Tunakwama wapi? Malawian Airlines (ndege 2) Vs Air Tanzania (ndege 11)

Tunakwama wapi? Malawian Airlines (ndege 2) Vs Air Tanzania (ndege 11)

Nimeshindwa kumjibu maana amesema wapumbavu tupo wengi!!

Ila nikunong'oneze tu, ukishakuwa na fleets za dreamliner 787 the only way to make profit is to go international. Wataalam wanasema angalau uruke masaa 13 kwa siku ,mfano Quantas dreamliber 787 ina route ya masaa 19 angani non stop.
Kama ni kweli tumenunua dreamliner kwa sababu ya local routes, ni sawa kabisa ma mtu anunue basi la yutong kwa safari za ubungo posta.
Sure. Hao Malawian Airlines Wana B737 LLW-BLZ-JNB linajaa. Nyie mnakimbizana DAR-MWZ.
 
Wanyasa kwa ufadhili wa Ethiopian airlines Wana ndege 2 wanafanya maajabu international destinations (DAR, NBO, LSK, JNB & HRE) . Sisi ndege 11 international destinations za kuhesabu kwann bado hatukamati destinations za maana? Tumirogwa?
Hii COVID ilipaswa kukamata alipofeli South Africa Airways ( DAR-JNB-CPT-DUR)

View attachment 2019984
Hili dude linarushwa na Captain Mansi.
 
CAG alisema ndege hizo zilinunuliwa bila hata kua na Business plan.

Nadhani kulikua na mgao wao kwny ununuzi wa hizo ndege,na lengo halikua kufanya biashara.
CAG abajua anachofanya? Mbona ndege zinaendelea kununuliwa? Au yeye amesoma makala ya mwaka 80 wakati leo ni 2021
 
Nimeshindwa kumjibu maana amesema wapumbavu tupo wengi!!

Ila nikunong'oneze tu, ukishakuwa na fleets za dreamliner 787 the only way to make profit is to go international. Wataalam wanasema angalau uruke masaa 13 kwa siku ,mfano Quantas dreamliber 787 ina route ya masaa 19 angani non stop.
Kama ni kweli tumenunua dreamliner kwa sababu ya local routes, ni sawa kabisa ma mtu anunue basi la yutong kwa safari za ubungo posta.
Sorry bro naomba nikuulize ... Qantas wanaruka destination zipi ambazo ni 19hours nonstop ? Maana nilisoma kwenye mtandao wa simpleflying.com na samchui.com kwamba walikuwa wanafanyia jaribio project yao moja inaitwa project sunrise ambapo walirusha ndege aina ya dremliner787 kutoka newyork hadi Australia kupitia London ambapo unashuhudia jua linachomoza mara 2 ukiwa angani.sasa sijajua kama ndio hiyo au ni ipi mdau nijuze
 
NEW YORK - SYDNEY
 
😄😄😄 hapana CAG hajui,Ila wewe ndio unajua unachokifanya.
Hujawahi kusikia nasema popote huu mradi haufaui. Yeye anasema halafu ndio fleet inazidi kuneneopeshwa. Lazima ajiulize anakosea wapi 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Sure. Hao Malawian Airlines Wana B737 LLW-BLZ-JNB linajaa. Nyie mnakimbizana DAR-MWZ.
Hapo sasa wanapata faida mara mbili! Boeing 737 ni ndege iliyoukuwa desined ikiwa na landing cylces nyingi za kutosha, wenzetu wanapoitumia ndege ya aina hii kwa safari ndefu maana yake ni kuwa wanaipa pia maisha marefu ya airworthiness , sisi ni kinyume chake sasa Boeing 787 ni heavy plane( wide body) , ndege hizi huwa kwa kawaida hazina landing cyles nyingi kutokana na uzito wake , ili upate faida kwa dream liner inatakiwa mizunguko ya kutua na kupaa iwe michache ili uweze kutumia mdege hii kwa muda mrefu na kupata faida.
Sehemu pekee hizi ndege kubwa zinapata faida kwa short routes ni Asia , Routes zao fupi zina guarantee ya kujaza ndege hata kama ni kubwa. Jappanesse carriers, JAL na ANA wamekuwa wanatumia madege makubwa kwa safari fupi fupi, imagine 2hours flight, walikuwa wanatumia boeing 747, !! ,
 
Kusafir raha Sana. Tatizo letu tumejifungia na Siasa za ilani
Surely kusafiri ni hobby yangu sema tu uchumi hauruhusu ila kusafiri kuna kujifunza mengi katika hii dunia, mfano unakutana na watu wapya, tamaduni, mpya ,vyakula vya kigeni n.k.
Hata kama ulikuwa una mawazo hasi dhidi ya jamii fulani popote pale duniani , ukitembea ndio unajifunza na ku respect cultural diversity ..
 
Waliopo Serikalini Wana uhakika wa mishahara, Wamebweteka...na hawana haja ya ubunifu...

Tabia ingine ni Kiburi, kwa Sababu ya nafasi walizopewa na mamlaka...Kwa maana hiyo hawasikilizi sekta binafsi...

Suluhisho: Mashirika ya umma kama ATCL yaendeshwe kwa ubia

Serikali, iuze hisa kwa sekta binafsi...Halafu Board of Directors inakuwa mchanganyiko wa Public na Private.

Faida yake ni Kwamba, Serikali itarudisha nusu ya Mtaji wa kununua hayo madege, na kupeleka sehemu zenye tija...

Mfano: kujenga miundo mbinu ya unwagiliaji kama Mabwawa na mifereji.

Tanzania izalishe vyakula adimu kama njegere, viungo na kuuza nje ya Nchi. Sekta binafsi itakodishiwa mitambo, walipe tozo kwa serikali.
 
Back
Top Bottom