Tunajua Mengi tunanyamaza, Lissu kudharau Mamlaka ya Ikulu kumefanya kufifisha juhudi zilizopangwa na Rais Samia kuleta maridhiano

..ripoti mbalimbali zimeeleza kwamba tume yetu ya uchaguzi sio huru.
 
Chadema walishaikimbia nchi tuwe wakweli Mbowe na Kina Lema wameanza mipango ya kurudi Tanzania baada ya dikteta kuondoka

Mbowe alishaikimbia nchi?

Taarifa zako unaziokota kwa waliopewa jukumu la kumsimika huyu kuwa rais 2025?
 
CCM ni wanyama ila kuna wakati hata upinzani kuna mambo unashangaa imekuaje anasema huyu ....Lissu anaongea mno mno na kibaya zaidi anajua kila kitu.
Athari za risasi 16 siyo mchezo, huku ukiwa umedhulumiwa haki zako za ubunge na matibabu umenyimwa. Tuendelee kumuombea kwa Mungu apate utulivu wa akili ili achague mambo ya kuongea.

Likewise vitu vilivyo wazi kama stahili zake za ubunge na matibabu apewe tu bila masharti
 
Kwa hiyo wenye utulivu wa akili ni hawa:

1. Waliotuaminisha kuwa jiwe yuko busy na mafaili?
2. Wanaojenga ofisi kwa 19bn/- pesa za Hangaya?
3. Wakiifuta njia ambayo Yesu na mkewe walitembea?

Au

4. Hawa waliovaa viatu vinavyowapwaya vya mtu viliyekuwa vinampwaya?
 
Lissu bwanaa.....
Huyu Tundu Lissu alichojaliwa ni kuwa na uwezo wa kuona ya mbele sana. Tatizo lake anataka kuyaishi mambo ya miaka ijayo ndani ya muda wa sasa.
Ukijaribu kusikikiliza kauli zake na kuzifuatilia huwa hazipotei huishi na kujidhihirisha.

Imani yangu inaniambia kuwa huyu bwana Tundu Lissu ipo siku Taifa litamuona kuwa ni shujaa mkubwa sana.
 
CCM ni wanyama ila kuna wakati hata upinzani kuna mambo unashangaa imekuaje anasema huyu ....Lissu anaongea mno mno na kibaya zaidi anajua kila kitu.
Hivi kunabinadamu mwenye akili timamu bado anafuatilia mambo ya lisu??
 
..ripoti mbalimbali zimeeleza kwamba tume yetu ya uchaguzi sio huru.
Wenig wa waandishi wa ripoti hizo hawajui sheria, hivyo wanachanganya kutokuwa huru na kutokuwa inclusive.
Tume ya Uchaguzi ni Tume huru, tatizo za chaguzi zetu sio Tume huru ya Uchaguzi, ni sheria mbovu ja Uchaguzi.
P
 
Shida inaaminika ya kwamba ili uwe mpinzani unatakiwa kuwa mvurugaji mipango Kama Lissu.

Alipoingia mama Samia ilikuwa ngumu Sana kurudi katika siasa za kuaminiana na mama Samia, na kesi kubwa ni kwamba. Lissu hajawahi kumuamini mtawala kwasababu za athari za kiharakati alizopitia.
 
Si kila kitu kikiandikwa kinafanya kiwe UKWELI. Hizo ni hearsay tu za vijiweni.
 
Umeninukuu vibaya, nina sympathize sana na Tundu Lissu na nina advocate kuwa alipwe stahiki zake
 
Umenena vyema mkuu, hii si mara ya kwanza hao chama cha majambazi ku U-turn, Kikwete huku akibariki na kusaini rasimu za Warioba ili tupate katiba mpya daaaa!!!akageuka dakika za mwisho kwenye kulihutubia bunge,kinyago ukichonge mwenyewe kisha ukiweke sebuleni halafu unakikimbia.
 
Ndugu Tundu Lissu ni "bwakubwaku".....

"Too much know" asiye na ulimi wa nidhamu wala heshima.....

Si kila MTANZANIA anaihitaji katiba mpya.....
Tafiti ya TWAWEZA kila Watanzania watatu wawili wanahitaji katiba mpya..wewe utafiti wako umetoa wapi...
 
Umeninukuu vibaya, nina sympathize sana na Tundu Lissu na nina advocate kuwa alipwe stahiki zake

Kwenye red ni maneno yako niliyoyanukuu ili ulinganishe utulivu wa akili za Lissu na hao wanne nililokudokeza hapo juu:

Nina wengine kibindoni bado wakiwamo wanaowataka majaji kwenye hukumu zao kuzingatia uelekeo wa serikali.

Au hayo kwenye red siyo ya kwako?
 
..Waliotoa maoni hayo ni MAJAJI kwa hiyo huwezi kudai kwamba hawajui sheria.

..Hata ripoti ya Tume ya uchaguzi wa 2020 ina mmapendekezo na maoni ya kutaka kuipa tume uhuru ktk utendaji wake.
 
..Waliotoa maoni hayo ni MAJAJI kwa hiyo huwezi kudai kwamba hawajui sheria.

..Hata ripoti ya Tume ya uchaguzi wa 2020 ina mmapendekezo na maoni ya kutaka kuipa tume uhuru ktk utendaji wake.
Mara kibao tuu majaji huonekana wazi hawajui sheria na wanatoa maamuzi ya ajabu ajabu. Naendelea kusisitiza, kwa mujibu wa sheria iliyounda NEC, NEC ni tume huru tatizo ni sio shirikishi, na sheria yetu ya Uchaguzi ndio sheria mbovu.
P
 
Maridhiano yakipatikana hawa wakimbizi itabidi waondoke huko na familia zao na hawataki kurudi nyumbani. Pili hivi vyama vinakuwa full funded na mabeberu na asilimia kubwa ya fedha inaishia mifukoni mwa viongozi waandamizi. Kwa kifupi hatuna Upinzani Tanzania bali genge la wahuni
 
Mara kibao tuu majaji huonekana wazi hawajui sheria na wanatoa maamuzi ya ajabu ajabu. Naendelea kusisitiza, kwa mujibu wa sheria iliyounda NEC, NEC ni tume huru tatizo ni sio shirikishi, na sheria yetu ya Uchaguzi ndio sheria mbovu.
P

..maoni yako kuhusu uhuru wa tume sio sahihi. Yanapingana na maoni ya wanasheria wenye rekodi zilizotukuka na uzoefu ktk masuala ya uchaguzi na sheria zake.

..pia huwezi kuwa na sheria mbovu ya uchaguzi halafu ukaishia na tume huru ya uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…