Tunajikumbusha kidogo tu ili kuweka kumbukumbu sawa

Tunajikumbusha kidogo tu ili kuweka kumbukumbu sawa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
1907.
Ujenzi wa reli ya kati
Wazee wetu walichapwa sana mijeledi
Malaria pia ikawamaliza
Mjerumani amekataa kutoa takwimu

FB_IMG_1687357353026.jpg
 
RTC Kigoma.
FB_IMG_1687357777654.jpg

Siku hii ilikuwa ni ya ajabu sana hapa mkoani Kigoma, siku iliyo valiwa hiyo jezi ilikua ni mechi kati ya RTC Kigoma Vs Simba SC Tanzania katika uwanja wa Lake Tanganyika Stadium.

Matokeo ilikuwa ni RTC Kigoma (2) Vs (0) Simba SC Tanzania wafungaji wa magoli hayo walikua ni Makumbi Juma na Sanifu Razaro
JEZI hizo ziliazimwa kutoka Seminari ya ujiji na geti walilopitia RTC Kigoma kuingia uwanjani ni geti la upande wa jukwa la URUSI.
Siku hii uwanja wa Lake Tanganyika ulijaa mapema sana mnamo saa tano asubuhi kulikua hakuna nafasi ya kukaa.
Kipindi hicho mkuu wa mkoa wa Kigoma alikuwa hayati MZENDAKAYA.
Ilikua ni Mwaka 1989.

Kipa wa Simba Moses Mkandawile alilia machozi baada ya dk 90 kumalizika ndani ya lake tanganyika stadium

Wachezaji hao wa RTC Kigoma ni'
'Khalidi Rehani 'Makumbi Juma 'Moza Bonga
'Mavumbi Omary 'Sanifu Lazaro 'Iddy Cheche
'Cheche Kagire 'Tingisha Nassoro

'Ally katolila 'Amri Ibrahim 'Hamza Maneno
'Yusufu Mfaume 'Jumaa Haruna 'Issa Hassan
'Dadi fares 'Leopard Magesa 'Wastara Baribari
 
KUMBUKUMBU Aprili 7, 1994, mauaji ya Kimbari yaliyosababisha vifo vya watu takriban milioni 1, huku ikiacha historia mbaya kwa nchi ya Rwanda yalianza.

Wahanga wakubwa wa mauaji hayo walikuwa ni watu wa kabila la Tutsi, na baadhi ya wahutu waliokuwa wakiwaunga mkono Watutsi.

Andika ujumbe wowote kusisitiza kuitunza amani yetu.

1687358539509.png
 
View attachment 2664508
Hii picha ya kumbukumbu ya marehemu ATHMANI MOMBA AKIWA NA MKEWE LUCY BANDAWE
Picha walipiga mwaka 1993
Walioana mwaka 1994
Wimbo wa lucy bandawe alimtungia mkewe ndiye huyo
Lucy bandawe nimepele nyasa.......
Picha kwa niaba ya lucy Bandawe
Ujana mtamu, enzi hizo maandalizi ya kupiga picha yalikuwa yanafanywa a week before

Huyu dada alikuwa netballer mzuri sana na inavyosemekana huyo jamaa alivutiwa sana na hilo
 
View attachment 2664508
Hii picha ya kumbukumbu ya marehemu ATHMANI MOMBA AKIWA NA MKEWE LUCY BANDAWE
Picha walipiga mwaka 1993
Walioana mwaka 1994
Wimbo wa lucy bandawe alimtungia mkewe ndiye huyo
Lucy bandawe nimepele nyasa.......
Picha kwa niaba ya lucy Bandawe
Kuna Linah Bandawe pia alitajwa kwenye wimbo wa Mabinti wa Mwana Fa, je ana undugu na huyu mama?
 
Anatusimua maggid

Bongo Hapo Zamani: Vicent Urio Alifurumushwa Mbio Alipopaparazi Unyago Mwananyamala..

Ndugu zangu,

Mmoja wa wapiga picha mahiri kuwahi kutokea kwenye ardhi ya nchi hii ni Vicent Urio, pichani katikati.

Huyu alipanda madaraja ya utendaji akaja kuwa Mpiga Mpicha Mkuu wa Magazeti ya Serikali, Daily News na Sunday News.

