Mimi nakubaliana na Mangula, tunahitaji SOKOINE mwingine Tanzania halafu pawe mshike mshike nguo chanika.
Sokoine sio tu alikuwa jasiri wa kusimamia maamuzi ya serikali bali pia alikuwa creative. Nakumbuka Watanzania walivyokuwa wajinga, wanakufa njaa, kisa NMC hawana uwezo wa kusaga mahindi yaliyojazana. Akatoa amri moja tu, wauzieni wananchi mahindi, watajua wenyewe watakakosaga. Baada ya miezi sita mashine za kusaga mahindi zikatapakaa Dar nzima, njaa ikapotea. Hiyo ndio creativity tunayotaka kutoka kwa viongozi wetu. Leo mtu anaweza kuona hilo kama jambo dogo, wakati ule lilikuwa kubwa, ingekuwa kwa wenzetu angeweza kupata prize kwa kuja na idea mpya na ambayo imefanya kazi.
Pia nakumbuka matatizo ya UDA, Sokoine akatembelea vituo, akaona wananchi wanavyosumbuka, huku vidaladala vinajificha kuogopa polisi. Akatangaza bila hata kutaka ushauri wa Mwalimu, ruhusu daladala ili wananchi wasipate usumbufu. Tamko hilo moja likaua usumbufu mkubwa kwenye usafiri.
Jamaa alikuwa anajua madaraka yanayoongozana na yeye kuwa waziri mkuu, alikuwa haangalii upepo wa mwalimu, yeye alikuwa anafanya kile anachoona kinafaa kwa taifa letu.
Sasa hawa mawaziri wakuu sijui Pinda, Sumaye naona sifuri kabisa. Afadhali hata Lowassa
kama isingelikuwa tamaa zake za utajiri na unyang'au wake.
I wish kuna Sokoine mwingine kajificha sehemu na anasubiri nafasi yake. TZ tuna viongozi wababaishaji wengi sana.