Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Huyu Mangula akae kimya tu apumzike huko aliko. Yeye ni mmoja wa waliolea hiyo rushwa hadi kufikia kiwango cha sasa ambacho kimeota mizizi. Angeiwahi ingali changa katika kipindi chake, isingekomaa kiasi hicho.
 
Kwakweli pamoja na ufisadi na rushwa kushamiri wakati wa uenyekiti wa fisadi mkapa na katibu wake Mang'ula, tumtendee haki mzee Mangula - sijasikia kuwa aliwahi kutoa au kupokea rushwa.

Hata baada ya kutoka ukatibu mkuu wa CCM, hajaandamwa na kashfa zozote za ufisadi uwe wa fedha, ngono wala lugha chafu. Amemaliza muda wake akaamua kurudi kwao kulima. Tumeona hilo kwa mwalimu Nyerere, na sasa Mzee Mangula. Pengine Sokoine angekuwa hai naye angerudi kijijini.

Tumlaumu Mangula labda kwa udhaifu wake wa kutokemea hadharani ufisadi, lakini mwenyewe Mangula binafsi alistahili kuitwa "mr. clean" na wala siyo boss wake fisadi mkapa.
 
Tumlaumu Mangula labda kwa udhaifu wake wa kutokemea hadharani ufisadi...

Na hii Mkuu Share ni dhambi kubwa sana ambayo uzito wake unaweza kulingana na waliofanya ufisadi. Alikuwa na nafasi ya kukemea maovu lakini akaamua kunyamaza na kuwaangalia watanzania wenzake wanaumizwa
 
Your motto , mkuu Mpita Njia, answers it all: That is; The aim of an argument or discussion should not be victory, but progress Happy New Year 2009 mkuu.
 
BAK, pole sana kumbe nawe yalikukuta kama yaliyonikuta mimi jana kila nikiingia Raia mwema inanipeleka Toleo Na 1. Sijui walikuwa na matatizo gani. Lakini naona wamerekebisha. Hii stori ya October 2007 Ila umeileta jamvini muda muafaka kwani bado ni ya moto kabisa. Inaendana na matendo yanaoendelea leo ndani ya CCM na Bongo.

Jamaa aliona mbali, ila kwa nini alipokuwa kiongozi hakutumia nafasi yake kuyatekeleza haya anayo yasema leo?http://raiamwema.co.tz/index.php?d=1
 
Sipendi sana kuchangia kwenye siasa kama hizi za Mangula lakini kwa hili itabidi nichangie tu.

Mchango wangu kwa Mzee Mangula ni kwamba ninamshauri akae kimya ili historia iweze kumhukumu badala ya kuanza kujieleza kwa yale ambayo yeye alipaswa kuyafanya huko nyuma akiwa kiongozi mkuu kwenye chama kilichoshika serikali. Hayo yote ambayo anayalalamikia ni uzao wa yale aliyoyalea wakati wa uongozi wao. Ili aeleweke vizuri angetubu makosa yake aliyoyafanya kama kiongozi badala ya kulalamika kama ambavyo anafanya sasa hivi.

Hebu tujiulize kama hali ni mbaya kama ambavyo anavyodai yeye, je kama angeupata uenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa angeongea nini leo hii?

Mzee mangula watu wanaona mbali hebu angalia nafasi yako sasa ni ipi na wala si vinginevyo.
 
Mchango wangu kwa Mzee Mangula ni kwamba ninamshauri akae kimya ili historia iweze kumhukumu badala ya kuanza kujieleza kwa yale ambayo yeye alipaswa kuyafanya huko nyuma akiwa kiongozi mkuu kwenye chama kilichoshika serikali. Hayo yote ambayo anayalalamikia ni uzao wa yale aliyoyalea wakati wa uongozi wao. Ili aeleweke vizuri angetubu makosa yake aliyoyafanya kama kiongozi badala ya kulalamika kama ambavyo anafanya sasa hivi.

aachwe aseme. anaweza kuwa na mengi ya busara na maana ambayo tunaweza kuyatumia kupunguza matatizo tuliyonayo.

tunapokuwa na matatizo tuombe na tupokee michango ya mawazo ya kila mtu na kila kundi. tuyatafakari na tukiona yana maana tuyafanyie kazi

kwamba hakukemea akiwa madarakani inaweza kuwa ni kwasabau ya kumuogopa aliyemweka pale.
lakini kuna wengine huona zaidi uhalisia wa mambo wanapokuwa pembeni.
 
Your motto , mkuu Mpita Njia, answers it all: That is; The aim of an argument or discussion should not be victory, but progress Happy New Year 2009 mkuu.

nashukuru sana mkuu, nawe ubarikiwe pia katika mwaka mpya
 
aachwe aseme. anaweza kuwa na mengi ya busara na maana ambayo tunaweza kuyatumia kupunguza matatizo tuliyonayo.

tunapokuwa na matatizo tuombe na tupokee michango ya mawazo ya kila mtu na kila kundi. tuyatafakari na tukiona yana maana tuyafanyie kazi

kwamba hakukemea akiwa madarakani inaweza kuwa ni kwasabau ya kumuogopa aliyemweka pale.
lakini kuna wengine huona zaidi uhalisia wa mambo wanapokuwa pembeni.