Kwangu Vicent Urio ni mmoja wa wapiga picha walionifanya nipende sanaa ya kupiga picha.

Niliziona picha za Vicent Urio kwenye Daily News tangu nikiwa Shule ya Msingi.

Vicent Urio alikuwa mwembamba na mrefu. Hakika alikuwa na jicho la picha. Ukitazama picha zake uliweza kuona tofauti na za wengine.

Moja ya kilele cha mafanikio yake katika kuitumikia nchi ni kwa Vicent Urio kwenda mstari wa mbele kwenye Vita Vya Kagera dhidi ya Idd Amin. Vicent Urio akawa ' War Photographer'.

Nakumbuka tulifuatilia hali ilivyokuwa kwenye uwanja wa mapambano kupitia picha za Vicent Urio zilizochomoza zaidi kuliko wenzake.

Ni imani yangu kuwa Vicent Urio ni mmoja wa waliotunukiwa Nishani ya Vita Vya Kagera.

Vicent Urio alikutwa na nini Mwananyamala?

Tukio hili alisimulia Vicent Urio mwenyewe kwenye moja ya mahojiano aliyofanyiwa na mwandishi wa Daily News miaka ya themanini.

Vicent Urio alikumbushwa Mwananyamala, tena na wanawake waliokuwa kwenye mkole wa Kizaramo, kuwa Mwananyamala ni uwanja mgumu wa vita kuliko Kagera.

Vicent Urio alisikia habari za ngoma za unyago na hakuwahi kupiga picha tukio kama hilo.

Na sifa moja ya mpiga picha bora ni kuwa na kiherehere. Vicent Urio alikuwa na kiherehere cha picha. Akafunga safari ya miguu kutoka Daily News Maktaba Street hadi Mwanyamala.

Unyago ulikuwa ukifanyika kwenye ua uliozungushiwa makuti wa nyumba ya udongo. Vicent Urio alichungulia kwa kupekecha makuti. Akaona kwa macho yake, kuwa humo uwani kulikuwa na kikundi cha wanawake kama 20 hivi waliovalia kanga tu huku matiti yakionekana.

Kiherehere cha picha kikamwongezeka. Ili apate picha nzuri, akaona aparamie mpapai na kamera shingoni.

Akiwa juu ya mpapai, Vicent Urio aliweza kuona vema tukio lile na kulenga kamera yake.

Wanawake wale kwenye taratibu za unyago na midundo yake, walizima ngoma ghafla na katika wakati huo Vicent Urio alifotoa picha kwa kamera za zamani zenye kutoa mlio, kachaa!

Mwanamama mmoja akanyanyua macho kuangalia juu ya mpapai ilikotoka sauti ile.

" Jamani mmeliona dume lile juu ya mpapai!"

Kilichofuatia hapo Vicent Urio mwenyewe alisimulia, kuwa hakuamini kuwa amefika nyumbani salama.

Vicent Urio alijirusha kutoka juu ya mpapai na kuanza kutimua mbio na kamera shingoni.

Wanawake wale walichomoka kupitia kwenye ua wa makuti wakimwandama Vicent Urio wakiwa na bakora na mawe mikononi.

Vicent Urio si tu alikuwa na miguu mirefu na mbio, bali pia alikuwa na uzoefu wa kuwakimbia maadui kwenye uwanja wa mapambano. Alisalimika.

Vicent Urio kwenye hili alitufundisha, kuwa picha nyingine ni muhimu kupigwa na kubaki kumbukumbu. Lakini, anayepiga awe tayari pia kulipa gharama zake, ikiwamo kupokea mkong'oto.

Nilikuwa ni mmoja wa waliopokea kwa masikitiko habari za kifo cha Vicent Urio. Alifariki kwa maradhi. Ni miaka mingi imepita.
Screenshot_20230621-174910_Facebook.jpg

Maggid.
 
