Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
- Thread starter
- #21
👉🏾Ukiacha ile Yanga ya kampa kampa tena Yanga (2016) kuna ile Yanga ya 2014 yanga ya kina Cannavaro Didi, Yondani, Ngassa, Msuva, Okwi, Chuji, kiiza, Domayo , Twite Joshua, Bahanuzi kavumbagu na wengine.
👉🏾Ambayo kwenye vikosi bora Ambavyo klabu ya Yanga imewahi kuwa navyo pale jangwani basi kikosi hicho cha 2014 kilikuwepo.
👉🏾1march 2014 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza (first round leg) ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga alicheza na Al Ahly katika uwanja wa Benjamin mkapa (Zamani taifa) na Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri bao la dakika ya 83 lilofungwa na beki Nadir Haroub "Cannavaro " akimalizia kazi nzuri ya mpira wa kona wa Simon Msava.
👉🏾Mchezo wa pili ukapigwa Misiri tarehe 9March 2014 ambapo yanga walikuwa na kiwango Bora sana Al Ahly wakisubiri mpaka dakika ya 71 kipindi cha pili ndio wakarudi mchezoni kwa bao Sayed Moawad na mchezo kumalizika kwa sare ya jumla ya kufungana bao moja kwa moja kwenye (aggregate ).
👉🏾Kwenye Changamoto ya mikwaju ya penalti Al Ahly akashinda kwa mikwaju ya penalti 4 kwa 3 . japo haikuwa rahisi kwenye mikwaju ya penalti Dida aliokoa penalti (2) penalti ya 4 na 5 ya Al Ahly zote aliokoa. huku kwa Yanga Oscar Joshua na Said Bahanuzi wakikosa penalti ya 4 na 5 . Kisha katika penalti moja moja Mbuyu Twite akakosa penalti yake . na Yanga kutolewa.
👉🏾Hapo Al Ahly ndio alikuwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo alichukua (2013) Hivyo Yanga aliondolewa katika mashindano hayo na Bingwa mtetezi. japo ilikuwa katika hatua ya awali ya michuano hiyo lakini watu walisema "Yanga amekufa kiume"
👉🏾kwenye moja ya michezo ya kimataifa ambayo ipo katika kumbukumbu za mashabiki wa Yanga basi ni mchezo huo kwa sababu ya wengi kuamini yanga walikuwa bora sana . na wengine waliamini kama sio uzembe wa wapiga penalti Basi Yanga wangesoma mbele.
👉🏾 Nafikiri hii ni kama ilitokea jana kwa Simba tofauti yake Yanga ilikuwa katika hatua ya awali ya ligi ya mabingwa Simba katika hatua ya Robo fainali ya ligi ya mabingwa.