Tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu umri sahihi wa mtu kuitwa kijana

Kijana > mtu wa makamo > Mzee

40s na 50s ni watu wa makamo
 
Je unafahamu hata huko CCM kwa miaka yako siyo Kijana? Kwa miaka yako huwezi kugombea nafasi ya uongozi jumuiya ya vijana wa CCM, lakini bado unajiita kijana.
 
Mwisho 35 hao wote wanaojiita vijana ilhali washavuka hapo, bi kujiognopea tu na kujaribu kujilinganisha na wazee wao ambao bado wapo kwenye mifumo thats why wanajiona vijana
 
Enhee..Na kwa mujibu wa hiyo sera kuanzia mwenye miaka 36 tunamuitaje?
Hiyo sera haiongelei watu wenye miaka zaidi ya 36 kwani sio vijana Kwa mujibu wa hiyo sera.
Pia tambua kuna sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 labda wapo Kwenye kundi hilo ila Sina uhakika
 
Kwa maelezo ya hiyo makala, uzee tz utaanzia kwenye 50s
View attachment 2892193
Uzee Tz nimekuonyesha mkuu kwa Mujibu wa Serikali unaanzia Miaka 60s
Na nimekupa Sera ya Afya kwenye kuzungumzia Uzee..
Ila ukasema unataka Sources nyingine nimekupa Umeanza kutengeneza Tena consiperacy wakati facts zipo za kitaifa na nimekupa..
 
Wewe ukishaona hujimudu , hata kutembea Km2 au kupanda ngazi ghorofa 5 huwezi hata kama una miaka 20 wewe umeshazeeka.Ujana ni kujimudu . Mchezaji wa miaka 25 unakimbizwa na mchezaji wa 38 halafu anakuweka benchi wewe ndio mzee
Huyo ni mgonjwa ana maradhi! Sio mzee!
 
Huyo ni mgonjwa ana maradhi! Sio mzee!
Tofautisha kujimudu (FITNESS ) na ugonjwa. Mpira ni dakika 90 halafu dakika 45 timu hoi, huwezi kusema wachezaji ni wagonjwa ila FITNESS level ipo chini. Ndio unakuta mchezaji wa 38 yupo vizuri uwanjani kuliko yule anayeitwa kijana mwenye miaka 23.
 
Kama nani anayeishi kwa wazazi?
utasababisha vita ya mitusi na kuharibu mjadala.

dalili za mtu mzima anaishi kwa wazazi na ni mtu mzima ziko wazi zinaonekana check level ya mihemko, ghadhabu, mitusi, kuzira na kususa 🤣

movements of the bodies, the tones and rhythm of words and language they use on their articles, their facial expressions when you meet them etc
 
Ujana unategemea na jinsia,kwa wanawake unaishia miaka 30 baada ya hapo ni shangazi/mama/bibi.....kwa mwanaume ujana unaishia miaka 59 baada ya hapo ni babu
 
wanatoka umoja wa wanawake wanarudi umoja wa vijana yaani vululuvululu.
 

Ujana sio Umri bali ni Afya+Muonekano+Uimara wa mwili.

Unaweza ukawa na 20 lakini ukaonekana babu na mtu wa 45 akawa kama 20s.
 
Mimi nadhani tafsiri ya ujana ama uzee iangazie zaidi muonekano wa mtu husika.

Kuna watu wana miaka 50 lakini muonekano wao kama miaka 30 hadi unayejiita kijana wa wa miaka 24 unaona aibu kumuamkia maana unamuona kama age mate wako tu.

Hapo hapo unakuta kijana wa miaka 30 tu anapewa shikamoo na kijana wa rika lake kwasababu ana muonekano wa kizee.
 

Mwanamke anaanza kuonekana mzee akifikisha 55 ila akijitunza hadi 50 anaonekana kigori ila kwa wanaume mipombe+mikazi migumu+stress+uzinzi+misosi mibovu ukfikisha 40 ushazeeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…