KUMBUKUMBU YA ANWAR SADAT:
Jumanne ya tarehe 6 Oktoba, mwaka 1981, Rais wa zamani wa Misri Hayati Anwar Sadat aliuawa katika shambulio la risasi alipokuwa anakagua gwaride la kijeshi jijini Cairo. Aliuawa baada ya kushambuliwa na wanajeshi waliokuwa katika msafara huo wa gwaride. Alikuwa jukwaani na viongozi wengine wakati shambulio hilo linatokea. Pamoja naye watu wengine kadhaa waliuawa pia.
Nalikumbuka tukio hilo kwa sababu siku hiyo ya tukio mwaka huo wa 1981, nikiwa kijana mdogo na anayependa sana kusikiliza taarifa mbalimbali za habari kutoka redioni, nililisikia tukio hilo wakati wa taarifa ya habari ya saa moja usiku kutoka Sauti ya Tanzania Visiwani (Zanzibar), taarifa hiyo ya habari siku hiyo ilisomwa na mtangazaji mmoja mwanamke lakini simkumbuki jina. Wakati huo nilikuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kigugu, kule Turiani, Morogoro. Nikiwa nacheza nje ya nyumba tuliyokuwa tukiishi katika kota za hospitali ya walemavu ya Chazi, taarifa ya habari ikisikika kutoka katika radio chumbani kwa mzee nami nikiwa chini ya dirisha nikaisikia taarifa hiyo ya redio kutoka chumbani nikiwa nje chini ya dirisha. Japo ni miaka mingi imepita lakini nalikumbuka vema tukio lile kama vile limetokea jana tu. Mtangazaji yule mwanamama alisema. Namnukuu." Cairo, Rais wa Misri Anwar Sadat ameuawa leo jijini Cairo, Misri baada ya kushambuliwa na askari walikuwa katika msafara katika gwaride la kijeshi jijini Cairo.
 
Screenshot_20230621-175639_Facebook.jpg

Sanamu hili linapatikana huko Vatican,mahala ambapo pamewekwa makao na kitovu cha Roman Catholic church,sanamu hili ni la kutisha kwa wengi,sanamu hili hujulikana kama ressuruction na lilitengenezwa ili kuwachochea waumini kua na kumbukumbu ya kiama au hatima ya maisha 🙄

Ukiangalia vizuri sanamu hilo utaona viumbe ambavyo vina muonekano sawa na Aliens,sijajua vina uhusiano gani hapo,huenda wapo watu wenye majibu zaidi wanaweza kutuambia 😳
 
KUMBUKUMBU YA MWANAMUZIKI SALUM ABDALLAH:
FB_IMG_1687359900362.jpg

Tarehe 18 Novemba mwaka huu ni siku ya Kumbukumbu ya Miaka 56 ya kifo cha mwanamuziki na kiongozi wa Cuban Marimba band ya Morogoro Salum Yazidu Abdallah aliyefariki kwa majeraha ya ajali ya gari mnamo Novemba 18, mwaka 1965

KIFO CHAKE:

Alhamisi tarehe 18 Novemba, mwaka 1965 ilikuwa ni siku yenye hekaheka kubwa mjini Morogoro, kwani ugeni mkubwa ulikuwa unasubiriwa katika mji huo.

Mheshimiwa Julius Kambarage Nyerere na Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa, viongozi wakuu wa nchi kwa wakati huo, walikuwa wakisubiriwa na wananchi wa hapo Morogoro katika sherehe ya kufungua Chuo cha Kilimo ambacho kwa sasa kinajulikana kama SUA (Sokoine University of Agriculture).

Pamoja na wageni hao pia alitegemewa kuwepo aliyekuwa Mbunge wa Morogoro mjini kwa wakati huo Mheshimiwa Oscar Thalatiel Kambona.

Bendi mbili kubwa maarufu za pale Morogoro mjini zote zilitegemea kupiga muziki siku hiyo, na pia zilipangiwa kutembelewa na viongozi hao wakuu wa nchi.

Kutokana na ushindani mkubwa wa bendi hizo wanamuziki na washabiki wa bendi hizo walikuwa roho juu kusubiri mpambano wa usiku huo.

