Tunakwama wapi? Malawian Airlines (ndege 2) Vs Air Tanzania (ndege 11)

Nategemea kuna mtu kama yuko serious wa serikali au shirika la ndege Tanzania akapita hapa kama ataona wazo linamfaa itakuwa vizuri. Tanzania ndege zetu ni wazi ngumu kushindana na mashirika makubwa kama EK,Qatar au hata Ethiopia sababu network yao ni kubwa sana lakini tunaweza kuwatumia hawa tukawa kama feeder. Ni vizuri tukaingia sharecode mfano na EK ambao network yao dunia nzima wanafika halafu sisi tukaenda nchi ambazo EK hawafiki ha Africa au wakatupa route ili mfano akikata mtu ticket mfano toka Comoro anaenda France basi anakata ticket moja tu to Comoro to France air Tanzania anapanda anafika Dar switch to EK ticket moja na nchi nyingine kama Malawi hata Burundi hapo mpaka Congo ndege zetu zitakuwa main feeder wa EK zitafanya route nyingi daily. Sababu kushindina na hawa itakuwa ngumu sababu hata Dubai watu wanaitumia kama transit wengi tu na wako watashuka Dubai ni lazima tuwe na business plan tukubali uhalisia hatuna uwezo wa kufika sehemu nyingi. Kupata mteja toka Congo kuja Dar wako lakini limited ila wa Congo kuwapata kwenda hata ulaya wengi ukishare code na hawa ma giant ina add kwenye network yako. hili ni wazo tu
 
Kiwango chetu cha upumbavu kimeenda juu ghafla, watu wanakuja na hoja za kitoto. Unafikiri kwenda International ndio kutengeneza profit? See how big is our country, compare it with Malawi halafu tafakari upumbavu wako.
La afadhali na wewe umejiweka huko katika upumbavu. Sina swali.
Ila mleta mada alikuwa na maana yake. Wewe ungemjibu tu kwa busara in analytical ways lakini kujibu nchi yetu kubwa siyo jibu kabisa.
 
KAMA MABASI YA MWENDOKASI TUNASHINDWA KUSIMAMIA , UNAFIKIRI NDEGE NI MCHEZO
 
Watumishi wa ATC ni kama wamelazimishwa kufanya kazi wanazofanya. Mates ya abiria kwao hayawahusu na hawana kitunchochote cha kuwafanya wateja wao Waone furaha kupata huduma zao...inasikitisha sana hivi waliwapata wapi??
 
wewe uliimba wimbo huu, mabepari walia kukatiwa mirija. walipotangaziwa walipotangaziwa Azimio la Arusha! tafakari utapata jibu!
 
leo uwaite mabebebru mitandaoni na katika mikutano ya hadhara halafu unataka wakupe safari za anga?muulize Ronaldo alipomkandia kocha wake Man. United, Aliishia wapi?
 
Kwa anayeomba mgawanyo wa ndege Tanganyika na Zanzibar elewa uchumi wa nchi huchangiwa na idadi ya watu,
Idadi ya Watanganyika 59,800,000 na Zanzibar ni 1,890,000.
Kwa Hizi ndege 11 Zanzibar itapata 3.21% ya ndege zote.
Tungekua na ndege 100 Zanzibar ingepata 3.
Kwa idadi hii haziganyiki hivyo kitakachofanyika ni kurudishiwa pesa kidogo ya kununua Deri basi.

Sent from my STK-L22 using JamiiForums mobile app
 
Duuh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…