Tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu umri sahihi wa mtu kuitwa kijana

Tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu umri sahihi wa mtu kuitwa kijana

Binafsi mimi ni kijana mdogo wa miaka 38 na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Huu uzi umeandikwa na kijana. Pamoja na kujitambulisha ila kama kichwa cha habari kinavyosomeka imefika sehemu kama taifa tunahitaji mjadala kuhusu upi ni umri sahihi wa mtu kuendelea kuitwa kijana tofauti na hali ilivyo kwa sasa. SABABU KUU YA KUULIZA ni kuwa karibu kila sekta utakuta kuna wazee wanaojiita vijana hali inayowanyima fursa wale vijana halisi kiumri. HII HAIKUBALIKI.

Kwa mfano huko CHADEMA utakuta kundi la Heche, Lema, Sugu, Halima Mdee, Hawa Bananga, Mnyika, na Cecilia Pareso nao wanatajwa kama vijana. Tena bila aibu hata wao hujiita viongozi vijana. Sio sawa. CCM utakuta mtu kama Kigwangala, Nchemba, Bashe, Silaa, Ridhiwani, hata Nape kwamba ni wabunge vijana.. inashangaza sana.

Ndugu wanaJF mnadhani ujana hukomea miaka mingapi?
Itapendeza sana ikiwa hivi...

Years..

0 hadi 14 = Mtoto
15 hadi 30 = Kijana
31 na kuendelea = MZEE
 
Miaka kuanzia 36 ni mzee? You can't be serious mkuu.

Mtu wa miaka 36 ni mbichi kabisa hana tofauti na wa miaka 26.
I think it's you who isn't serious. Alie kuambia ukitoka ujana unaingia uzee ni nani?
Sasa Kwa taarifa yako kijana ni kuanzia miaka 15 Hadi 24 Kwa mujibu wa UN. Nchi au kwe nahitaji Fulani wanna extend Hadi 35.

NB: UKITOKA KWENYE UJANA UNAINGIA UTU UZIMANA SIO UZEE.
 
Mwanamke anaanza kuonekana mzee akifikisha 55 ila akijitunza hadi 50 anaonekana kigori ila kwa wanaume mipombe+mikazi migumu+stress+uzinzi+misosi mibovu ukfikisha 40 ushazeeka.
Nikweli mkuu,orodha niliyoitoa ni Kwa mjibu wa maisha ya kawaida kulingana na uafrika wetu kimazingira.

Hivyo maisha yakiwa mazuri Kila mtu ni mchalo.
 
Back
Top Bottom