Sisi ndio tutakaoteseka kama mambo yataendelea kama yanavyoendelea sasa hapa nchini. Kwa kweli tumerudi nyuma mno kwenye masuala ya uongozi na usimamizi wa utendaji wa watumishi wa serikali na rasilimali zetu.
Huu ndio wakati muafaka sana kwa viongozi wa upinzani kuungana na kuwa sauti moja kusaidia kuwaunganisha watanzania kuinusuru nchi yao.
Kama mambo yataendelea hivi tutaishia pabaya muda si muda. Viongozi wasifurahie kuona wanachi wamekaa kimya tu, hakuna kitu kibaya kama mtu akaaye kimya baada ya kudhulumiwa.
Watanzania tunahitaji kufanya kitu hata kama ni kuonesha kutoridhishwa kwetu kwa kuandika ama kwa jinsi yoyote kwani sisi ndio tutakaoteseka na hali hii inayozidi kuwa mbaya.
Mungu inusuru nchi yetu na watawala wasiojali hali za wananchi na kuangalia maslahi yao tu.