Itakuwa vema aandike kitabu ili kuweka kumbukumbu sawasawa akielezea ni jinsi gani alivyoboronga, lakini hili la kuongea na waandishi kesho na keshokutwa akirudishwa kwenye ulaji atakataa kuwa aliongea hayo anayoyasema.

Ni vema akaandika kitabu na kuelezea uozo alioufanya huo ndio ustaarabu, vinginevyo yeye ni sehemu ya matatizo ya rushwa ambayo tunaiona leo hii.
 
Hii habari kumbe ni ya mwaka juzi. Lakini bado inaonesha kuwa naye anajionesha udhaifu wake, uongoze miaka 10, tena ndio ulikuwa wakati Takrima inaruhusiwa, uje useme CCM inahitaji kiongozi kama Sokoine.

Ina maana hakuna viongozi safi CCM?, na kama wapo wachache.....
 
Mimi nakubaliana na Mangula, tunahitaji SOKOINE mwingine Tanzania halafu pawe mshike mshike nguo chanika.

Sokoine sio tu alikuwa jasiri wa kusimamia maamuzi ya serikali bali pia alikuwa creative. Nakumbuka Watanzania walivyokuwa wajinga, wanakufa njaa, kisa NMC hawana uwezo wa kusaga mahindi yaliyojazana. Akatoa amri moja tu, wauzieni wananchi mahindi, watajua wenyewe watakakosaga. Baada ya miezi sita mashine za kusaga mahindi zikatapakaa Dar nzima, njaa ikapotea. Hiyo ndio creativity tunayotaka kutoka kwa viongozi wetu. Leo mtu anaweza kuona hilo kama jambo dogo, wakati ule lilikuwa kubwa, ingekuwa kwa wenzetu angeweza kupata prize kwa kuja na idea mpya na ambayo imefanya kazi.

Pia nakumbuka matatizo ya UDA, Sokoine akatembelea vituo, akaona wananchi wanavyosumbuka, huku vidaladala vinajificha kuogopa polisi. Akatangaza bila hata kutaka ushauri wa Mwalimu, ruhusu daladala ili wananchi wasipate usumbufu. Tamko hilo moja likaua usumbufu mkubwa kwenye usafiri.

Jamaa alikuwa anajua madaraka yanayoongozana na yeye kuwa waziri mkuu, alikuwa haangalii upepo wa mwalimu, yeye alikuwa anafanya kile anachoona kinafaa kwa taifa letu.

Sasa hawa mawaziri wakuu sijui Pinda, Sumaye naona sifuri kabisa. Afadhali hata Lowassa
kama isingelikuwa tamaa zake za utajiri na unyang'au wake.

I wish kuna Sokoine mwingine kajificha sehemu na anasubiri nafasi yake. TZ tuna viongozi wababaishaji wengi sana.
 
Mangula: CCM yahitaji Sokoine mwingine

“Tatizo linalokipata chama chetu, ni kwamba wajumbe hawa wa mikoa, wanaoomba ‘soda’ kutoka kwa wagombea, ndio hao hao wanakwenda kushiriki katika chaguzi za ngazi ya taifa.

“Huko pia hujifunza kutokana na rafu wanazozifanya viongozi wanaowania uongozi wa kitaifa. Wanarudi na dhambi ya kutaka ‘soda’ kwenye maeneo yao. Huu ni ugonjwa.” anasema.

Hii ni hatari kubwa na viongozi wa dini mnaokipigia debe CCM mulione hili. Ama kweli leo nimeamini kuwa Watanzania tuko tabuni kwani hawa ndio wateule kutuongoza. Kauli kama hizi za Mangula zinatisha kwani zinaonyesha jinsi wenye madaraka wanavyokaa kimya wakiona na kushiriki vitendo viovu na huamuwa kuviweka wazi pale tu wanapokosa madaraka.

Swali kwa Mangula; Unataka kurudi kwenye uongozi wa CCM unayosema wewe mwenyewe kuwa ina vitendo vichafu, Kwanini? Kama ulishindwa kukemea na kukisafisha CCM ukiwa Katibu Mkuu utaweza kufanya hivyo kwa nafasi ya chini? Au ni hivyo tena kipofu haachi mkongojo wake, unataka urudi ukafaidi hicho kamchezo?
 
Ngekewa,

Hayo ni matatizo ya Tanzania nzima, vyama vyote vya siasa, vyama vya michezo na jumuia zingine.

Rushwa ni cancer kwenye system ya uongozi Tanzania.

