Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...


Mkuu,
Lengo la muungano huu ilikuwa si kuipata Tanzania tu Bali ilikuwa njia ya kuipata USA(United States of Africa).Lakini kwa kuwa wanasiasa wameshindwa kuja na mfumo wa kisiasa unaoleta usawa Kati ya Tanganyika na Zanzibar basi ni bora tu Tanganyika irudi tu labda tukikutana kwenye shirikisho malengo ya Afrika moja yatarudi tena.
Mwisho,tungekuwa na nia ya dhati na muungano tungeweka muungano wa serikali moja lakini mbili au tatu ni kudanganyana!

Asante!
 
Inakuwaje ije katiba mpya bila tanganyika kuja kwanza?ilikuwa ije tanganyika mwanzo halafu ndo katiba mpya,kiini macho.
 
Bashiru Ali amesema kupitia BBC eti Uzanzibari na Utanganyika ni UKABILA, kwamba eti Sudani Kusini inavopigana vita ya wenyewe kwa wenyewe ni sababu ya utengano na toka Sudani. Huyu na mhadhiri pale UDSM na kawalisha vijani wake upotofu huu. Sudani ilikuwa moja na ilitengana kutokana na masilahi ya kiuchumi, Tanzania iliunganishwa na Tanganyika na Zanzibar kama ilivokuwa Ethiopia na Eritrea na hawatoi mfano huu wa Eritrea kutoka Ethiopia ila wanaogofya watu kwa kutoa mfano wa Sudani Kusini.
 
Wakafie mbali huko...Tanganyika ni lazima irudi ebo..!
Mkuu, pana hawa wahadhiri wa UDSM Bashiru Ali kupitia BBC kawaogofya watu kwa kutoa mfano wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudani Kusini na Sabatho Nyamsenda kupitia gazeti la ----- la tarehe 2 mwezi huu anatoa data za hovyo kabisa eti asilimia kubwa haiitaki rasimu hii ya katiba inayoelekeza muundo wa serikali tatu. Sasa CCM ina wanachama wasiozidi milioni 5 hivi lakini ndio inayotawala nchi kwa kupigiwa kura na baadhi ya Watanzania. Kuwa na wahadhiri hao chuo kikuu tena cha umma ni hatari kwa elimu kwa vijana.
 
Lazima Tanganyika irudi kwanza, mengine baadae. Huyu Bashiru Ally huyu...
 
Wala hauko pekee katika kulilia Tanganyika
hakika tuko wengi waililiao Tanganyika
Wale walio wavivu wanyonge ndio hawaitamani Tanganyika
Muungano wa kweli ni wa kuiheshimi Zanzibar sawia na Tanganyika
Hivi ilikuwaje ikawepo Zanzibar Bila kuwepo Tanganyika?
Hakika naupenda muungano wenye usawa wa Zanzibar na Tanganyika
Sipendi sana Tanzania bara badala ya Tanganyika
Iweje Zanzibar iitwe Zanzibar halafu nchi yangu isiitwe Tanganyika???????
 
Miaka mitano ijayo mafuta yatakuwa hayana thamani tena ,kama hiyo ndio sababu ya kuvunja muungano basi mmepoteza
Imebakiza michache tu tuone kama mafuta hayana thamani tena ? Na maji lini yatakuwa hayana thamani ?
 
Mimi hawa wapemba na ardhi yetu huku boko bunju siwataki kabisa warudi kwao zenj haraka Tanganyika irudi bana.
 

Hivi haya mawazo mgando na kukariri kutaisha lini. Mtu mzimA na akili zake anaamua kuwa zuzu kiasi hiki kwa makusudi.Hii haina tofauti na kusema Mult Party system ni vita! Sasa ukisoma yale muanzisha UZI,yeye anaililia Tanganyika yake, halafu wewe unasema swala la KUVUNJA MUUNGANO, hayo ni mawazo yako tu bhana. Watu wanataka kulazimisha kuwa Tanganyika ikirudi basi Muungano unakufa! Hiyo siyo kweli. Ila kama itafanyika hujuma ya makusudi labda kama wale Fundamentalist na wahafidhina wasiopenda 3 Government.
 
Nirudishie TANGANYIKA Yangu...

Kama ni Muungano mnaogopa kuvunjika, Mbona palikuwako Zanzibar na muungano ukawepo mpaka Leo??


Wacheni Mboyoyo na Ulaku ninyi Watawala, Rudisheni TANGANYIKA Yangu.
 

Acha uwoga ww, Usipende kuhukumu kitu usichokiona. Hyo Tanganyika ulishawahi kuona mpka useme tutashindwa.Tanganyika iwepo tukishindwa ndo utuhukumu na hatutashindwa.Tanganyika hakipata uhuru ili iungane na Zanzibar ilipata uhuru ili iwe nchi huru,muungano ulitokea tu.
 
Ninafuatilia Bunge la katiba kwa umakini. Ninawaona vile wazanzibari wanavyoiongelea nchi yao. Wanaitamani Zanzibar huru. Wanaitamka Tanganyika bila hofu. Wabara wanajiita watanzania bara. Ifike muda muda sasa hawa wajumbe wa bara wavue wogs na kuitamka Tanganyika maana wapende wasipende wazanxibari wanaitaka nchi yao. Wajumbe wetu wajiandae kwa serikali tatu na uzao mpya wa Tanganyika
 
Huo ni ukweli usiopingika. Hata CCM wanajua hivyo ila wanajifaragua tu! Huwezi kuwalazimisha Wazanzbar vinginevyo! Watanganyika mara nyingine ni Wadanganyika ndo maana hata sasa wengine kati yao pale Bungeni wana rasimu feki kwa sababu ya udanganyika wao lakini ukweli utabaki palepale. Tanganyika hiyoooo inakuja!
 
Tanganyika nchi yangu!!rudi Tanganyika!nakupenda Tanganyika
 
Nyerere alitusomesha hivi....kuna watanganyika...kuna wazanzibari....na kuna wazanzibara....unawajua wazanzibara? Tafakari. (2 ) Nyerere alitusomesha tena hivi...ataigeuza pwani kuwa bara na bata kuwa pwani..je unawajua wa pwani? ndio waswahili...jiulize...pwani unaweza kuiita tanzania bara tafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…