Kwenye muda wa saa kumi na mbili jioni baada ya shamrashamra za kupokea viongozi kwisha bwana Ramadhan Mdidi aliyekuwa msaidizi wa mmoja wa madereva wa Salum Abdallah alikuja kumueleza mkuu wao huyo kuwa moja ya gari lake limenasa kwenye mchanga katika mkondo wa mto walikokuwa wakichimba mchanga, kwa hiyo ilikuwa busara kuliondoa gari usiku uleule au la kama mvua ingenyesha gari lingeweza kuchukuliwa na maji.

Salum Abdallah akaagiza gari likavutwe.

Salum Yazidu Abdallah ndiye aliyekuwa kiongozi muimbaji wa bendi ya Cuban Marimba, pia alikuwa ana malori kadhaa aliyokuwa akimiliki na akiyatumia pia katika mradi wa kujenga nyumba za National Housing pale Morogoro kwa wakati huo.

Salum akamtuma mwanamuziki wake Waziri Nyange atangulie kwenye ukumbi ambako wangepiga muziki ili kuweka vyombo sawa tayari kwa onyesho la usiku ili yeye aende na lori jingine kwenda kuvuta gari lililonasa kwenye mchanga.

Siku hiyo Cuban Marimba walikuwa wapige muziki Community Center wakati wenzao Morogoro Jazz Band walikuwa wapige muziki Kichangani.

Kiasi cha saa moja hivi mmoja wa waliokuwemo kwenye lori lililoondoka na Salum Abdallah alirudi mbio nyumbani na kuwataarifu kuwa kumetokea ajali na Salum ameumia.

Ajali hii ilikuwa ya ajabu na imekuwa daima ikileta maneno kwa walioikumbuka.

Kwa maelezo ya waliokuwepo, giza lilikuwa limekwisha ingia na wakati lori likikaribia Msamvu taa zilizimika ghafla na gari likayumba lakini taa zikawaka tena, kiasi cha waliokuwemo kuanza kucheka, lakini kicheko chao kilikatika ghafla baada ya kugundua kuwa mlango wa upande aliokuwa amekaa Salum ulikuwa wazi naye amedondoka.

Walirudi nyuma na kumkuta akiwa kalala barabarani akiugulia kwa maumivu.

Mzungu mmoja alipita wakati uleule na gari dogo akawapa lifti watu wawili toka kwenye lile lori, mmoja akaenda nyumbani kwa Salum kutoa habari na mwingine akaenda kuchukua taxi iliyomchukua majeruhi mpaka hospitali.

Hivyo wote waliopata habari wakakimbilia hospitali wakamkuta mwenzao anaugulia maumivu, madaktari walimuomba anyooshe mikono na kisha miguu alipoweza, wakaamini hajavunjika bali ni maumivu ya juu juu ambayo yangeisha, kiasi cha kumruhusu arudi kwake na awahi matibabu kesho yake asubuhi.

Salum mwenyewe akawaambia wenzie wafungue vyombo wasipige dansi siku ile, wengi wakakesha nae.

Usiku kucha ulikuwa wa maumivu makubwa, asubuhi mgonjwa alipelekwa hospitali akafanyiwa upasuaji ikagundulika alivunjika kiuno na mifupa alipasuka kibofu cha mkojo, jambo ambalo kutokana na kuchelewa kugundulika lilikuwa ni baya sana.

Kama saa 7 mchana alitolewa chumba cha upasuaji na wenzie waliokuwa wakisubiri wakaambiwa waende makwao wakale vizuri ili waje baadaye kutoa damu kwa ajili ya mgonjwa.

Wakatoka kwa furaha wakijua mambo yatakuwa mazuri. Walielekea kwenye klabu yao wakatengeneza chakula na kula kwa furaha. Kulianza hata kuwa na utani kuwa "Mwarabu" akipona atatoa kibao kikali cha tukio hilo. Ikumbukwe kuwa baba yake Salum alikuwa Mwarabu halisi. Lakini ilipotimu saa kumi jioni taarifa ikaja kuwa Salum amefariki. Watu wakaanza kumiminika nyumbani kwake, wakakuta hata maiti imeshafikishwa kwake na imewekwa katika chumba kimoja ambacho kilikuwa kimetayarishwa kwa ajili ya fremu ya duka.

