsi mimi ni kijana mdogo wa miaka 38 na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Huu uzi umeandikwa na kijana. Pamoja na kujitambulisha ila kama kichwa cha habari kinavyosomeka imefika sehemu kama taifa tunahitaji mjadala kuhusu upi ni umri sahihi wa mtu kuendelea kuitwa kijana tofauti na hali ilivyo kwa sasa. SABABU KUU YA KUULIZA ni kuwa karibu kila sekta utakuta kuna wazee wanaojiita vijana hali inayowanyima fursa wale vijana halisi kiumri. HII HAIKUBALIKI.

Kwa mfano huko CHADEMA utakuta kundi la Heche, Lema, Sugu, Halima Mdee, Hawa Bananga, Mnyika, na Cecilia Pareso nao wanatajwa kama vijana. Tena bila aibu hata wao hujiita viongozi vijana. Sio sawa. CCM utakuta mtu kama Kigwangala, Nchemba, Bashe, Silaa, Ridhiwani, hata Nape kwamba ni wabunge vijana.. inashangaza sana.

Ndugu wanaJF mnadhani ujana hukomea miaka mingapi?
Chadema vijana wengi ni watu wazima lakini bado wanaishi kwa wazazi 🐒
 
Mkuu!
Unajua kwanini Miaka ya mwisho iliwekwa Ya kuajiriwa ni 45?
Unahisi ni kwa sababu ya Uzee?

Hapana!
Ngoja nikujuze

Mtumishi uanza kusomwa kuwa pensionable au kuweza kuanza kulipwa Pension ya uzee iwapo atakuwa amechangia zaidi ya miezi 180 ambayo ni sawa na miaka 15..(Kulingana na sheria za LAPF na PSPF ambazo kwa sasa Zinaitwa Sheria za PSSF)

Ukiajiri mtu Mwenye miaka 46 na kuendelea Hatakidhi vigezo vya kuwa Muajiriwa wa Pensionable terms..

Hivyo itaathiri Kuweza kupata Mafao ya uzeeni au huenda asipate kabisa akapata only Michango yake aliyochangia..

So haihusiki na uzee ila inahusika na mafao..

Usilolijua..
Sera ya Afya Ya mwaka 2007 ambayo bado inatumika..

Inamtaja Mzee Ni mtu mwenye Umri kuanzia Miaka 60..
Naonaa unapigania ujana mzee wangu.
 
Acha Hizo zako aliyekuambia zaidi ya miaka 45 wazee ni nani?
Au umejitungia sheria yako?
Wazee kuanzia miaka 60 na ndo maaana Serkali inajua na inawastaafisha..

Mimi nina miaka 52 na Bado ni kijana pengine kukuzidi hata wewe..

Ujana mwisho ni miaka 59
Ungetoa na sababu ili ueleweke

Ujana mwisho 39, 40s ni middle years(umri wa makamo)

Binadamu anaishi miaka 70 kwa wastani kwahiyo 30 ya mwanzo ni ujana, 30 ya mwisho uzee, ile 10 ya kati(ambayo ni 40s) ni umri wa makamo

50+ ni uzee

Kuwa mzee ni vibaya? Sidhani
 
Nimetoa Mkuu Post za nyuma hapo ila ngoja nirudie..
Ukisoma sera ya Afya ya mwaka 2007 (Ndiyi inatumika mpaka sasa)

Kipengele 5.4.8.3 kipengele kidogo (a) Maelezo
Kinasema

"Serikali inatambua kuwepo kwa wananchi wasio na uwezo wa kuchangia gharama za huduma za afya, ikiwa ni pamoja na wale walio katika makundi maalum ya kijamii, mfano wazee (Wazee ni walio na umri zaidi ya miaka 60)........."

Sio maneno yangu ni maneno ya Sera ya Afya..na Serikali
 
Binafsi mimi ni kijana mdogo wa miaka 38 na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Huu uzi umeandikwa na kijana. Pamoja na kujitambulisha ila kama kichwa cha habari kinavyosomeka imefika sehemu kama taifa tunahitaji mjadala kuhusu upi ni umri sahihi wa mtu kuendelea kuitwa kijana tofauti na hali ilivyo kwa sasa. SABABU KUU YA KUULIZA ni kuwa karibu kila sekta utakuta kuna wazee wanaojiita vijana hali inayowanyima fursa wale vijana halisi kiumri. HII HAIKUBALIKI.

Kwa mfano huko CHADEMA utakuta kundi la Heche, Lema, Sugu, Halima Mdee, Hawa Bananga, Mnyika, na Cecilia Pareso nao wanatajwa kama vijana. Tena bila aibu hata wao hujiita viongozi vijana. Sio sawa. CCM utakuta mtu kama Kigwangala, Nchemba, Bashe, Silaa, Ridhiwani, hata Nape kwamba ni wabunge vijana.. inashangaza sana.

Ndugu wanaJF mnadhani ujana hukomea miaka mingapi?
Mabro na masister wamegoma kuwa wazee sisi sijui tugome kuwa vijana ..

Basi kuanzia sasa mm ni mtoto wa 17 years..
 
Wewe ukishaona hujimudu , hata kutembea Km2 au kupanda ngazi ghorofa 5 huwezi hata kama una miaka 20 wewe umeshazeeka.Ujana ni kujimudu . Mchezaji wa miaka 25 unakimbizwa na mchezaji wa 38 halafu anakuweka benchi wewe ndio mzee
 
Nimetoa Mkuu Post za nyuma hapo ila ngoja nirudie..
Ukisoma sera ya Afya ya mwaka 2007 (Ndiyi inatumika mpaka sasa)

Kipengele 5.4.8.3 kipengele kidogo (a) Maelezo
Kinasema

"Serikali inatambua kuwepo kwa wananchi wasio na uwezo wa kuchangia gharama za huduma za afya, ikiwa ni pamoja na wale walio katika makundi maalum ya kijamii, mfano wazee (Wazee ni walio na umri zaidi ya miaka 60)........."

Sio maneno yangu ni maneno ya Sera ya Afya..na Serikali
Yaani kwanini uzee uanzie 60 na sio 50, 'serikali imesema' sio sababu ya kueleweka
 
Acha Hizo zako aliyekuambia zaidi ya miaka 45 wazee ni nani?
Au umejitungia sheria yako?
Wazee kuanzia miaka 60 na ndo maaana Serkali inajua na inawastaafisha..

Mimi nina miaka 52 na Bado ni kijana pengine kukuzidi hata wewe..

Ujana mwisho ni miaka 59
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom