Tunalaani uwanja Chato, nchi hii upendeleo ulianza zamani Wachaga mkiongoza

Tunalaani uwanja Chato, nchi hii upendeleo ulianza zamani Wachaga mkiongoza

Maendeleo endelevu ni gradual process. Sehemu zote zinazotajwa kuwa zimeendelea, hazikufikia hali hiyo kwa mwaka mmoja, miwili, mitano, kumi na hata ishirini.
Fikra na ushabiki wa upendeleo wa mtu anapotoka, kabila au kanda ni matokeo ya upumbavu kupewa fursa na majukwaa katika jamii.
Taifa laweza kuangamia kama propaganda za kijingajinga zitatumiwa na wapumbavu kuhalalisha upuuzi.
Tujadili Maendeleo ya watu wetu kwa mtazamo mpana kwa mustakabali mwema wa taifa.
 
Labda nikuweke sawa. Historia ya Wakoloni popote pale itizame: Wakoloni kujenga shule haikuwa tafsiri ya wakazi wa eneo wanaokoloniwa wanapenda elimu. Tukumbuke mkoloni alikuja na malengo yake na ukamilishaji wa malengo yake iulifuata mfumo wake moja wapo ni suala la elimu.

Kwa hiyo ujenzi wa shule kwenye baadhi ya maeneo lengo ni kuweka daraja ambalo mkoloni litamsaidia kukamilisha malengo yake. Na hayo yote yaliwezekana ikiwa hilo eneo lilikuwa ni lenye amani. Kwa ufupi halikuwa na upinzani kwa Wakoloni. Wachagga hawana history ya kupambana na wakoloni.
Hakuna zawadi kubwa mtu aliyopewa na Mungu kama akili, hekima ni kitu bora sana! Wachaga walijitambua mapema sana. Haikuwa shida kwa wakoloni kuwabeba sababu walibebeka. Ona kama mjomba wetu alivyo jaa majigambo na ujuaji hivi ni nani mwenye akili zake atamsaidia!? Tunajifunza kwa walioendelea hiyo piga ua aliye kutangulia kakutangulia tu.
 
Daah, tumeishiwa vya kujadili, tunajadili vitu vya kijinga.
We have a long way to go, mimi ni mchagga, wachaga wanajua kubebana, wanasaidiana kwenye shida na raha. Tatizo la baadhi ya makabila huwa hawasaidiani, wanaoneana wivu, hilo nalo ni tatizo.
Suala la Kilimanjaro kuendelea sio kwa sababu za upendeleo wa viongozi, bali upendeleo wa wamisionari walioweka kambi kaskazini na kujenga miundombinu mingi kama vile shule na hospital pia na military base.
Tukiachana na bahati ya kupendelewa kama mnavyodai pia watu wa kaskazini ni watafutaji sana. Wapo maeneo mengi ya nchi wakifanya biashara. Mfano mzuri dar hapa tupo wengi na tunafanya biashara. Huko chato pia wachaga wakiona fursa wataenda kuzichukua na kwenda nazo kwao huku wanachato wakabaki wakishangaa.

Tuache ukabila na ukanda, tuangalie fursa zilipo hata kama ni chato.
 
Alichozungumzia jamaa Patriot ni sahihi, wewe unachojibu ndiyo unaharibu kabisa. Sisi wote ni Watanzania, na Tz inaundwa na makabila tofauti. Suala la ajira la kitaifa kwa vile mdogo wako ana sifa ndiyo umpachike? Ndiyo utaratibu huo? Hivi unafikiria kwa mapana kweli?

Wachagga mna ukabila na hili lipo wazi! Na huyu tuliyenaye ana hiyo tabia na hili lipo wazi. Muhimu ni kukubali kwamba tulikosea na tuing'oe hiyo mizizi.
Hakuna mtu anae unga mkono ukabila! Mi nasema binadam wote tuna ubinafsi na hiyo ni sifa kuu ya binadam. Sema hapo kwenye ubinafsi kuna wengine wana roho mbaya. Uchagani kuchangishana kwa ajili ya ujenzi wa shule au kutengeneza barabara ni vitu vya kawaida kabisa. Huyo mtu kawa waziri miaka mingapi?
 
Hakuna zawadi kubwa mtu aliyopewa na Mungu kama akili, hekima ni kitu bora sana! Wachaga walijitambua mapema sana. Haikuwa shida kwa wakoloni kuwabeba sababu walibebeka. Ona kama mjomba wetu alivyo jaa majigambo na ujuaji hivi ni nani mwenye akili zake atamsaidia!? Tunajifunza kwa walioendelea hiyo piga ua aliye kutangulia kakutangulia tu.
Dhambi ya umimi ndiyo iliyomuangamiza Ibilisi. Naona na wewe unapiga mahesabu kama ya kwake ya umimi a.k.a Usisi

Unamsema Magu wakati wewe mwenyewe ndiyo walewale. Na sijui falsafa ya kusema "wakoloni waliwabeba watu wa kada fulani sababu walibebeka" sijui umetolea wapi. Kama wewe ndiye unayesema ni miongoni mwa mliyobebeka basi kapitie tena makabrasha yako kuhusu hiyo statement.
 
Hivi agenda za namna hii bado zipo nchi hii? Tuna kazi kweli kweli
 
Tofauti kubwa ya kimaendeleo katika maeneo ya Tanzania, kanda au mikoa ni kwa sababu ya madhara tulioridhi kwa mkoloni, tofauti ya kitamaduni na uzembe wetu. Sidhani kama kuna wakati bajeti ya nchi ilipangwa kwa upendeleo. Bajeti ya nchi inakuwaga wazi. Je kuna wakati wowote nchi hii iliwahj kuwa na upendeleo wa kibajeti?
 
Watu wenye element za ubaguzi kama hizi ni hatari sana kwa sababu wanaweza kuja kuwa viongozi na kuwaumiza wananchi wasio na hatia. Sumaye alikuwa WM kwa muongo mzima, amemaliza matatizo ya Hanang'? Hanang' hakuna ufukara? BWM alikuwa rais kwa muongo mzima. Hakuna ufukara Mtwara? au hata hiyo Kilimanjaro, hakuna ufukara? wale wamama wananaotuuziaga nyanya na vitunguu kwa lazima pale njia panda ya Himo ni matajiri? Wamachinga kibao pale stand ya Moshi wanatoka Mtwara? Nchi hii kuna maeneo yenye ahaueni tu kuliko mengine. Sio kitu cha kuhalalisha tabia ya wanasiasa kufanya mambo ya ajabu ya kifahari. Badala ya Airport na Hifadhi ya Wanyama, viongozi wangepeleka maji, umeme, mikopo bila riba, shule bora, vituo vya afya kila kijiji, masoko ya pamba nk
 
Dhambi ya umimi ndiyo iliyomuangamiza Ibilisi. Naona na wewe unapiga mahesabu kama ya kwake ya umimi a.k.a Usisi

Unamsema Magu wakati wewe mwenyewe ndiyo walewale. Na sijui falsafa ya kusema "wakoloni waliwabeba watu wa kada fulani sababu walibebeka" sijui umetolea wapi. Kama wewe ndiye unayesema ni miongoni mwa mliyobebeka basi kapitie tena makabrasha yako kuhusu hiyo statement.
Mkuu hatubishani nataka nikuambie Nyerere kama asinge pewa upendeleo na wakoloni hivi leo asingekuwa baba wa taifa. Wakoloni ndiyo wanajua nini kwanini walipa Nyerere na siyo wale wanzilishi wakudai uhuru.
 
Hii ya Chato ni mbaya! Lakini kwa nini hatuko tayari kulaani yote yaliyotokea na yanayotokea nchi hii?