Inasemekana baada ya Salum kufariki Daktari Mkuu wa Mkoa aliendesha gari lake hadi nyumbani kwa Salum na kupaki gari lake nje na kuanza kulia jambo ambalo mara moja ndugu walielewa kuwa mambo yameharibika, hivyo waliweza kutayarisha sehemu hiyo ambayo iliwezesha watu kuja kuweza kuona mwili wa Salum kwa mara ya mwisho.

Haikuchukua muda habari zilisambaa na ulinzi ukalazimika ukimarishwa kwa kusaidiwa na polisi.

Watu wakakesha na marehemu.

Kesho yake hali ilizidi kuwa ngumu wakati wa kusindikiza maiti kwenda makaburini ilikuwa kama kila mtu alikuwa akitaka japo abebe kidogo jeneza, hadi ikalazimu FFU wawepo kuleta amani.

Jeneza la Salum liliweza kubebwa kutoka Nunge nyumbani kwa mama yake hadi Msamvu kwenye eneo alipozikwa, watu wakiwa wamejipanga mstari mrefu, hakukutumiwa gari.

KUJITABIRIA KIFO CHAKE KUPITIA WIMBO WAKE:

Wimbo wake wa WALIMWENGU alioutunga kabla ya kifo chake pia ulileta tafsiri nyingi hasa kutokana na kifo chake cha ajabu.

Wimbo wenyewe huu hapa:

WALIMWENGU:

Eeeeh Mola wangu eeeeh Mola wangu,
Nivue na ya dunia,
Hao walimwengu, hao walimwengu,
Wanitafuta kwa madawa,
Wataka wadhulumu roho yangu,
Wapate furahia,
Natoa salamu zangu,
Ningalimo mu dunia,
Kwa ndugu na jamaa zangu
Za mapenzi na furaha
Za kuwatoa uchungu
Ajali itakaponifikia
Nahadithi ndugu zangu,
Nyuma waliobakia,
Kubeba maiti yangu
Huku wakinililia
Ninashtakia Mungu
Nilotendwa mu dunia.

Weka namba ya Whatsapp hapa upate wimbo huu na nyimbo nyingine za Gwiji huyu wa zamani wa muziki nchini Tanzania.

Source:

Anko John Kitime John Mwa Kitime na Wikipedia.
 
FB_IMG_1687360347671.jpg


Juni 26, ni siku aliyofariki aliyekuwa Mbunge kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amina Chifupa, Mwanadada huyo alijipatia umarufu mkubwa nyakati alipoingia Bungeni na kusema kuwa yupo tayari kufichua watu wote kwa majina wanaohusika na suala zima la dawa za kulevya hata kama angekuwepo mume wake angemtaja bila ya kusita, lakini kwa bahati mbaya Chifupa aliaga dunia siku ya kilele cha maadhimisho ya kupambana na dawa za kulevya duniani Juni 26, 2007.

Tunaendelea kumuombea aendelee kupumzika kwa amani
 
MARUDIO:
FB_IMG_1687360493419.jpg

The way back, 35 years ago, 1986:

Suleiman Mathew Luwongo nambari tano wa kutegemewa wa Tukuyu Stars wakati huo akisimama pale nyuma na Godwin Aswile Mlimba "Scania" kuhakikisha "custodian" Mbwana Makatta anakuwa salama.

Juu yao dimba la chini akisimama Aston Pardon, ukisogea kidogo kuna Yusuf Kamba na mbele katikati kuna yule mshambuliaji aliyekuwa mrefu na mwenye nguvu, Richard Lumumba akicheza pacha na nambari kumi wake Peter Mwakibibi mwajiriwa wa ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma na pembeni kuna Karabi Mrisho, mwenyewe wakati huo tukimuita "Stanley Ndunduma" huyu Ndunduma alikuwa winga wa kushoto wa Zimbabwe wakati huo. Hapo kuna wachezaji wengine kama kina Kelvin Haule huyu alikuwa na nguvu na anakimbia kama Tony Yeboah wa Ghana, John Alex Lwena, Hussein Zitto Kiaratu, winga Taisy Mwalyoga, kiungo Danford Ngessi, beki mstaarabu Daniel Chundu, beki kisiki Ally Kimwaga, golikipa wa akiba Selemani Mwankenja na wachezaji wengine wengi.