Sidhani kama kuna kiongozi wa siasa Tanzania ambaye anaweza kusema amepata madaraka bila rushwa yoyote. Labda kinachotofautiana ni ukubwa wa hiyo rushwa. Hata uchaguzi waTFF juzi kulikuwa na rushwa.

Vita vya uhujumu uchumi vilikuwa kama rushwa kwenye uchaguzi kwasasa. Lilikuwa ni tatizo kuanzia chini mpaka juu.

Kama hili tatizo lingelikuwa CCM peke yao ingelikuwa rahisi mno kulimaliza, lakini kwa Tanzania ninayoiona mimi hili ni tatizo la nchi nzima. Hao ambao sio mafisadi kwasasa ni kwasababu hawajapewa nafasi.

Mwalimu alituambia Mkapa alikuwa clean, Mkapa hakuwahi kuwa clean, alikuwa hajapata nafasi. Alipokuwa pale elimu alikuwa anachukua virushwa vidogo vidogo ambavyo ilikuwa sio rahisi kumfanya awe milionea. Alipopewa nafasi, akajichotea mpaka kuvimbiwa.

Kwenye hili la siasa inabidi kutafuta solution ya nchi na watu wake wote.
 
Kwa kweli CCM hii ya sasa inatisha. Hivi vyama kama CHADEMA wakati waq chaguzi zao kunakuwaga na rushwa pia? Au hawajawahi kufanya chaguzi? Nipeni jibu
 
Mangula wewe umeingia choo cha kike kwa kugombea uenyekiti mkoa hukujua hayo?mbona unasema ulikuwemo kwenye mchakato wa kuwaengua waliohonga chaguzi zilizopita?

Kwa mfumo gani au karipio gani zingefanya uchaguzi wa iringa uwe wa bila rushwa wakati ulijua nini wajumbe wamezoeshwa? Ulifuata nini? Au umesahau nini huko chamani?

Soma alama babu Mangula.....umechemka, kalime viazi ule kiinua mgongo chako na kutubu madhambi uliyaona na kuyatenda....happy new year...tuombe mungu twasubiri nani anaefuata kisutu maana mlolongo mrefu sana......
 
Mzee Mangula kabla ya yote tunaomba arudishe nyumba ya serikali aliyokopeshwa ilhali yeye hastahili kwani hakuwa mtumishi wa serikali.

Huyu ni bad loser tu hana jipya ajikalie huko alime viazi vyake anajiabisha tu.
 
..Sokoine alikuwa Waziri Mkuu, Mangula alikuwa Katibu Mkuu wa Chama.

..Waziri Mkuu ni mtu mdogo ndani ya Chama kulinganisha na Katibu Mkuu.

..haiingii akilini kwa Katibu Mkuu[mangula] ashindwe kusafisha chama chake, badala yake analilia chama hicho kipate Waziri Mkuu[sokoine] wa kukisafisha.

..labda Mangula alimaanisha ndani ya CCM kunahitaji kiongozi mwenye tabia na mwenendo kama ule wa waziri mkuu Sokoine. kama ni hivyo kilichomshinda Mangula kuiga matendo ya Sokoine ni nini?

..swali hilo hapo juu lilipaswa kuulizwa na mwandishi wa habari aliyemhoji Mzee Mangula.

NB:

..Mangula alikuwepo kwenye kamati ya ushindi ya uchaguzi mkuu ya Kikwete. alifanya hivyo akielewa fika mbinu alizotumia Kikwete kufikia kuwa chaguo la CCM.
 
- Mangula akubali tu yaishe, sisi huku taifa ngoma inogile maneno yote Kisutu, Sokoine hakupeleka mtu yoyote mzito Kisutu zaidi tu wauza Colgate, sasa CCM tunapeleka Kisutu mawaziri wa zamani ambao yeye alipokuwa katibu mkuu wao wa CCM hakuyaona madhambi yao, under current CCM waziri mkuu na mawaziri wawili wamelazimika kujiuzulu kukwepa sheria na sasa wako njiani kufika Kisutu pia, Mangula hajaona haya?

- Mkapa mkuu wa Mangula, ndio hivyo mguu mmoja ndani na mwingine nje kuelekea Kisutu, labda tuwaombe serikali waangalie nini mchango wa Mangula kwenye wizi wa Mkapa maana definetely he knows and did something as patner in crime!

Mangula jaribu kuja mjini sometimes maana unaonekana kupitwa sana na yanayojiri Kisutu, CCM at this point and time tunahitaji ushahidi kama wake Mangula kumharakisha Mkapa Kisutu sio maneno ya Sokoine maana ya sasa Sokoine cha mtoto, Feleshi noma tupu hata Sokione kasingiziwa sasa tunamsubiri Mama Meghji next, Mangula miaka 10 CCM hakuna lolote zaidi tu ya kulia lia huko pembeni, debe tupu bwana kwa kelele tu!

Wakulu Invisible na Halisi, tupeni dataz vipi wiki hiii zamu ya nani Kisutu?
 
Back
Top Bottom