Ukiamua kutetetea tuuuu hapo ndo tunasema wengi tunafurahia upendeleo unaotufikia kwa neema. Tunalazimisha kutumia hata takwimu zisizokuwepo na hasa hilo la elimu. Hapa TZ Wilaya pekee inayoweza kujivunia wasomi wa kiwango cha juu kabisa kuliko wilaya yoyote nyengine ni Ukerewe. Nasema tena Ukerewe na hiyo inafahamika. Kwa nini hawakujaa juu kote? sema jingine tu!

Kusoma kwa miaka ile, usiwape pongezi wazee wa kichaga, toa pongezi kwa wamisionari, hata Ukerewe ni hilo!
Mbona uchagani mmependelewa barabara lami Hadi Migombani wakati Kigoma na Katavi hakuna mtandao mkubwa was lami?
 
Mtu kwao mkataa kwao mtumwa iyo ni nature ya binadamu yoyote Mimi unipe urais ata kwa wiki2 SGR, MFUGALE,DARAJA LA KIGAMBONI na Flyover zote zitaamia kwetu matombo morogoro ikiwa tangu uhuru adi leo ata baiskeli haiwezi kufika.
 
Hakuna mikoa ambayo inahitaji kuendelezwa kuliko huko kwa JPM???...mnhhh eti usawa??? mambo yote yanayofanyika Chato ni usawa?? you must be blind my friend...
Kwani wakati huko uchagani wanajenga barabara hadi migombani hawakujua kuna sehemu kama singida hawana stand?Hawakuona maeneo potential mengine zaid ya huko?
 
A
Sasa huko Geita ndugu zake Magufuli wakiwaona WAZUNGU wana timua mbio na kujificha wakiogopa kuadhirika kwa Kiingereza..!!!
Wewe unafikri kwanini Rais wako Magufuli anakaribia kumaliza muhula wa kwanza bado hajakanyaga nchi hata moya ya Ulaya???Kiingereza bhana ni shiiiiida kwa Wasukuma...!!.

Williamson Diamond alipofika Mwadui Shinyanga akakuta wazee wa Kisukuma wanacheza BAO kwa kutumia ALMASI..!! Mzungu chapuchapu akaenda kununua GOLOLI(sparkling glass materials) akawaambia hizo ndizo zinawafaa na akakusanya madini yote ya Almasi akaondoka nayo....!! Ndiyo maana hadi leo Shinyanga, Mwanza na Geita bado ni Mikoa maskini pamoja na kuwa kwenye maeneo ya MADINI....na bado wazungu weusi wa CCM wamerithi yaleyale ya kina Dr. John Williamson kutoka Canada aliyewatapeli wazee wa Kisukuma...!!
Acha kuleta hadithi za sungura na fisi waliouza bagamoyo ni wasukuma?
 
Je watanzania wote kama walimu, madaktari, wahandisi, wakurugenzi, waandishi wa habari, wakuu wa mikoa na wilaya, makatibu wakuu, na makamishna, mawaziri waanzesasa kufikiria kupendelea kwao? Hivi kama kiongozi anaonyesha mfano gani kwa subordinates wake!!

Tumekuwa mara nyingi sana tukitetea eti ni watendaji wake, kweli na hili ni watendaji wake!!!

Sina uwezo wa kupendelaa kwetu kwa kujenga barabara au airport lakini nawezafanya kitu fulani japo ni kidogo. Je, mimi mwalimu niendelee kufundisha kwa bidii huku usukumani wakati kwetu ni Morogoro!!!

Najiiuliza itakuwaje kama kila mtanzania akiwa na mawazo ya kupendelea kwake hii itakuwa nchi!!! Je, tutabaki na nchi inayoitwa Tanzania au mikoa na vijiji. Sio kila mtanzania lazima ajenge uwanja wa ndege kwako lakini kwa nafasi ya kila mmoja anaweza kufanya kitu fulani.

Ewe mtanzania mwenzangu uwe wakujisajili kama line ya simu, uwe wa kuzaliwa, uwe wa kufikirika ambapo hata kuonyesha kaburi la babu ya babu yako huwezi, sote tuungane tukemee jambo hili linamadhara makubwa kwetu kama Taifa.
 
Back
Top Bottom