This was Tukuyu Stars!
Banyambala!

Walipanda daraja katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga mwaka 1985, wakaondoka mjini humo wakiwa hawajui kuwa wamepanda daraja hadi walipofika mjini Manyoni ndipo wakajua kupitia kipindi cha michezo cha Redio Tanzania Dar es salaam. Kwa furaha mfashili wa timu Ramnik Patel "Kaka" aliendesha Lori la Isuzu tani saba walilokuwa wakisafiria wachezaji hadi mjini Tukuyu.

Mwaka 1986 walianza kucheza ligi daraja la kwanza hadi wakachukua ubingwa na kuwa timu ya kwanza kutoka wilayani kupanda daraja na kuchukua ubingwa wa ligi daraja la kwanza Tanzania Bara.

Walipoteza mechi tatu (Suleiman Mathew) ananiambia walipoteza mechi mbili tu mwaka huo, kwamba Pamba walimpiga nje ndani kama Yanga.

Walifungwa na RTC Kagera kule Kaitaba bao 1-0, Pamba ya Mwanza Kirumba 1-0 na Simba ya Dar es Salaam uwanja wa Sokoine bao 1-0 bao la Edward Chumila baada ya Suleiman Mathew Luwongo kumkwatua Zuberi Magoha nje ya 18 na Ramadhani Lenny Maufi kupiga faulo ya akili ambayo Edward Chumila aliutokea mpira na kwenda kuujaza wavuni. Lakini katika mechi ya kwanza jijini Dar es salaam, Simba ililala kwa mabao 2-1.

Yanga ya Dar es salaam kama nilivyosema hapo juu ilipigwa nje ndani. Ikianza kupigwa jijini Dar magoli 2-1 na miini Mbeya Yanga illala bao 1-0 bao la kona ya moja kwa moja iliyopigwa na nambari tatu wa Tukuyu Stars Daniel Chundu na mpira kujaa wavuni.

Nilihudhuruia mechi karibu zote za Tukuyu Stars katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mara nyingi nikisafiri kutoka mjini Tukuyu umbali wa kilometa kama sabini hivi baada ya kuwa namuomba ruhusa marehemu bibi yangu niliyekuwa nikiishi naye bibi Tunsume Kilasa Mungasulwa Mwamafupa Mwaipaja "Gwamumpata" "Gwammasoko" naye bila hiana akawa akiniruhusu kwenda mjini Mbeya kuangalia mechi hizo. Mwaka huo nilikuwa darasa la saba katika shule ya msingi Mabonde Tukuyu.

Mechi yangu ya kwanza kuhudhuria ilikuwa kati ya Tukuyu Stars na Biashara ya Shinyanga na Tukuyu Stars ilishinda kwa magoli 2-1. Baada ya hapo kila weekend ilikuwa lazima niende Mbeya ama kwa lori la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe lililokuwa likiendeshwa na dereva mmoja tukimuita Hamza au nikisafiri kwa kupata lift ya baba wa rafiki yangu tuliyekuwa tukisoma wote shule ya msingi Mabonde, Costantino Nyilawila ambaye mzee wake alikuwa Mhasibu wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe wakati huo. Costantino pia ni kaka wa bondia maarufu nchini, Karama Nyilawila.
 
Novemba 1, 1981, alizaliwa muigizaji wa filamu wa Ufilipino, Rodel Pacheco Nacianceno maarufu kama Coco Martin.
FB_IMG_1687360649755.jpg
 
Anatusimuli maggid

Bongo Hapo Zamani… Na Sasa…

Picha ya kwanza niliipiga mwaka 1986. Ya pili ni ya leo, 2023. Kituo ni hicho hicho, Posta ya Zamani, na miti ya mikungu ingalipo. Lakini, mazingira yamebadilika.

Maggid

PS:

Hizo zilikuwa zama za usafiri wa chai-maharage. Tangu zama hizo, nikiwa mdogo sana, nilitamani sana kupiga picha na kuzihifadhi zije kuwa kumbukumbu. Napenda sana historia.
Naam, tuliopanda chai-maharage tutambuane.
FB_IMG_1687360824289.jpg
FB_IMG_1687360828263.jpg
 
Back
Top Bottom