Tunajua Mengi tunanyamaza, Lissu kudharau Mamlaka ya Ikulu kumefanya kufifisha juhudi zilizopangwa na Rais Samia kuleta maridhiano

Kisingizio kisicho na mshiko, vyama vya upinzani siyo Lissu na watanzania siyo Lissu. Zuio la mikutano ya vyama vya upinzani na kuwalazimisha watanzania kuisikiliza CCM pekee kunawanyima watanzania haki ya demokrasia, bahati mbaya viongozi wa CCM wanadhani demokrasia ni vyama vya upinzani tu!
 
Ulizaliwa lini? Ni kipindi gani tangu mageuzi ya kisiasa yaruhusu mfumo wa vyama vingi 1992 aliwahi kutokea mwana-CCM aliyewahitaji wapinzani?
 
Mama Samia Raisi wetu mpendwa mm nakuomba Uvae tu VIATU vya Marehemu hata kama vitakupwaya hawa watu ni PUNDA hawendi mpaka kwa bakora ,waswahili chakula cha simba tu ,huna wema wowote utaofanya wasikuseme kwa ubaya watie adabu sana ili wanyoeke.
Ni wazi kuwa utawala bora uliishawashinda na mnauogopa.
Udhalimu huu huo mnaoutegemea kukubakisheni madarakani ndio msingi mkuu wa kuharibu amani na imani ya nchi hii na ndio utakaokuja ipeleka nchi hii pabaya
 
CCM ni wanyama ila kuna wakati hata upinzani kuna mambo unashangaa imekuaje anasema huyu ....Lissu anaongea mno mno na kibaya zaidi anajua kila kitu.
Mkiambiwa Lissu ni ziro brain mnabisha
 
Nyie ni watu hovyo kabisa. Watu wanaoumizwa ndio mnawalaumu?

Mnaua biashara za watu ili wawapigie magoti?

Akili ya hovyo kabisa hii.
Mbona wewe hujaumizwa ???

Mimi mtu akiumizwa kama Akwilini au Azory Gwanda nitamtetea.

Lakini wewe kama Rais anasema jambo fulani halitakiwi halafu wewe ukasema hapana, atake asitake utafanya maana yake uko tayari kwa vita na mapambano.

Sasa ukiingia vitani tena kupigania tumbo lako, ukapigwa unategemea mimi nianze kuhuzunikia mtu mpumbavu.
 
Ulizaliwa lini? Ni kipindi gani tangu mageuzi ya kisiasa yaruhusu mfumo wa vyama vingi 1992 aliwahi kutokea mwana-CCM aliyewahitaji wapinzani?

Ingekuwa hawauhitaji upinzani wangetumia nguvu za ziada namna ile kulazimisha wakina Halima Mdee waingie Bungeni kama wapinzani?

Hauwezi kujiita Demokrasi halafu katika Bunge lako chama kilichokupa ushindani mkubwa katika kampeni wakawa na mbunge mmoja tu. Hakuna atakayekuelewa.

Amandla...
 
Rais akisema uwe shoga utakuwa? Be specific wakati mnatoa hoja zenu. Watanzania sio wajinga
 
CCM ni wanyama ila kuna wakati hata upinzani kuna mambo unashangaa imekuaje anasema huyu ....Lissu anaongea mno mno na kibaya zaidi anajua kila kitu.
Nimesoma alichoandika,nimegundua vitu viwili:
1.Walimuweka Mbowe ndani kupisha vuguvugu la katiba
2.Wanaamini sasa Mbowe akitoka atatulia sasa

Wana propaganda wao wataandika sana sasa hivi kuonyesha tatizo sio Mama Samia bali alikuwa Magufuli,kwamba ndo aliandaa kushikwa kwa Mbowe
Na cha kusikitisha watatumika na watu wa ndani ya Chadema kuonyesha kwamba Samia hana tatizo,tatizo kalikuta
 
..na uhuni waliofanyiwa NCCR nao chanzo chake ni Tundu Lissu kutokupokea simu toka kwa Maza!!

..na uchaguzi wa marudio jimbo la Konde umefanyika mara mbili. Tatizo ni CCM waliiba kura ktk marudio ya kwanza. Je, hilo nalo tumlaumu Lissu aliyeko maelfu ya kilomita toka hapa nchini?
 
Mtoa mada huu ni ujinga. Tundu Lissu alilielezea kwa uzuri Sana kule space. Wewe unapotosha.
Lissu alisema siku alivyopigiwa Simu ilikuwa ghafla, akawaambia watafute siku nyingine wazungumze. Wewe unasema akamkwepa ,,,, akamkwepa. Uongo mtupu. Chadema Ndio walioandika barua ya kuonana na Samia . Wewe unatamka blabla hapa.

Kama Samia ameamua kumbakiziza Mbowe Kesi kisa Lissu amekataa kuzungumza nae basi hiyo ni ishara ya incompetence. Hafai kuwa rais.
 
Umeandika nini hiki wewe...?

Nimesoma "between the lines" yote uliyoandika, naweza kusema bila shaka yoyote kuwa, THIS IS TRULY A FICTION STORY 100% because it hasn't any tangible proof at all...

Umetumia "hearsay" kutengeneza story hii. Kwa sababu kwa nature na mtu wa calibration ya Tundu Lissu, hawezi kumkwepa huyu mwanamke kuzungumza naye....!

Ambacho amekisema mara zote na kwa uwazi kabisa ni;

1. Yeye kupitia kwa yule bwana katibu binafsi wa Rais Bwana Mkomya (kama sijakosea) kupokea simu ya TL kuomba amuunganishe na Rais ili azungumze naye na kupewa ahadi kuwa angepigiwa...

2. TL kushauriana na kukubaliana na M/Kiti Mh. Freeman Mbowe kuwa aandike barua rasmi kwenda kwa Rais ili wakutane nae kuzungumza maswala ya nchi. Ilifanyika, barua ikapokelewa na Rais kukubali na kuliweka kwa uwazi hili ktk hotuba take siku anahutubia bunge Dodoma kama Rais, kuwa atakutana na vyama vya upinzani kuzungumza nao..

3. Surprisingly, from no where kukawa na bonge la U - TURN kwa Rais juu ya jambo hili. Na siku chache baadae wakapigia TL simu lakini kwa maelezo yake mwenyewe alikuwa kwenye mkutano muhimu, aliyepiga simu akaelewa na makubaliano yakawa atapigiwa wakati mwingine...

4. Haya mengine uyasemayo wewe unaweza kuya - justify kwa namna gani...? Mwenzako TL anasema haya wazi kwa sauti kubwa kila mtu akisikia wakiwemo wahusika (Ikulu). Kama anaongopa si watoke wakanushe na waweke ukweli wao..? Mbona unawasemea wao? Wewe ni Kungai? IGP Simon Sirro? Au Gerson Msigwa msemaji wa serikali?
 
Zungumza agenda wewe mende. Achana na stori za wala mirungi.
Niko kwenye ajenda yako uliyosema rais akisema basi inatakiwa kufanywa. Ndio nikakuuliza akikuambia ufanye yale ambayo ni kinyume na msimamo wako utafanya kwa sababu rais kasema? Hii sio nchi ya kifalme kaka yangu.
 
Who is Tundu Lissu to say our president is incapable?!!

Who is he by the way?!!!

Deluded chap?

Psychopath?!!!

How would one treat this guy nicely while he got bad tough.....

It is havoc......

SIEMPRE URT!
Mke Mwenza wa Michenzani ningeshangaa nisingekuona hapa ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…